Mapungufu ya wazazi wetu na athari zake... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapungufu ya wazazi wetu na athari zake...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Jul 3, 2012.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Ukisikiliza watu weengi wanavyowazungumzia wazazi wao
  ni nadra sana kusikia wakizungumza in a negative way
  mara nyingi utakuta wanawasifia sana wazazi wao
  hata kwa vitu ambavyo hao wazazi walikuwa wrong

  mfano watu husifia ukali wa wazazi wao hata kama ukali huo ulikuwa unakuja
  na negative side nyiingi mfano abuses na kadhalika....

  utakuta mtu 'anawapiga wanae kipigo cha mbwa mwizi'
  huku akisumulia jinsi yeye alivyokuwa anapigwa na wazazi wake zamani alivyokuwa mdogo

  au mama anatukana watoto 'matusi ya nguoni' na ya kuumiza
  ukifatilia utakuta sijui shangazi fulani alikuwa hivyo au bibi alikuwa hivyo...

  in short kuna 'urithi' wa vizazi na vizazi wa mambo fulani ambayo watu huwa
  wana kawaida ya 'kujisfia' navyo kama sifa hivi....


  utasikia mtu akisema 'mimi baba yangu alikuwa hakubali upuuzi huu'
  kwa kitu ambacho pengine yuko wrong lakini amelelewa kuamini ni sahihi na yeye
  anaendelea nacho kwenye familia yake......

  sasa leo ningependa tujadii haya......

  umewahi kujiuliza kuhusu mapungufu ya wazazi wako?
  umewahi kujitazama na kuona kwa jinsi gani 'umerithi' mapungufu hayo?
  unaamini 'principles za wazazi wako kama zilivyo'?
  au uko tofauti kiasi gani na wazazi wako?

  je mkeo/mumeo amerithi nini hasa kutoka kwa wazazi wake ambayo unatamani asingerithi?

  je watoto wako una wa instill principles zako au unawaacha wa develop 'personality zao wenyewe?
  what if uko wrong?
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  very challenging.

  Kwanza, kurithi tabia ya mzazi inategemea mahusiano yako na mzazi yalikuwaje, kama yalikuwa mazuri hata tabia zake zitakufurahisha ziwe nzuri au mbaya.

  Ila kama mzazi hakuwa na maelewano na watoto, basi kila tabia yake itaonekana ina walakini

  japo kwa wazazi wenye mahusiano mazuri na watoto lazima at a certain point unajikuta unawafundisha/rithisha vitabia vyako hata kama haviko sawa.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  not necessarily iwe hivyo
  wapo watoto walikuwa wanawachukia baba zao kwa ulevi
  guess what....
  ukubwani na wao walaja kuwa walevi mbwa kuzidi baba zao

  upo utafiti ulifanyika ulionesha kuwa watoto wanaotoka
  kwenye familia ambazo baba alikuwa anampiga mama
  walikuja kuwa wanapiga wake zao
  licha ya kuwa walipokuwa wadogo walikuwa wanachukia na kulia wakati mama zao wanapigwa
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Fifty fity aisee

  wapo wanaorithi regardless walikuwa wanachukia kiasi gani, wapo ambao wanakuwa the opposite.

  Japo kuangukia kwenye trap ile ile ni rahisi sababu deep inside unajipa moyo kuwa japo kitabia hiki ni kibaya lakini kufanya ruksa sio 'taboo'
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  kama kwa wazazi haikuwa taboo lazima mtoto atarithi tu
  binti ambae mama alikuwa na vidumu tele
  au mvulana ambae baba alikuwa anazaa ovyo ovyo unategemea nini?
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Nitarudi alfajiri with a fresh mind; by the way nyie kapo hapo juu, nini kimetokea hadi mnaanza kudig family histories?
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa wote walikwishafariki nilifunga ukurasa wa kufikiria kama walikuwa na ubaya fulani. Na mara nyingi hufikiria vitu vizuri walivyonifanyia.

  Unajua watu huwa hawaelezei mabaya ya wazazi kwa sababu moja kubwa: Tumeshakuwa na tunajitegemea yaliyopita yamepita, baba/mama hawezi kutulima mboko kama zamani, kututukana n.k..........wanajua tumekuwa, na heshima wanayotupa ni tofauti na ilivyokuwa zamani.

  Lakini tusisahau hakuna hata mmoja ambaye anafurahia adhabu kali na matusi kwa ule umri wa utotoni, na wengine hudiriki kuhama nyumba kabisa...........hasira,kunung'unika n.k. Lakini unapokua na kukutana na suruba za huku duniani zinazoumiza roho,mwili na moyo unapiga taswira nyuma unasema "pamoja na yote waliyoyafanya lakini angalau walinionyesha upendo kwa mbali' kuliko haya manyang'au.
   
 8. mito

  mito JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,605
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  If other factors are constant, tabia ya mtoto hujengwa na mzazi au mwalimu. Kwa maneno mengine at some stages mtoto anaamini cho chote afanyacho mzazi au mwalimu ni sahihi, ndo maana yuko likely kuchukua tabia za baba yake hata kama ni mbaya, anakuwa anaamini hizo tabia ndo zimemfanya baba yake awe baba, so anahisi asipozichukua hata kuwa baba kamili. Na hii ndo sababu ya hapo kwa red
   
 9. mito

  mito JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,605
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  zina-reflect the current na ku-predict future generations! aaaah, sorry just joking!
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ha ha ha, acha ukorofi

  nimeiba mboga akajali.

   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,650
  Trophy Points: 280
  Twenzetu wife tukalale! . . . .
   
 12. n

  ndagabwene Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa jembe bwana mpaka kaamua kutoa haya mawe kuna kitu ameona.so sio kitu maswali kwani ukijua kuuliza ujue pia na majibu.unajua inabidi ttafakari kwa kina sana tabia za wazazi wetu.ze problemu iz zat huyu jamaa hakuhusisha wasio na wazazi mimi nikiwa mmoja wao kwa hiyo sitoweza kujibu kwa kuwa sina ushahidi mkubwa na bado sijaoa.take it easy!
   
 13. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hii topic ni muhimu afu ni ngumu. Kumbuka kuna wazazi wawili in most cases; baba na mama
  Napenda kuchukulia mfano wa maisha yangu kuliko kuongelea theory.

  Baba yetu alikuwa ni baba ambaye hata tukikaa na ndugu zangu tunaambizana hakuna kati ya marafiki na jirani zetu aliyebahatika kuwa na baba kama baba yetu; alikuwa na kasoro zake lakini alikuwa ni baba rafiki. Ni baba ambaye tukiwa nyumbani hatuchoki kukaa pembeni yake kusikiliza story za maisha. Hakuwahi hata kumpiga mtoto kibao (kwa kumbukumbu zangu). Lakini alikuwa hachoki kutuambia tusome na kutupa mifano hai ya waliosoma maisha yao yakoje na wasiosoma maisha yao yakoje wakati mwingine alikuwa anatupa mifano ya ndugu zake wa kijijini. Ni baba aliyekuwa anaamini kwenye reinforcement na si punishment. Kwa kweli na mimi niliamua kuiga model ya baba yangu na si mama yangu kwa sababu niligundua ina work kwani wote tulisoma at least hicho ndicho kilikuwa kilio cha baba.

  Mama ni quit opposite. Kwanza alikuwa hana muda na mtoto; the only memory that we have of our mother ni kichapo. Kwa kweli tulipokuwa wadogo siyo siri wote tulikuwa TUNAMCHUKIA mama. Tumeshamsamehe baada ya kukua. Ni mama ambaye hakuna mtoto alikuwa anataka kukaa karibu yake. Maana anaweza kukutuma umletee maji ukajichanganya ukaleta juice ukala kibao cha nguvu. Na si muongeaji; na wala haongei mara mbili. Uwa tunakaa na ndugu zangu na kuangalia mchango wa mama kwenye malezi yetu hatuuoni kwani tulikuwa distant. Lakini tulichokuja ku conclude ni kuwa mama alilelewa maisha yake yote na mama wa kambo. Hivyo hajuhi kupenda kwa sababu hakuwahi kupendwa.

  Wakati mwingine baba na mama walikuwa wanatofautiana hasa mama akiwa anatuchapa baba akiwepo. Na mama alikuwa ana m criticise baba kwa kutulea KIDHUNGU; anamwambia watoto wa kiswahili hawalelewi kwa vitabu. Maana baba alikuwa na library ya vitabu vy malezi ya watoto na anajua vizuri saikolojia ya watoto kwani anapenda sana kusoma.

  Mimi wanangu sitaki kuwachapa na sipendi hata mtu mwingine afanye hivyo. Kumchapa mtoto karne hii ya 21 nachukulia kama ni uvivu wa kulea. Mtoto akikosea inabidi udadisi ni kwa nini anafanya anavyfanya kwani kupiga hakusaidii. Baba yetu hata maswala ya ma boyfriend nilikuwa makini kwa kuwa nilijua baba yangu atakufa akisikia nina ujauzito; nilijua hatanipiga ila nitamfanya afe kwa BP na nilivyokuwa nampenda nilikuwa na behave ili asiwe disappointed kwani nilijua ana believe so much in me.

  Mi ndio maana kuna siku niliwambia watu humu mwanangu namlea kwa kumsifia sana pale anapofanya vizuri na kumwambia he is better than that anapochemsha watu wakaja juu eti mtoto wa kiafrika sifa zitamharibu; lakini mimi nimelelwa kwa sifa na zili work
   
 14. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  huwezi amini watoto wa siku hizi wanakuchallenge na kukuambia usoni, sikwenda kuabudu kwa muda kama wa miezi mitatu, nilichoambia na mtoto sitakaa nisahau,he went further kuandika text kwa grannies wake, sasa kama anaweza fanya hivyo sidhani kama ataweza kumezea mapungufu mengine yanayomkwaza, nahisi mimi pia sina uvumilivu na wazeewangu
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  this is very interesting aisee
  but hapo angalau umeona 'mama wa kambo' aliemlea mama yenu alivyomu affect
  mna bahati na baba
  je mngelelewa na mama peke yake?
  umewahi fikiri mngekuwaje ukubwani?
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  watoto wa siku hizi wako influenced na vitu vingi
  tv mfano..
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  asante
  hata kama hukulelewa na baba au mama
  yoyote alie kulea utotoni atabaki na influence ya tabia zako
  hata kama alikuwa mjomba au kaka
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....hii thread ina akili sana aisee. Hili jambo siku zote ndilo linatafsiri maisha yetu huko tulikotokea...
   
 19. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwakweli kuna katabia nimerithi kwa mama yangu yani ni sawa na copy and paste,
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Imefika mahali naanza ku-admire system ya wahindi ya kuoana ndani ya familia. Manake mnajua the same things, u believe in the same stuff and morals are more or less the same. Hata kugombana ni tofauti. Kama mmetoka familia ya kuzurura hadi usiku wa manane ndo mrudi home mnakuwa poa tu! Kama ni wa kula dinner na kusali kama familia mnaelewana!

  Niko extra careful kulinganisha malezi tuliyopata, na ya wengine na kuwa realistic especially pale ambapo nadhani wazazi wangu walikosea. Kwa hiyo I'm careful not to repeat their mistakes, especially za mama yangu (ambazo zinamhusu pia baba indirectly).

  Strongest link niliyopata kwa wazazi ni kuona positive side of every situation. When I'm mistreated that is when I should surprise my offender of what I'm capable of. Na ukaribu wa kindugu ni muhimu. So we tell each other 'unakumbuka mom/dad alishafanyaga 1,2,3. That is exactly what you are planning to do na matokeo yatakuwa haya. You don't have to repeat your parents' mistakes!'

  Isitoshe Bible inasema 'nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao. Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu', so napambana spiritually too maovu ya wazazi yasinirudie. Kama kuna mtu aliambiwa wajukuu zako, ama wanao pia watatendwa hivi hivi, mie hayatanipata in the name of Jesus! Nnayoyajua naomba toba na nisiyoyajua pia. So ni kweli wazazi wana influence kubwa kwa watoto kama ambavyo NK na TB mmeongelea.
   
Loading...