Mapumziko garden

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Hi
Jijini Dsm kuna upungufu mkubwa wa sehemu nzuri za kupumzikia familia ( yaani mahali ambapo wewe na familia yako unaweza kwenda bila kigugumizi),mahali ambapo unaweza kuyaona mazingira yenye heshima ya Kiafrika. Naamini familia nyingi zingependa kwenda mahali ambapo ni free fro alcohol, free from uzinzi,free from kiti moto, bali kuna juice ya matunda,ugali wa dona,kuku wa kienyeji,maziwa ya mbuzi,muziki laini kwa sauti ya chini kabisa.

Bustani itakuwa na vyumba vizuri kwa bei nzuri ambayo MKESHA HOI/LAT/KAKA KIIZA wa JF anaweza kumudu bila maumivu na akatamani kurudi tena.Bustani itakuwa na mboga za majani kama mnafu na nyinginezo. Michezo ya watoto wetu itawekwa.

Nahitaji michango ya huduma gani zaidi ziwepo ili kupafanya pawe bora zaidi. Eneo lipo,linafikika kwa daladala,lina maji na ni kubwa kama eka kumi. Hili eneo sitaki kuliharibu, nataka libaki na uasili wake kwa kuitunza miti niliyo ikuta pamoja na nyasi zake. Nitaongeza miti ya matunda tu.
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
Hi
Naamini familia nyingi zingependa kwenda mahali ambapo ni free fro alcohol, free from uzinzi,free from kiti moto, bali kuna juice ya matunda,ugali wa dona,kuku wa kienyeji,maziwa ya mbuzi,muziki laini kwa sauti ya chini kabisa.

Bustani itakuwa na vyumba vizuri kwa bei nzuri ambayo MKESHA HOI/LAT/KAKA KIIZA wa JF anaweza kumudu bila maumivu
una wazo zuuuri.............mana ukisema vyumba kwa ajili ya kulala tu haiingii akilini

mana huwezi acha chumba nyumbani ukaenda kutafuta huko garden

ni hayo tu
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
una wazo zuuuri.............mana ukisema vyumba kwa ajili ya kulala tu haiingii akilini

mana huwezi acha chumba nyumbani ukaenda kutafuta huko garden

ni hayo tu

Hapa nina maanisha,ni kwa ajili ya hawa wa honey moon,sio wale wa short time. Wakati mwingine unaweza kwenda nje ya nyumbani kwako na mamsap wako na mkalala huko huko.
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
1.Swimming pools.

Yes,

Unajua kuna kundi kubwa la jamii linakosa huduma kama hizi, hivi Maaskofu/walokole/mashehe hawapendi nyama choma? au hawapendi kuogelea ktk swimming pools, sasa kama wanataka/penda wapi wanapata huduma hizi? For sure, mchemsho wanapenda, ngoja niwajengee sehemu mwafaka kwao.
 
PatPending

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
490
80
Ni vizuri pia ukawa na maonyesho ya sanaa za asili hususan kwa nyakati za jioni kama vile ngoma na sarakasi.
 
Mama Joe

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,504
823
Good idea my brother,
vyumba safi ni muhimu sio lazima kwenda mikoani kwetu kila likizo mara nyingine tunahitaji kupumzika tu na familia zetu tatizo hoteli zilizotulia ni ghali na adimu.
mie naongezea free internet access na saluni safi ya kinamama ya kusuka kiasili kabisa sio kuweka dawa au urembo asilia mwingineo
Barikiwa

Hi
Jijini Dsm kuna upungufu mkubwa wa sehemu nzuri za kupumzikia familia ( yaani mahali ambapo wewe na familia yako unaweza kwenda bila kigugumizi),mahali ambapo unaweza kuyaona mazingira yenye heshima ya Kiafrika. Naamini familia nyingi zingependa kwenda mahali ambapo ni free fro alcohol, free from uzinzi,free from kiti moto, bali kuna juice ya matunda,ugali wa dona,kuku wa kienyeji,maziwa ya mbuzi,muziki laini kwa sauti ya chini kabisa.

Bustani itakuwa na vyumba vizuri kwa bei nzuri ambayo MKESHA HOI/LAT/KAKA KIIZA wa JF anaweza kumudu bila maumivu na akatamani kurudi tena.Bustani itakuwa na mboga za majani kama mnafu na nyinginezo. Michezo ya watoto wetu itawekwa.

Nahitaji michango ya huduma gani zaidi ziwepo ili kupafanya pawe bora zaidi. Eneo lipo,linafikika kwa daladala,lina maji na ni kubwa kama eka kumi. Hili eneo sitaki kuliharibu, nataka libaki na uasili wake kwa kuitunza miti niliyo ikuta pamoja na nyasi zake. Nitaongeza miti ya matunda tu.
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Good idea my brother,
vyumba safi ni muhimu sio lazima kwenda mikoani kwetu kila likizo mara nyingine tunahitaji kupumzika tu na familia zetu tatizo hoteli zilizotulia ni ghali na adimu.
mie naongezea free internet access na saluni safi ya kinamama ya kusuka kiasili kabisa sio kuweka dawa au urembo asilia mwingineo
Barikiwa

Dada nikushukuru sana kwa nyongeza ya maoni ktk kuboresha huduma ninayotaka kuifanya.
 
LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
1,293
mkuu Malila

kuna kitu wanaita live bird dishes. ... yaani kunakuwa na jamii ya ndege (kuku,bata,kanga,bata mzinga, bata bukini) ambao wapo wanafugwa hapo, halafu mteja akifika anachagua ndege akiwa alive anachinjwa (angalizo; halal)halafu anachagua aina ya mapishi (barberque, fry ,boil etc)

very entertaining
 
Sabayi

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
2,313
980
Usisahau vinywaji vya asili tu kama Togwa n.k (Sina uhakika kama gongo nayo ni kinywaji cha asili kama nacho ni cha asili tuwekee mwanawane)
 
Mkuu heshima mbele kwa kunielewa,
Mtu anakuja anasema nataka kuku au bata huyu au beberu hili, chinja hivi au banika hivi, na pilipili nayo nitalima kidogo, tayari bata/kuku/mbuzi tayari nimeshawapeleka wakaanzishe kijiwe,huku najenga taratibu. Bado sijapata badizzo,Ubungo pale wameishiwa.
 
  • Thanks
Reactions: LAT

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Usisahau vinywaji vya asili tu kama Togwa n.k (Sina uhakika kama gongo nayo ni kinywaji cha asili kama nacho ni cha asili tuwekee mwanawane)

Machozi ya simba yatanigombanisha na mashehe/wachungaji/walokole na watoto wadogo. Alafu afande kula kula atakuwa anawasumbua sana vijana wangu.
 
LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
1,293
Mkuu heshima mbele kwa kunielewa,
Mtu anakuja anasema nataka kuku au bata huyu au beberu hili, chinja hivi au banika hivi, na pilipili nayo nitalima kidogo, tayari bata/kuku/mbuzi tayari nimeshawapeleka wakaanzishe kijiwe,huku najenga taratibu. Bado sijapata badizzo,Ubungo pale wameishiwa.

mkuu Arusha TFA badizzo ipo, ... unahitaji hichi kifaa ili mabeberu yanone

actually you have a very good idea. ., biashara hii ya utalii wa ndani (domestic/local tourism) imesahaulika kabisa

keep it up mkuu
 
Shadya

Member
Sep 14, 2011
87
37
Kaka ni wazo zuri sana na hata ukiongezea ufundishwaji wa vitu mbalimbali kwa watoto, yaani kama vile jinsi ya kikombe kinavyotengenewza watoto wae na elimu hiyo na mengine mengi kila la kheri katika mipango yako wadau tupo tutakuunga mkono aidia kama hizo ndizo zinazotakiwa kuelimishana sio ubishani usio na kichwa wala miguu
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Kaka ni wazo zuri sana na hata ukiongezea ufundishwaji wa vitu mbalimbali kwa watoto, yaani kama vile jinsi ya kikombe kinavyotengenewza watoto wae na elimu hiyo na mengine mengi kila la kheri katika mipango yako wadau tupo tutakuunga mkono aidia kama hizo ndizo zinazotakiwa kuelimishana sio ubishani usio na kichwa wala miguu

Asante,
Ndio maana imebidi niombe mchango toka kwa wadau kwa sababu nakwenda kuhudumia jamii,kwa hiyo lazima jamii ipate nafasi,hatimaye malengo yafikiwe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Top Bottom