MenukaJr
Member
- Apr 24, 2021
- 50
- 128
Maoni yangu:
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa taarifa ya utendaji wa Serikali kwa siku 78 za Rais Samia Suluhu ofisini-Ikulu. Pamoja na mambo mengi mazuri, taarifa hiyo ina mapungufu kadhaa kwa maoni yangu, kama ifuatavyo:
1. Mkataba wa Gesi Da'slam-Mombasa
Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali imekosa kueleza jambo moja muhimu sana kutokana na ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Kenya. Akiwa Kenya Rais Samia Suluhu akizungumza nyuma ya Rais Kenyetta wa Kenya alisema kuwa Serikali ya Tanzania imeingia mkataba na Kenya kwa ajili ya kusafirisha gesi kutoka Da'slam kwenda Mombassa. Gharama za Mkataba ule hazifahamiki hadi sasa.
Baada ya taarifa ile, watu wengi walihoji uhalali wa mkataba ule na haraka ile. Kwa vyovyote vile taarifa ya Serikali ilipaswa kuingiza jambo hili kwa ajili ya wananchi na kuondoa utata. Kukosekana kwake kunaendelea kuzua utata na kuimarisha tetesi kwamba tumepigwa tena!!
Ushauri: Msemaji wa Serikali afanye anavyoweza kutoa taarifa hii kwa maana ni kati ya mambo makubwa yaliyofanyika katika siku 78 za Rais na yalitegemewa kutolewa taarifa kwa umma.
2. Kodi na Mapato
Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali inasisitiza kuhusu uwiano wa makusanyo ya kodi kabla ya March na baada. Lakini ukweli takwimu zinaonesha tofauti kati ya wakati wa ubabe na wakati wa lipa kwa hiari. Mtu anayelenga kukusanya 1.99 trion akakusanya 1.67 sawa na 84.1% (March) hawezi kulingana na mtu aliyelenga kukusanya 1.61 trion halafu akakusanya 1.34 trion sawa na 83.2 (April). Tofauti ya malengo na makusanyo ni kubwa, deficit hii ikitokea kila mwezi kwa mwaka mzima tumepoteza pesa nyingi.
Ushauri: Hakuna kodi inayokusanywa kwa hiari Duniani kote. Ulipe kwa hiari usalimike au usilipe ufungwe na kufilisiwa (ubabe). Ni principle!
3. Utegemezi
Asilimia zaidi ya 70 ya taarifa ya Serikali imeonesha utegemezi. Ni kama nchi yetu imejiandaa kukopa zaidi na kutegemea misaada. Hizi dalili sio nzuri, tunaweza kurudisha nyuma jitihada zetu za kujiomboa na hatimaye kujitegemea.
Ushauri: Hatuwezi kujenga nchi kwa kutegemea misaada na mikopo. Ile spirit ya kwamba nchi yetu ina uwezo wa kujitegemea iendelee. Taifa lenye kutegemea hisani kwa kila kitu ni rahisi sana kupoteza uhuru wake.
4. COVID-19
Taarifa inaeleza kwamba Kamati iliyoundwa na Rais kwa ajili ya kufanya tathmini ya kuishauri Serikali juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Aidha, taarifa imesema kuwa kamati hiyohiyo ya wataalam wa afya imekabidhi mapendekezo yenye mpango wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati wa kukabiliana na Corona.
Ushauri:
1. Kamati ya wataalam wa afya haiwezi kufanya kazi ya kufikiria na kupendekeza kwa ufanisi mambo ya rasilimali (pesa) kwa ajili ya mkakati wa kupambana na korona. Ile timu imejaa watu wa afya, Rais aunde kamati nyingine ya wataalam wa uchumi na diplomasia ya Dunia kwa ajili hiyo.
2. Imeelezwa kuwa Baraza la Mawaziri litaketi hivi karibuni kujadili ripoti ya Kamati ya corona. Uwezekano wa kukubaliwa chanjo ni mkubwa. Kimsingi jambo hili halina maana yoyote zaidi ya kutii ITIFAKI ya Dunia, Baraza la Mawaziri likikubaliana lijenge hoja ya kuanza kufanya utafiti na kujitengenezea chanjo yetu wenyewe ili kunusuru kuifilisi nchi kwa kuiingiza katika madeni makubwa ya kughalamikia chanjo.
5. Ndoto za Idara ya Habari Maelezo
Msemaji Mkuu wa Serikali amesema anayo ndoto ya kuanzisha Televisoni (kwenye king'amuzi) kwa ajili ya kufanya vipindi vya taarifa za Serikali 24/7. Amesema pia uamuzi huo utaambatana na kufungua Redio na Gazeti la Habari Maelezo.
Kwa maoni yangu hizi ni fikra mbovu sana. Serikali yenye Televisheni ya Taifa, Redio ya Taifa na Magazeti ya Serikali haiwezi kufikiria kuanzisha Televisheni nyingine, Redio nyingine na Gazeti jingine kwa kazi hiyohiyo. Huu utakuwa upotevu wa pesa za Serikali bila sababu.
Ushauri: Pale TBC kuna vipindi vingi vya kipumbavu. Msemaji wa Serikali apendekeze maboresho pale, achukue vipindi kwa namna anayoona inafaa. Hotuba za Viongozi anazotaka kurusha zitarushwa pale, utekelezaji wa Serikali vitatangazwa pale na kila kitu. Kadhalika Redio na Magazeti. Hiyo ndio kazi vya Vyombo vya Habari vya Serikali. Hatuwezi kuwa na utitiri wa vyombo vya Serikali kwa kazi zilezile katika nchi maskini kama hii.
#TutakukumbukaDaimaJPM.
MenukaJr,
Da'slam.