radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,450
- 32,293
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilidai ilimkamata mwekezaji wa Kiwanda cha Kiluwa Steel kilichopo Kiluvya wilayani Ubungo jijini Dar es salaam bwana Muhamed Kiluwa anayetuhumiwa kumpa hongo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi Dola za Marekani 40,000 (Sh. milioni 90.7) ili amsaidie kupata hati 20 za ardhi kwa kuwa zile 50 alizokuwa amepewa awali hazimtoshi katika uwekezaji wake ameachiwa kwa dhamana.
Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Takukuru Makao Makuu, Mussa Misalaba, aliiambia Nipashe jijini jana kuwa mwekezaji huyo aliachiwa kwa dhamana jana asubuhi.
"Leo (jana) asubuhi tumemwachia kwa dhamana. Uchunguzi unaendelea. Tulipomkamata alihifadhiwa kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay. Amepewa dhamana huko, sheria zinatubana kuendelea kumshikilia lakini suala lake tunaendelea nalo," alisema.
Misalaba hakuwa tayari kueleza kuhusu masharti ya dhamana ya mtuhumiwa huyo, hata hivyo.