Ifike hatua tuache chuki dhidi ya watoto wa kishua na vigogo wakati makosa ni ya wazazi wetu walichezea maisha

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Wakati wazazi wao wako bize na kusoma na kutengeneza maisha ya kizazi chao cha badae sisi wazazi wetu wako bize na starehe na kula Bata.

Wakati wazazi shuleni walikuwa wanazingatia masomo sisi wazazi wetu walikuwa kila siku wako chimbo .

Wakati wazazi wao kila wakipata pesa wanawekeza kwa ajiri kizazi cha badae sisi wazazi wetu kila wakipata pesa inashia kwenye kula Bata

Wakati wazazi wao walikuwa watu kujishusha na kujumuika na watu muhimu sisi wazazi wetu walikuwa wanajifanya masikini jeuri hawawezi kujishusha .

Alafu kesho kutwa watoto wao wana enjoy maisha sisi tunabakia kujenga chuki na makasiriko wakati wazazi wetu walichezea maisha .
 
......bora umelisema mkuu, mimi sio wa ushuani lakini moja ya mambo makubwa yanayotufanya masikini tusijikwamue katika janga hili, ni hili swala la kujenga chuki dhidi ya wenye mafanikio, kuna ujinga fulani tunao wa kuona kwamba matajiri na wenye fedha wametunyang'anya au kutudhulumu sisi masikini.........

..........ukifuatilia deep down utagundua sababu ni wivu mkali tulio nao sisi 'njaa kali' , unakuta matamanio yetu sio kuwafikia hao wenye mafanikio bali ni kutaka kuwashusha wawe masikini, lakini pia tunataka matajiri watunyenyekee, eti tunataka mtu ila akipita na gari yake kwenye kijiwe chetu ashushe kioo atusalimie ndo aende, what a non sense!........
 
Ngoja waje, makasiriko huwa ni ya grade A. Thed weld dwelaz
 
Mimi mzazi wangu hakuchezea maisha,alipambana kadiri ya uwezo wake sema bahati haikua upande wake.

Kunilea tu mpaka kufika hapa haya ni mafanikio tosha inabidi na mimi niendeleze palipobaki.

Hua nikiendaga kijijini kwa Babu jinsi kulivo hua namuona mzee alikua shujaa sana.

Inamana asingekua jasiri wa kutoka kijijini na kuja mjini kupambana pasipokujua atafikia wapi,atakula wapi na atalala wapi ina mana na mimi ningezaliwa kijijini na kua mwanakijiji.
Huenda ningekua mchoma mkaa maarufu huko kijijini kwetu who knows?
 
Daa kaka nimependa ushuuhuda wako

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
.......bora umelisema mkuu, mimi sio wa ushuani lakini moja ya mambo makubwa yanayotufanya masikini tusijikwamue katika janga hili, ni hili swala la kujenga chuki dhidi ya wenye mafanikio, kuna ujinga fulani tunao wa kuona kwamba matajiri na wenye fedha wametunyang'anya au kutudhulumu sisi masikini.......
.........ukifuatilia deep down utagundua sababu ni wivu mkali tulio nao sisi 'njaa kali' , unakuta matamanio yetu sio kuwafikia hao wenye mafanikio bali ni kutaka kuwashusha wawe masikini, lakini pia tunataka matajiri watunyenyekee, eti tunataka mtu ila akipita na gari yake kwenye kijiwe chetu ashushe kioo atusalimie ndo aende, what a non sense!!!......
Ukifatilia kwa mbali haya mambo kwa mbali utagundua kuwasema watu waliofanikiwa vibaya

Tunatumia kama njia ya kujifariji

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Wakati wazazi wao wako bize na kusoma na kutengeneza maisha ya kizazi chao cha badae sisi wazazi wetu wako bize na starehe na kula Bata.

Wakati wazazi shuleni walikuwa wanazingatia masomo sisi wazazi wetu walikuwa kila siku wako chimbo .

Wakati wazazi wao kila wakipata pesa wanawekeza kwa ajiri kizazi cha badae sisi wazazi wetu kila wakipata pesa inashia kwenye kula Bata

Wakati wazazi wao walikuwa watu kujishusha na kujumuika na watu muhimu sisi wazazi wetu walikuwa wanajifanya masikini jeuri hawawezi kujishusha .

Alafu kesho kutwa watoto wao wana enjoy maisha sisi tunabakia kujenga chuki na makasiriko wakati wazazi wetu walichezea maisha .
We sema wazazi wako usitujumlishe, wengine wazazi wetu wali porwa tu mali zao na hao vigogo.
 
Mimi mzazi wangu hakuchezea maisha,alipambana kadiri ya uwezo wake sema bahati haikua upande wake.

Kunilea tu mpaka kufika hapa haya ni mafanikio tosha inabidi na mimi niendeleze palipobaki.

Hua nikiendaga kijijini kwa Babu jinsi kulivo hua namuona mzee alikua shujaa sana.

Inamana asingekua jasiri wa kutoka kijijini na kuja mjini kupambana pasipokujua atafikia wapi,atakula wapi na atalala wapi ina mana na mimi ningezaliwa kijijini na kua mwanakijiji.
Huenda ningekua mchoma mkaa maarufu huko kijijini kwetu who knows?
Hii ni kweli kabisa

Sisi sote tumetoka jamii hoehae

Kwene familia yenu ukirudi nyuma kizazi kimoja tu au viwili huko nyuma utakuta waliishi maisha duni sana tena sana

Ukiona leo mmejipata jua kuna mtu hapo kati aliumia sana kwa ajili yenu wa mbeleni
 
Wakati wazazi wao wako bize na kusoma na kutengeneza maisha ya kizazi chao cha badae sisi wazazi wetu wako bize na starehe na kula Bata.

Wakati wazazi shuleni walikuwa wanazingatia masomo sisi wazazi wetu walikuwa kila siku wako chimbo .

Wakati wazazi wao kila wakipata pesa wanawekeza kwa ajiri kizazi cha badae sisi wazazi wetu kila wakipata pesa inashia kwenye kula Bata

Wakati wazazi wao walikuwa watu kujishusha na kujumuika na watu muhimu sisi wazazi wetu walikuwa wanajifanya masikini jeuri hawawezi kujishusha .

Alafu kesho kutwa watoto wao wana enjoy maisha sisi tunabakia kujenga chuki na makasiriko wakati wazazi wetu walichezea maisha .
MJINGA SANA WEWE. shukuru kwa neema kama upo vizuri
maskini wote siyo wazembe
 
Huwezi kusema mzee wako alichezea maisha wakati yeye akiwa na umri kama ulio nao wewe sasa, alikua ameshajenga na ameoa! Na wewe bado unaishi kwake.
Wenyewe siku hizi wana kauli mbiu yao yenyewe inasema “kataa ndoa"

Yaani kijana kila siku anaamka nyumba moja na wazazi wake wanamlisha lakini bado anasema kataa ndoa.
 
Umeandika upuuzi tu tena umeenda mbali kwa wazazi wakati mimi kuna watu nimesoma nao walikuwa vipanga shuleni ila nyumbani kwao walikuwa hovyo ikabidi wapige chini shule kwa kukosa ada waingie mtaani ili wasaidie familia sasa inakuwaje unawatukana na kuwakejeli unajua mazingira ya elimu zamani wewe kuna wanafunzi wengi kipindi nakua walikosa nafasi baada ya kufaulu kwasababu shule zilikuwa chache unakuta mkoa mzima shule ni moja bora ungesema vijana ila kuwatukana wazazi kwa kutokusoma kwa uzembe wa joka la kijani inaonyesha jinsi ambavyo hujitambui.
 
siku ukija kugundua kwamba si juhudi pekee huamua mafanikio ya mtu,bali lazima bahati iingie kati pia ndipo utajua hata hao wa kishua wanaobinua makalio kwa hela za baba zao wanastahiri kukasirikiwa maana ni wajinga kama wewe.

yaani baba yako alikuwa waziri unataka kusema alikuwa smart sana si ndio???
 
Back
Top Bottom