Habarini wakuu,leo nina kuja na mada tena kwa style ya swali kwa wadada zetu kama mkakati wa kuwarekebisha akina sisi tujue madahara ya tunachowafanyieni au kuwajeruhi kiroho katika sekta nzima ya mapenzi
Hivi mdada unajisikiaje yule jamaa/Mshikaji ambaye amekufukuzia sana kwa gharama kubwa,kwa muda wake mwingi then ulipokuja tu kufungua njia ukamuonjesha hadhina yako(kama vijana wengi wa mjini tunavyoamini uthamani wako uko hapo kati) then baada ya hapo tu unaona mwenzio anaanza kuonyesha Negative attitude yaani simu na meseji zinaanza kupungua dramatically ikiwezekana hadi uanze wewe ,anakulia cobs hata mkukutana ratiba hataki tena iwe faragha ,anakukwepa ,yale maneno matamu hamna tena (matured wananielewa) ,yaani jamaa hatamani hata kurudia tena yaani kama ukikuta nae kama vile hamjafanya(LOL) ,hata kuja kuku pick tena ndo basi....n.k
Sasa je wewe kama ndo imewahi/ulitokewa au utatokewa na hivyo nini hasa utahisi? Na kama itakutokea mara kadhaa hutajihisi balaa kweli au una kasoro?(Ukaoge maji ya bahari)
Na kwa upande wa pili,sisi wanaume ni kitu gani hasa(common) ambacho hukutarajia kilikusababisha utamani iwe kama haijatokea vile.....wakati ulikua unapigia misele kama mbwa mwenye njaa
Na Mwisho kabisa Je hii kitu haiwezi kuathiri mahusiano yako yajayo(future) yako wewe msichana?
Alamsiki Wasalamu,Nawasilisha