Mapya yaibuka kuhusu baba wa diamond

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
SIKU chache baada ya baba mzazi wa kachala wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnum’, mzee Abdul Juma kufunguka kuwa mwanaye huyo hamthamini toka amepata mafanikio, watu waliodai wao ni ndugu wa tumbo moja na mkali huyo wa muziki wa kizazi kipya wameibuka na kusema baba mzazi wa Diamond alishafariki dunia mwaka 2004, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.
CHANZO CHATIRIRIKA
Baada ya habari ya kuibuka kwa baba wa Diamond kuchapishwa kwenye gazeti ndugu la hili (Amani) mwishoni mwa wiki iliyopita, chanzo makini kiliwatonya mapaparazi wetu kuwa baba aliyejitokeza (Abdul Juma) siyo wa damu.
“Jamani nyie Amani mmeandika baba wa Diamond ni mzee Abdul Juma, mbona tunavyojua sisi, baba wa Diamond anaitwa Salum Idd na alishafariki dunia tangu mwaka 2004, kama mnataka ukweli zaidi fuatilieni,” kilisema chanzo hicho huku kikiahidi kutoa ushirikiano.
MAPAPARAZI WAINGIA KAZINI
Mapaparazi wetu walianza kazi ya kufuatilia nyeti hiyo ambapo kwa msaada wa chanzo, Julai 12, mwaka huu walifanikiwa kutinga nyumbani kwa msichana aliyedai ni dada kwa baba mmoja na Diamond.
Msichana huyo anaishi Kariakoo, jijini Dar es Salaam na mdogo mwingine wa Diamond aitwaye Idd Salum ambaye naye anaimba kama kaka yake.
TUJIUNGE NA IDD ALIYEPO KARIAKOO
Baada ya salamu za hapa na pale na mapaparazi wetu kujitambulisha kwa familia hiyo, lilifuata swali kama kweli wao ni ndugu wa damu moja na Diamond.
Idd: “Mbona kila kitu kipo wazi, hata yule mzee Abdul Juma anaelewa kila kitu kwamba sisi na Diamond ni ndugu, Diamond ni kaka yetu na amekuwa akinisaidia mimi katika shida na raha, baba yetu alishafariki dunia tangu mwaka 2004.
“Yeye (Abdul) ni baba mlezi tu na anafahamu wazi kuwa yeye ni baba mlezi wa Diamond na kwamba baba yetu alishatutoka.”
IDD AIBUA JIPYA
Kwa mujibu wa mdogo huyo wa Diamond, Idd, mwaka 1989, mama Diamond (Sanura Khassim ‘Sandra’) alipewa ujauzito na Salum (baba yake) kisha waligombana na kuachana.
Akasema baada ya kuachana, mama Diamond alikutana na Abdul ambaye alikubali kuwa naye kimapenzi na kuulea ujauzito huo wa mtoto (Diamond).

KWA HABRI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: MAPYA YAIBUKA KUHUSU BABA WA DIAMOND
 
Matatizo haya ni ile dhanna ya bwana wa mama au mume mpya wa mama kumuita "baba" au jitu lisilo na uhusiano wowote na wewe kuliita "baba", mwishowe kila mtu anakuwa "baba". Wachungaji wa kondoo ma "baba", rais anakuwa "baba", mkuu wa kanisa "baba"! kila rafiki wa mama ni "baba"!

Tuwachaneni na hizi tamaduni za kijinga. Baba ni yule aliyekuzaa tu.
 
Mkuu sasa swala la makanisa limetokea wapi tena? Hivi huwa haiwezekani kujadili bila kuhusisha udini?
 
kama jamaa alimlea kama mwanae anayo haki yakuitwa baba.. Kazae mwanao umtekeleze afu akifanikiwa ukajidai ndo baba wakat kuna dume jengine limekusaidia kulea.. Diamond ataamua mwenyewe na busara zake, magazet wafanya biashara 2..
 
Nukta haziungani hapa! Mama kupewa ujauzito na Salum na kuachwa. Kisha anapata mpenzi mwingine, Abdul. Anasiyemulia kisa ni MDOGO wa Nasibu (wa baba mmoja). Ina maana mama alirudi tena kwa Bw. Salum na kupata ujauzito wa huyo mdogo? Au nijihesabu na mimi ni miongoni mwa wale wagumu kuelewa?
Kwa kawaida sipendi kufuatilia habari za namna hii lakini nimelazimika kutoa maoni yangu ili hili liwekwe sawa na ndipo "majaji" watoe hukumu ya haki.
Hata hivyo, huyo baba mlezi kama ni kweli alilea ujauzito na baadaye mtoto, ana haki ya kuitwa baba. Jamani, kuzaa sio kazi, kazi kulea mwana!
 
Aah magazet haya yanafuatilia mambo ya ajabu! Sijui kama Dimond asingekuwa maarufu wangefuatilia.
siunajua mambo ya ajabu ndiyo habari yenyewe??? hata wao huwa hawana habari na mtu asiye maarufu.
 
SIKU chache baada ya baba mzazi wa kachala wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnum', mzee Abdul Juma kufunguka kuwa mwanaye huyo hamthamini toka amepata mafanikio, watu waliodai wao ni ndugu wa tumbo moja na mkali huyo wa muziki wa kizazi kipya wameibuka na kusema baba mzazi wa Diamond alishafariki dunia mwaka 2004, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.
CHANZO CHATIRIRIKA
Baada ya habari ya kuibuka kwa baba wa Diamond kuchapishwa kwenye gazeti ndugu la hili (Amani) mwishoni mwa wiki iliyopita, chanzo makini kiliwatonya mapaparazi wetu kuwa baba aliyejitokeza (Abdul Juma) siyo wa damu.
"Jamani nyie Amani mmeandika baba wa Diamond ni mzee Abdul Juma, mbona tunavyojua sisi, baba wa Diamond anaitwa Salum Idd na alishafariki dunia tangu mwaka 2004, kama mnataka ukweli zaidi fuatilieni," kilisema chanzo hicho huku kikiahidi kutoa ushirikiano.
MAPAPARAZI WAINGIA KAZINI
Mapaparazi wetu walianza kazi ya kufuatilia nyeti hiyo ambapo kwa msaada wa chanzo, Julai 12, mwaka huu walifanikiwa kutinga nyumbani kwa msichana aliyedai ni dada kwa baba mmoja na Diamond.
Msichana huyo anaishi Kariakoo, jijini Dar es Salaam na mdogo mwingine wa Diamond aitwaye Idd Salum ambaye naye anaimba kama kaka yake.
TUJIUNGE NA IDD ALIYEPO KARIAKOO
Baada ya salamu za hapa na pale na mapaparazi wetu kujitambulisha kwa familia hiyo, lilifuata swali kama kweli wao ni ndugu wa damu moja na Diamond.
Idd: "Mbona kila kitu kipo wazi, hata yule mzee Abdul Juma anaelewa kila kitu kwamba sisi na Diamond ni ndugu, Diamond ni kaka yetu na amekuwa akinisaidia mimi katika shida na raha, baba yetu alishafariki dunia tangu mwaka 2004.
"Yeye (Abdul) ni baba mlezi tu na anafahamu wazi kuwa yeye ni baba mlezi wa Diamond na kwamba baba yetu alishatutoka."
IDD AIBUA JIPYA
Kwa mujibu wa mdogo huyo wa Diamond, Idd, mwaka 1989, mama Diamond (Sanura Khassim ‘Sandra') alipewa ujauzito na Salum (baba yake) kisha waligombana na kuachana.
Akasema baada ya kuachana, mama Diamond alikutana na Abdul ambaye alikubali kuwa naye kimapenzi na kuulea ujauzito huo wa mtoto (Diamond).

KWA HABRI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: MAPYA YAIBUKA KUHUSU BABA WA DIAMOND

diamond anaitwa Naseeb Abdul Juma, baba abnayesema ni baba mzazi anaitwa Abdul Juma. mdogo wake anaitwa Iddi salum na baba yake anaitwa Salum Iddi??????

hainiingii akilini kuona kama watu wanaweza kufuatilia hili wakati siri ya nani baba wa mtoto anayo mama. pia hapa kama huyu baba yake dimond alimtelekeza huyu mama mjamzit kisha akaja kukutana na huyu abdul salum diamond anachokataa kuwa siyo baba yake ni nani? na nani aliye mwabia kuwa wewe ulikuja mimba tu kwa huyu baba? na pia hao wadogo iweje wakazaliwe kwa yule baba ambaye walikuwa wameshatengana?

wenywe akili hapa tunagundua kuwa ni njia ya kudhalilisha wanawake na kuonyesha uchafu wa huyu mama diamond. Pia vidudu mtu ni wabaya sana mpaka mkajua alikuwa mimba wala hakutokea kwa huyo baba inawahusu mlimshkia miguu nyie achen upaparaz wa kipumbavu.

Diamond carry on na maisha yako, huyo baba kama yupo give him respect na mama yako mpe repect halaf mwambie mama asiseme lolote na hawa wakuda wanania ya kumdhalilisha tu. nimechukia sana.
 
Matatizo haya ni ile dhanna ya bwana wa mama au mume mpya wa mama kumuita "baba" au jitu lisilo na uhusiano wowote na wewe kuliita "baba", mwishowe kila mtu anakuwa "baba". Wachungaji wa kondoo ma "baba", rais anakuwa "baba", mkuu wa kanisa "baba"! kila rafiki wa mama ni "baba"!

Tuwachaneni na hizi tamaduni za kijinga. Baba ni yule aliyekuzaa tu.
Baba sio lazima akuzae.Na kwa kesi hii kama huyo diamond alilelewa toka akiwa mimba ni haki huyo kuwa baba yake..
 
Matatizo haya ni ile dhanna ya bwana wa mama au mume mpya wa mama kumuita "baba" au jitu lisilo na uhusiano wowote na wewe kuliita "baba", mwishowe kila mtu anakuwa "baba". Wachungaji wa kondoo ma "baba", rais anakuwa "baba", mkuu wa kanisa "baba"! kila rafiki wa mama ni "baba"!

Tuwachaneni na hizi tamaduni za kijinga. Baba ni yule aliyekuzaa tu.

Sasa kama mtu kalea mama na mimba yake, na anaishi na mamako, wewe ukazaliwa utamuita nani Zomba? anko? wakati ni mume wa mama yako? na anakulea wewe? Acha utani.. huyo ni baba yake .. tena kama anataka laana amdharau tu atakiona cha mtema kuni..
 
Kweli huyo ndio babaake maana alilea mimba iliyokataliwa, akamlea akiwa mdogo, suala kwamba kaachana na mama yake sasaivi sio sababu ya kutokuwa na shukrani na kumkana. anavyofanya ameibua hii aibu ya familia yao ilivyo na pia anajitafutia laana. Hata kama hana kitu muheshimu maana yeye alikupokea ukiwa umekataliwa ulipaswa kumjali zaidi. mama pia ni mbaya na limbukeni anamletea laana mtoto bure.
 
Back
Top Bottom