Mapya anayetuhumiwa kumhonga waziri mil. 90/-

Mapya anayetuhumiwa kumhonga waziri mil. 90/-

Usikute Lukuvi kaamua kumchomekea hiyo jamaa ili azidi kupata kiki tuu.
Hawezi mtu kukujia akuambie kuwa nakupa $40,000 bila kuwa na mahusiano ya aina hiyo awali. Mwisho yatajulikana, sio kwa takukuru kuachia MTU kirahisi hivyo

True na sio huyu tunayemjua !!
 
Waziri Lukuvi anastahili pongezi ni mawaziri wachache sana wenye roho ya kusema NO!..wangelikuea ni wale mawaziri vivuli wangevuta asubuhi asubuhi.
 
Nimekuelewa Mkuu, lakini naomba usome tena neno kwa neno ulichoandika pale mwanzoni
Nilimaanisha na madiwani wanaojifanya kujiuzulu nao pia wanahongwa. So Nchi masikini Rushwa ni gonjwa la ukoma
 
Nachojiuliza huyo ndo wa kwanza kumfuata mh. waziri kutaka kumuhonga ??
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilidai ilimkamata mwekezaji wa Kiwanda cha Kiluwa Steel kilichopo Kiluvya wilayani Ubungo jijini Dar es salaam bwana Muhamed Kiluwa anayetuhumiwa kumpa hongo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi Dola za Marekani 40,000 (Sh. milioni 90.7) ili amsaidie kupata hati 20 za ardhi kwa kuwa zile 50 alizokuwa amepewa awali hazimtoshi katika uwekezaji wake ameachiwa kwa dhamana.

Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Takukuru Makao Makuu, Mussa Misalaba, aliiambia Nipashe jijini jana kuwa mwekezaji huyo aliachiwa kwa dhamana jana asubuhi.

"Leo (jana) asubuhi tumemwachia kwa dhamana. Uchunguzi unaendelea. Tulipomkamata alihifadhiwa kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay. Amepewa dhamana huko, sheria zinatubana kuendelea kumshikilia lakini suala lake tunaendelea nalo," alisema.
Misalaba hakuwa tayari kueleza kuhusu masharti ya dhamana ya mtuhumiwa huyo, hata hivyo.
Hapa Bahati nzuri kakata, lakini ingekuwa tofauti Na tunacho elezwa basi ni wazi nafasi ya mtu wa kawaida kupata haki ni ndogo saana . Na hapa ni katika ngazi ya juu ya wazuri ambaye amekata, lakini huko chini maafisa Ardhi wengine si watakuwa wamemuwekea faili vizuri hata Kwa kuwaumiza wengine
 
Usikute Lukuvi kaamua kumchomekea hiyo jamaa ili azidi kupata kiki tuu.
Hawezi mtu kukujia akuambie kuwa nakupa $40,000 bila kuwa na mahusiano ya aina hiyo awali. Mwisho yatajulikana, sio kwa takukuru kuachia MTU kirahisi hivyo
mod naomba mufunge hii thread. hio undelined ndio hitimisho
 
Back
Top Bottom