Marafiki walimuonya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marafiki walimuonya Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Sep 1, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Marafiki walimuonya Kikwete

  Ansbert Ngurumo

  MWISHONI mwa mwaka 2005, baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani, baadhi ya watu waliokuwa karibu naye kikazi na kifamilia walimuonya.

  Walimpa onyo katika mfumo wa ushauri – kwa kuogopa ‘kumuonya’ rais; kwa maana baadhi yao walikuwa wateule wake na wasaidizi wake wa karibu, jambo lililowafanya kupima vema kila kauli waliyompa mkuu wao wa kazi.

  Ushauri waliompa rais ulihusu maswahiba wake wakuu, ambao baadhi ni wafanyabiashara maarufu, ambao walifikia hatua ya kutoa fedha kuchangia kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizompa Kikwete ushindi mnono.

  Walimwambia rais afanye awezavyo kuwaweka mbali marafiki zake katika masuala ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne, kwa maelezo kwamba: “Malengo na masilahi yao ya kisiasa yangeweza kuingiliana na kutuingiza kwenye matatizo.”

  Baada ya kuwasikiliza, Rais Kikwete alifanya mambo mawili. Kwanza, alifuta mpango wa kuwateua serikalini. Pili, hakukubaliana na ushauri wa kuwaweka baadhi yao mbali na serikali.

  Hadi mapema mwaka huu lilipozuka sakata la ufisadi wa Richmond, mmoja wa maswahiba wake alikuwa mmoja wa washauri wake wakuu wasio rasmi, na anasemekana alikuwa karibu naye kuliko hata baadhi ya mawaziri.

  Mmoja wa mawaziri wa Kikwete wakati huo aliwahi kusema mahali fulani kwamba wapo baadhi ya viongozi wenzake ambao wakitaka kuvuka utaratibu wa kimangimeza wa kuomba miadi ya kuonana na rais, wanamtumia swahiba wake huyo.

  Na mambo ya Richmond yalipozidi kuwa magumu, zikaanza kusikika tetesi kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba ndiye aliyeileta kampuni hiyo feki na kuitetea kwa mkuu wa nchi.

  Maelezo haya yalisaidia baadaye kueleza kwa nini Rais Kikwete alishikwa na kigugumizi cha kushughulikia wezi wa EPA na Richmond; na kwa nini amekuwa akitumia mifumo ya chama chake na serikali kujaribu kuwasafisha na kuwalinda watuhumiwa.

  Wanaokumbuka majibu yake aliposhauriwa amtose rafiki yake mwaka 2006, wanasema rais aling’aka kwamba asingeweza kufanya hivyo, kwani “Si utu kumweka mbali, kwani ametumia pesa zake nyingi kutusaidia sana katika mchakato mzima wa kampeni na uchaguzi…”

  Utu huu ambao rais aliusisitiza wakati ule, umemfunga mikono katika kuchukua hatua dhidi ya wezi wa EPA na Richmond – licha ya mamlaka makubwa aliyonayo. Na baadhi ya watuhumiwa, akiwamo swahiba wake huyu, wanadaiwa kumtisha rais kwa kusambaza maneno ya chini chini kwamba “akitugusa tu, naye tunamvua nguo.”

  Hata sasa, ambapo inajulikana wazi kwamba pesa hizi zilizowasaidia sana hazikuwa za wafanyabiashara hao, bali ni sehemu ya pesa zile zinazohusishwa na miradi na wizi huo, serikali imeshindwa kuchukua hatua kali, ikisingizia inaogopa kuvunja haki za binadamu.

  Inashangaza kwamba binadamu wanaolindiwa haki zao hawazidi 10, huku binadamu wanaodhulumiwa haki zao ni Watanzania milioni 40 wanaoathirika kwa wizi huo na matumizi mengine mabaya ya madaraka.

  Waliojua mazingira hayo mapema ndio walikuwa wa kwanza kutilia shaka hatua za serikali kuunda tume ya kuchunguza ufisadi wa EPA.

  Ndio waliokuwa wanatilia shaka muda mrefu wa tume hiyo kufanya kazi, huku ikiundwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi mwingine, uliowahusu watu wale wale.

  Walijua serikali inafanya mchezo mchafu wa kuchezea akili za Watanzania. Na kwa sababu hiyo, ndiyo maana wapo watu ambao wamekuwa wakitamka bila woga kwamba serikali ya wezi haiwezi kushughulikia wezi wale wale walioiweka madarakani!

  Baadhi yetu tulipotilia shaka uwezo, nia na umakini wa rais katika suala hili tulishauriwa na baadhi ya wasaidizi na mashabiki wake kwamba ‘tumpe muda.’ Tumempa muda, ameutumia vibaya.

  Sasa baada ya hotuba yake ndefu bungeni wiki iliyopita, tunaweza kujivuna kwa kuwa na viongozi wa aina hii? Tunaweza kumnasua Kikwete kwenye ufisadi wa EPA na Richmond? Je, sasa tunaelewa vema kinachozuia mikono yake kushika rungu tulilomkabidhi kuwatwanga wahalifu?

  Jambo moja ni dhahiri. Rais bado anatetea ‘utu’ ule ule ambao washauri wake walimwambia auweke pembeni mapema, akakataa.

  Kwangu, hii ndiyo tafsiri ya haraka ya kauli ya Rais Kikwete bungeni alipodai serikali inashindwa kuchukua hatua kali dhidi ya mafisadi kwa kuogopa kuvunja ‘haki za binadamu.’

  Ndiyo! Kwake, hawa ndio binadamu. Hawa ndio wenye haki zinazopaswa kulindwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Haki za Watanzania milioni 40 hazimo miongoni mwa ‘haki za binadamu!’

  Wala tusijiulize sana kwa nini serikali inayojidai kuwa ya ‘kasi mpya’ inatumia miezi kuchunguza ufisadi ulio wazi, halafu inakuja na matamko yasiyo na mashiko! Hatuna sababu ya kushangaa kwa nini hata baada ya nusu mwaka, inashindwa kutekeleza mapendezo ya kamati ya Bunge kuhusu ufisadi wa Richmond.

  Hii ni serikali goigoi ya kasi mpya, ambayo inasifika kwa kuomba ipewe muda, huku nayo ikitoa muda kwa wasiostahili; tangu pale Rais Kikwete aliposema anawafahamu wala rushwa, lakini anawapa muda wajirekebishe.

  Ilikuwa mwaka 2006. Leo, miaka miwili baadaye, bado hajaridhika kama wamejirekebisha. Analinda haki zao!

  Tusisahau kwamba ni huyu huyu ambaye katika mwaka huo huo (2006) alijitapa jinsi ambavyo anataka kuunda mabilionea wa Kitanzania.

  Bila shaka si kwa mabilioni yale yaliyochotwa CRDB na kusambazwa mikoani kwa jina la Mabilioni ya Kikwete!

  Hayo yameshasahaulika.

  Mabilionea waliodhamiriwa ndio hawa, hawa wa EPA na Richmond, wafadhili wa serikali. Halafu tunatarajia serkali ile ile itoe tamko kali na kuchukua hatua kali dhidi yao?

  Ikumbukwe kuwa serikali imetoa matamko juu ya EPA na Richmond baada ya muda mrefu wa maandalizi ya kutosha na upotoshaji wa hali ya juu kuhusu ufisadi unaoikabili serikali.

  Wamejaribu, lakini bado wameshindwa kutuhadaa kuhalalisha wizi wao. Hapo ndipo uwezo wa upotoshaji wa serikali ulipoishia.

  Na huu ni ushahidi mwingine kwamba tunaongozwa na watu wenye uwezo mdogo sana au wasio makini kabisa, au wasioitakia mema nchi hii!

  Wafanye watakavyo, watutenge katika makundi ya binadamu na wasio binadamu. Rais aendelee kuwa katika kuchukua hatua.

  Mwisho wa yote, ajue kwamba tunatambua kuwa anafanya hivyo makusudi, kwa sababu alipuuza ushauri aliopewa. Alionywa mapema, akapuuza. Haya ndiyo matokeo yake.


  ansbertn@yahoo.com
  +447853850425
  www.ngurumo.blogspot.com
   
  Last edited by a moderator: Sep 2, 2008
 2. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kila jambo lenye mwanzo mbaya na mwisho wake ni mbaya tena kuliko mwanzo sasa hawa jamaa ni siku tu watachinjwa kama kuku.

  Nguvu ya wananchi ni kubwa sana wanaweza wakaaamua otherwise ikawa mbaya sana hali ya nchi nafikiri hawa mabwana hawfikirii sana hili kwa makini kwani wamelewa madaraka na fedha. Anyway haya ni maono yangu yanayotishia amani ya nchi ikiwa hatua hazichukuliwi haraka.

  Kabla sijamaliza na kusahau kuna jamaa mmoja alishaniambia Tanzania ukiiiba fedha nyingi au mali yenye thamani sana jela si mahali pako bali wewe ni uraiani tu kwani ni senior citizen, utalindwa na kila kitu kinachofanana na hicho. Sasa tunaona kwa macho wazi wazi hili likidhihirika. Mbona mwizi wa kuku hukamatwa na ikiwezekana kesho yake anaanza kutumikia kifungo ama faini?

  Sheria za Tanzania zinatekelezwa kinyume na katiba sasa katiba ni ya nini? Mimi nafikiri hii ni shame upon us all especially wanasheria amabao nao wenyewe unethically ni washiriki wakuu wa mikataba ya kifisadi nk. Je tutafika?
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Fuatilia makala niliyo post ya conflict theory na utajuwa kwanini masikini wanachomwa moto kwa wizi wa kuku na mafisadi wana HAKI ZA KIBINADAMU.
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  CONFLICT THEORY

  The several social theories that emphasize Social conflicts have roots in the ideas of Karl Marx (1818-1883), the great German theorist and political activist. The Marxist, conflict approach emphasizes a materialist interpretation of history, a dialectical method of analysis, a critical stance toward existing social arrangements, and a political program of revolution or, at least, reform.

  In conflict theory there are a few basic conflicts.

  One of the basic conflicts in conflict theory is that of class.

  There are low and high ranks in class, and that gives a certain group more power over another group which causes conflicts.

  For the most part, when an individual is part of a high ranked class they usually own a lot of property.

  That means that if you are of a lower class, then you don't own as much property.

  This usually causes conflict on who owns the most property and what property one does own.

  In Marx's original conception, ownership of property was the most essential determinant of the class structure.

  On the other hand Weber thought that property ownership was only one factor determining class structure.

  Also, in the words of Jurgen Habermas, the conflicts of different social structures and classes provide the many motives it takes to create and preserve many patterns of culture.

  Another basic conflict in conflict theory is that of race and ethnicity. Much like in the class system, groups in this system are ranked by their prestige and power.

  This means that if a certain race or ethnicity has more education, prestige, and power then it is considered the better race or ethnicity which creates conflict.

  Another kind of conflict is that of gender. This type of conflict can be noticeable by the implication of a type of culture that is for men and a type of culture that is for women. Regions are another kind of conflict.

  This type of conflict is brought about by all of the different assumptions that people from one region have about people that are from another region. The regions could range from one country to another or one state/province to another.

  Lastly, there is the conflict of religion.

  The conflict of religion is itself quite stratified;

  even though there is a group of people belonging to each religion they are divided much like the social structure of classes.

  All of these groups seek to gain power and use it to reshape society the way they see it best. It seems that this is the determining factor in the ruling class.

  In conflict theory there are different modes of conflict. One mode of conflict theory is that of warfare and revolution.

  Warfare and revolutions take place phases due to the rocky “collations among a variety of social classes.” An example of warfare is that going on currently in Burma, where there is military versus population fighting for control over the country’s government.

  Another mode of conflict in conflict theory is that of strikes.

  Modern society has created a main social divider between workers and managers.

  When workers feel they have been treated unfairly, they go on strike to regain their right to power.

  Another mode of conflict in conflict theory is that of domination. Most social classes don't form their ideologies the same. Different groups will struggle in conflict over what they think is right, what the norms are, and their ideologies.

  Higher classes have more abstract ideologies, while subordinated classes that are much less to their advantage but still reflect the want in their own lives.

  The ideas of the ruling class are the ruling ideas, where the ruling material force is the ruling intellectual force.

  Competition.Competition over scarce resources (money, leisure, sexual partners, and so on) is at the heart of all social relationships.

  Competition rather than consensus is characteristic of human relationships.

  Structural inequality Inequalities in power and reward are built into all social structures. Individuals and groups that benefit from any particular structure strive to see it maintained.

  Revolution Change occurs as a result of conflict between competing social classes rather than through adaptation.

  Change is often abrupt and revolutionary rather than evolutionary War.

  Even war is a unifier of the societies involved, as well as possibly ending whole societies.

  In modern society, a source of conflict is power where by politicians are competing to enter into a system which upon they act in their self interest, not for the welfare of people.(
  www.findarticles.com)

  Conflict theory is based upon the view that the fundamental causes of crime are the social and economic forces operating within society.

  The criminal justice system and criminal law are thought to be operating on behalf of rich and powerful social elites, with resulting policies aimed at controlling the poor.

  The criminal justice establishment aims at imposing standards of morality and good behavior created by the powerful on the whole of society. Focus is on separating the powerful from have nots who would steal from others and protecting themselves from physical attacks. In the process the legal rights of poor folks might be ignored. The middle class are also co-opted; they side with the elites rather the poor, thinking they might themselves rise to the top by supporting the status quo.

  Thus, street crimes, even minor monetary ones are routinely punished quite severely, while large scale financial and business crimes are treated much more leniently. Theft of a television might receive a longer sentence than stealing millions through illegal business practices.

  William Chamblis in a classic essay “The Saints and the Roughnecks,” compared the outcomes for two groups of adolescent misbehavers.

  The first, a lower class group of boys, was hounded by the local police and labeled by teachers as delinquents and future criminals, while the upper-middle class boys were equally deviant, but their actions were written off as youthful indiscretions and learning experiences.

  Radical criminology or critical criminology is a branch of conflict theory, drawing its ideas from a basic Marxist perspective. For Karl Max (1818-1883), modern capitalist societies were controlled by a wealthy few (bourgeoisie) who controlled the means of production (factories, raw materials, equipment, technology, etc.) while everyone else (the proletariat) was reduced to the lot of being wage laborers.

  While Marx himself never really addressed in detail the criminal justice system’s specific role in keeping such a system in place, from his writings a radical tradition has emerged. From this perspective, certain types of crime take on a different character. Stealing can be seen as an attempt to take away from the rich. Eric Hobsbawn referred to the like as “social banditry.” Protest-related violence may actually be the start of proto revolutionary movements, ultimately leading to a workers’ revolt and the establishment of a just society.

  At a minimum this perspective aids in the explanation of certain actions; civil rights and antiwar protesters were being locked up in the 1960s because they threatened the established social order. The FBI and the CIA both directed efforts at monitoring such behavior. Thus, the law enforcement community had come down on the wrong side of those seeking social change.

  Scenes of police officers attacking civil rights protesters with dogs, clubs, and water hoses and police riots such as the 1968 Democratic National Convention in Chicago appeared on nightly television news.
  A number of other varieties of conflict theory have appeared since the 1960s. These include radical feminism, left realism, and peacemaking criminology. The latter two are attempts to tone down some of the rhetoric, and present a more balanced approach.

  Radical feminism focuses on the plight of women under capitalism. Male domination has been the norm, and women have been subject to it in the home and workplace, as well as on the street. Radical feminist criminologists have looked at the unjust treatment of female teens, who are much more frequently subject to institutionalization for status offense violations (offenses that would not be criminal if an adult) such as running away from home, and particularly singled out for sexual deviance. While away from home or work alone, women must always be on their guard for potential attacks or advances from men.

  Living in fear has consequences, according to organizations such as Rape, Abuse, and Incest National Network (http://www.rainn.org/).

  Left realism emerged in the 1980s, partially as a response to the crime victims’ movement of that decade. Victims forced criminologists to recognize that the primary victims of crime are not the wealthy, but the poor.

  Most predatory crimes are not “revolutionary” acts; they are attacks on family members and neighborhood residents.

  As advocated by Stanley Cohen and others, left realists recognize that the criminal justice system must act to stop criminal victimization without regard to the class of the perpetrators. At the same time, continued focus on the crimes committed by the rich and powerful is warranted. White collar and business related crimes remain important.

  Peace making Criminilogy sought to expand the role of the discipline by looking at international issues such as war and genocide. International struggles for human rights and universal social justice are related foci of concern. Hal Pepinsky and Richard Quinney are major authors in this area. In addition, there are a number of not for profit non-government organizations (NGOs) involved in efforts such as these. For example, Witness (http://www.witness.org/) gives video cameras and photographic equipment to victims of government abuse and civil strife and asks them to document their experiences. These are then shared via the World Wide Web so that other can witness what is happening.(www.criminology.fsu.edu)
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  Kiongozi aliyeingia madarakani kimezengwemizengwe kupitia kwenye mtandao wa kifisadi kamwe hawezi kuwashughulikia mafisadi hao waliomuweka madarakani kwa kuogopa kuadhiriwa na mafisadi hao. Nafuu ya nchi yetu itapatikana pale Watanzania bila kujali itikadi zetu tutakaposimama kidete kuhakikisha huyu kiongozi asiye na uwezo haruhusiwi tena kusimama katika uchaguzi wa 2010.
   
 6. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2008
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  A mentally fit President may defy this. Do you remember The Late great Mwanawasa? (RP). Chiruba thought he got his made man to be used for his interests.

  Chiruba said NO. If you favoured me for no merits then it is your problem, but I believe to be competent for the post. Independent for the post.

  Hawa wa ketu ni kujidekeza tu!
   
 7. C

  Chuma JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bubu...Tatizo si Kikwete ni Mfumo Mzima....We need overall Change....Who is Clean in CCM?
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  ni kubadili katiba ambayo pia Warioba na Butiku wameshalipigia debe la kuwa na katiba mpya. Hawa mafisadi waliokuwa madarakani hawatakubali hilo kwa madai kwamba katiba haina kasoro. Sasa tunachoweza kukifanya kwa wale wenye mapenzi ya kweli na Tanzania ni kumpinga huyu jamaa kwamba hakustahili kuingia madarakani 2005 na hastahili kuendelea kuwepo madarakani baada ya uchaguzi wa 2010. Tukifanikiwa hilo basi naamini kabisa tutaweza kuubadilisha mfumo mzima.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  Kubadili mfumo ni kubadili katiba ambayo pia Warioba na Butiku wameshalipigia debe la kuwa na katiba mpya. Hawa mafisadi waliokuwa madarakani hawatakubali hilo kwa madai kwamba katiba haina kasoro. Sasa tunachoweza kukifanya kwa wale wenye mapenzi ya kweli na Tanzania ni kumpinga huyu jamaa kwamba hakustahili kuingia madarakani 2005 na hastahili kuendelea kuwepo madarakani baada ya uchaguzi wa 2010. Tukifanikiwa hilo basi naamini kabisa tutaweza kuubadilisha mfumo mzima maana usukani utakuwa umeshikwa na wananchi badala ya kushikwa na mafisadi.
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Haya yametokea Shinyanga baada ya mtendaji wa Kata kutumia "haki za binaadamu" na kuwaachia huru watuhumiwa!

  Jamani Kikwete jirudi na ufute kauli yako ya kiburi na hata hayo majisifu uliyopewa na Dr. Khan wa IMF yatakuwa angamizo kwako.

   
 11. M

  Mutu JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu Rev. Kishoka
  Haaaaaaaaaa kwa hiyo OFISA Mtendaji wa Kijiji kawaachia majambazi kama rais alivyofanya ili haki za binadam zisivunjwe ila yeye alikutana na walume wamemtoa uhai.

  Hii inafundisha kuchukuliwa watu hatua za kisheria watu wataheshimu sheria ,ila serikali ikishindwa kufamnya hivyo wanainchi wanachukua hatua wenyewe either kwa muhusika ama kwa wewe uliyemwajia maan si ndio kama umemuwekea dhmana.Tehe tehe tehe.
   
 12. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  REV,

  Unahofia wananchi kuchukua sheria mikononi mwao?. TZ bado sana hilo. Watauwawa vibaka tu.
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Sihofii wananchi kuchukua hatua mikononi, bali naonyesha ni jinsi gani sheria zinapovunjwa na viongozi, athari zake ni hizo watu kujiamulia mambo!
   
 14. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sheria miguuni au mikononi si jambo bado hata kidogo ni nyakati tu na upeo wa wananchi wakiisha kuwa well informed kinachofuata ni kutaka what they deserve and by principle kama kuna mtu anaweka mizengwe iliyopinda wanainyoosha. Kwani huoni ni matokeo ya nyakati tunaihoji sasa hivi serikali tukijaribu kuifanya responsible kwa wananchi? Ulifikiri itakuwa hivi 2 or 3 yrs ago? No. But now it is! We need to respect making timely precise decisions when granted leadership positions for the betterment of the citizens majority. Hii nchi ni ya wananchi bwana si ya mtu mmoja ama rais ama waziri ama fisadi ama mbunge ama mwanasheria mkuu ama mkuu wa majeshi ama askofu mkuu ama mtu yeyote unayemjua ambaye tunali[pa rent ya kukaa nchini, they need to be responsible to us all and all for US. We need to rethink and reconsider this!
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inaelekea Muungwana ni mwanafunzi mzuri sana wa wananchi wake. Awali wananchi ndio walikuwa wanajichukulia sheria mikoni peke yao (na bado wanaendelea kufanya hivyo). Lakini katika hili la EPA, Muungwana naye ameamua kwuaiga wananchi wake kwa yeye naye kujichukulia sheria mkononi na kuamua kutoa msamaha
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  1.Dr.Shein lakini hana maamuzi
  2.Mizengwe Pinda lakini tuna hofu nae mafisadi wanamnyemelea.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Anaonekana kuwa hana maamuzi labda kwa sababu amebanwa, hajapewa hiyo nafasi ya kufanya maamuzi.
   
 18. I

  Iga Senior Member

  #18
  Sep 2, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ' Na kwa sababu hiyo, ndiyo maana wapo watu ambao wamekuwa wakitamka bila woga kwamba serikali ya wezi haiwezi kushughulikia wezi wale wale walioiweka madarakani!'
  www.ngurumo.blogspot.com


  SI HILO tu ni kwamba nchi inayoshindwa hata kuwa na sheria na taratibu zinazoheshimiwa na wenye daladala, madereva na makonda wao kweli utasema ina waziri husika na mkuu wa nchi anamuona waziri huyo ni sawa tu akipigwa na kiyoyozi ofisini pake badala ya kuonja machungu wananchi wenye kutumia usafiri wa umma wanaoupata?

  Kweli soko huru lakini hivi watu wanaweza kuachiwa kupandisha bei kiholela tu wakati tayari ziko juu mno ili kuwakomoa Waislamu wanaofunga hata hao wanaofanya hivyo wakiwa ni waislamu wenzao si wanastahili kwenda kufuturu dona ya mahabusu!

  Na hivyo chama tawala kinaweza kuwa na katibu mkuu mropokaji au mshauri wa kisiasa ambaye anadiriki kusema hadharani wataumaliza upinzani. Hivi ndivyo CCM inavyojenga demokrasia Tanzania.

  Dalili ya mvua ni mawingu ingawa sijui dalili ya mawingu ni nini. Hivi kwa hali kama hii hata tukiwa wapumbavu namna gani tunakubali kwamba kuudhofisha upinzani ni kheri kweli? Landa kama sisi ni mataahira au ndondocha na hatujui hata kama tuko hai au tumekufa!!

  Wenzetu huko Uchina hawa kina mafisadi wangelikwishakuwa chakula cha risasi muda mrefu.

  Tulidanganywa na bwamkubwa kwamba tusidhani tabasamu lake litakuwepo siku zote kwa wale watakavyofanya ndivyo sivyo. Kweli kanuna, lakini rohoni anacheka kwa kutukejeli Watanzania milioni 38 kwamba kuna watu katika nchi hii kama 10 au 30 hivi ambao ni bora kuliko Watanzania wote wakiwekwa pamoja; kwamba yeyote anayefanya madhambi kupitia mgongo wa chama au wanasiasa walioko serikalini hawezi kamwe kupatikana na kosa; na kwamba kwa kuwa sisi ni kondoo watiifu na waaminifu daima dawamu wakubwa wanaweza kufanya lolote na sisi tusiwe na jeuri ya kuwaambia komeni, acheni au ondokeni!

  NCHI hii ikipata viongozi wazuri inaweza kutajirika bila misaada toka nje. Na hizi sio siasa -uchumi njaa mababu wa CCM walizowaachia wajukuu wao. Sasa tunataka siasa za kiuchumi ambazo kwazo waziri anakula tokana na anachozalisha, katibu mkuu anakula kwa jinsi anavyolinda mali ya umma na watumishi wa umma wana malengo ambayo kwayo hutoa haki kutokana na mchango wa mtu na sio kila mtu kulipwa tu iwe kafanya au hakufanya kazi; au mtu kafanya kazi vizuri mno na kaliingizia taifa pato la haja analipwa sawa na yule anayengoja kula kinachozalishwa tu! Kama mmeua ujamaa basi uweni na mabaya yake au sio!

  Serikali ya kasi mpya imegeuka serikali ya mwendo wa konokono ambako waziri wa afya anashindwa kusimamia hata mradi wa chanjo ipasavyo; serikali ya nguvu mpya, imegeuka serikali ya nguvu ya kuhangaika na yasiyochangia maendeleo ya nchi na watu wake; serikali ya ari mpya imegeuka serikali ya ari ya kulinda uchafu wa kisiasa na ufisadi na madhambi ya wenzetu na jamaa zao!

  Hivi Rais wa nchi hawezi kweli kwa kulitumia bunge lake na katiba yao ya viraka kuzifanya sheria ziwalinde wananchi. Basi kule kuapa kulinda haki za wanachi anakufanya kwa namna gani. Na kama kiongozi hawi mlinzi wa haki zetu nani atakuwa mlinzi wa haki zetu. Na maneno ya demokrasia kuwa wengi wape kwake sivyo bali ni wachache wape????

  Tuelewe kwamba ukisikia bilioni 10 wamepewa sijui CRDB au NMB tambua kuna milioni 10 zimekwenda kwingine na katika hesabu hutaona ndani! Na fedha hizi njugu zilivyogawa mbona hatupewi ripoti kwamba zimewawezesha wananchi kwa kiasi gani au ndio zimetumbukia kwenye shimo lisilo na mwisho.

  Tunawaomba wafadhili WAPENI WATANZANIA MSAADA MOJA KWA MOJA na siyo serikali yao tu; na barabara na madaraja jengeni wenyewe hakuna cha kuingiliwa mambo ya ndani hapa. Maana kinachotokea ni kwamba mkiipa serikali bilioni 1 basi nusu yake inakwenda kujenga mahekalu na kuwekwa nchi za nje kwa faida ya watoto na wajukuu ambao hata bado hawajazaliwa!

  Hakika wema na wazuri hawajazaliwa!
   
 19. I

  Iga Senior Member

  #19
  Sep 2, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeangalia kwenye kamusi ya Kiingereza ninaambiwa kwamba serikai ya wezi inaitwa KLEPTOCRACY.

  Ni muhimu kutambua kwamba kuna njia nyingi za mtu kuiba ikiwa ni pamoja na mwajiriwa wako [wabunge, mawaziri na watumishi wa serikali] kujichukulia magari ya fahari yanayokula mafuta sawa sawa na bei ya kununua kila mwaka; kujikopesha na kujijengea majumba ya fahari; misururu ya watu 40-50 kwenda safari za nje kila mwezi; kulipwa mishahara huku wameshindwa kuzuia mianya ya wizi na ufisadi; kulindana na kuenziana kama kawa!
   
 20. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi bado hamjashituka tu????. anawatumikia waliomchagua, kama mnafikiri mulimchagua mumepotea njia
   
Loading...