Write your reply. Hujatoa ushauri, bali umetoa ukosoaji usio na mantiki.
Hujasoma vizuri kwani kwenye uzi huo kuna hoja na ushauri wa kila lililochunguzwa!! Nakubaliana nae kwa mara 100% kuwa muelekeo wa kutaka kuijenga nchi kwa kutegemea wajomba kutoka nje kutaweka uhuru wa nchi hatarini. Nchi ilikuwa inasisitiza kutumia rasilimali zetu vizuri na kutoka kwenye kutegemea madeni ya benki ya Dunia na IMF; lakini sasa inaelekea msimamo ule umeanza kuyumba na kuendekeza mikopo toka nje kwa maendeleo ya nchi. Tusipokuwa waangalifu muda si mrefu tunaweza kujikuta tunaomba misaada toka nje kulipa mishahara ya wafanyakazi wetu!!!!