Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,908
- 7,752
Wakati Jana jumapili ya Tarehe 28.08.2016 waumini wa KKKT Mtwara wakiandamana kabla ya Ibada kushinikiza Mkuu wa Kanisa Dr. Shoo kupeleka timu ya wachunguzi watakaoshirikiana na vyombo vya uchunguzi vya dola kuchunguza Ufisadi uliokithiri unaofanywa na Askofu wa Dayosisi hiyo ndugu Mchungaji Lucas Mbedule, mazito yameibuliwa yanayohusu elimu yake Askofu huyo.
Askofu Mbedule anadaiwa kuwa ni mhitimu wa Kidato cha NNE aliyefeli.
Imeelezwa kuwa kabla hajafika kidato cha NNE, Askofu Mbedule alikuwa ni Darasa la Saba tu. Kwa kutambua umuhimu wa elimu katika nafasi kubwa kama hiyo, Mbedule aliamua kuanza kujikongoja ambapo alijiunga na masomo ya QT ambapo alifaulu na kuwa na ruhusa ya kufanya mtihani wa kidato cha NNE ambapo matokeo yalipotoka, Askofu huyo alifeli vibaya masomo yote likiwamo somo la Bible Knowledge ambalo alipata Alana F.
Hivi sasa Mbedule ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Tumaini Makumira, akidai anasoma masomo ya shahada ya kwanza ya theolojia huku wanaomfahamu wanasema anasoma Certificate ya Muziki.
Katiba ya KKKT dayosisi ya Kusini Mashariki anayoongoza Mchungaji Mbedule ilichakachuliwa kwa makusudi ili kulazimisha Mbedule kuwa Askofu. Katika kipengele kinachoainisha elimu ya Askofu, Mbedule alichakachua na kuandika 'elimu inayofaa' bila kusema elimu inayofaa ni ya kiwango gani.
Inaelezwa kuwa Mbedule amelazimisha kuwa signatory wa akaunti za Kanisa kuu ambapo amekuwa akifanya ufisadi mkubwa. Kanuni zinataka ili fedha itoke Benki, Hundi inatakiwa isainiwe na signatories wawili ambapo kwakuwa yeye muda mwingi anakuwa Arusha, huondoka Mtwara akiwa amesaini hundi nyingi ili akiwa Arusha anaagiza tu fedha isainiwe na mtu wa pili Kisa atumiwe yeye.
Wachungaji wa Dayosisi hawajalipwa posho zao za kila mwezi kwa muda mrefu sasa kwa kisingizio cha kutokuwepo kwa fedha.
Suala la elimu ya Askofu Mbedule limekuwa mjadala mzito sana Mtwara na inaaminika kuwa KKKT Ofisi kuu itachunguza kwa umakini elimu yake na na kuna kama anastahili kuendelea na wadhifa huo au la