Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Wasaidizi wa rais kama waziri mkuu, mwanasheria mkuu na katibu mkuu kiongozi nadhani bora wangejiuzulu tu kwasababu zifuatazo.
Aidha.
Wameshindwa kumsadia rais kutekeleza majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yetu. Tumeshuhudia makosa mengi katika teuzi za rais ambayo hayakutakiwa kuwapo kabisa kama wasaidizi wa rais na washauri wake wangefanya kazi zao zinavyotakikana kwa mujibu wa sheria. Rejea teuzi za rais tangu alipoingia ikulu.
Au.
Huenda rais wetu haambiliki, hashauriki, na kile anachokiamua ndio huwa hichohicho na huja kubadilika mambo ya kiharibika. Sasa kama wasaidizi na washauri wake hawasikilizwi na ushauri wao haufanyiwi kazi, kwanini wasijiuzulu tu kama Magufuli anadhani urais ni cheo na si taasisi?
Rais mstaafu Kikwete na waliomtangulia walikuwa na mapungufu yao lakini si mapungufu haya ya kutia kinyaa na kutuaibisha watanzania wote kama taifa.
Rais kama hashauriki yatakikana abadilike na asikilize ushauri wa watu waliowekwa na katiba maalumu kwaajili ya kumsaidia na kumshauri, na kama anashaurika basi ni ajabu kwa rais kuendelea kumkumbatia mwanasheria mkuu wa serikali na hata waziri mkuu kwa kitendo chao cha kushindwa kuona makosa msingi katika teuzi zake.
Ninashaka na huko tuendako, tunaweza kuona mengi ya kinyaa kuzidi hata haya!
Rangimoto.
0622845394
Morogoro.