Pinokyo Jujuman
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 552
- 104
Hunter: naomba nisaidie nahitaji kufahamu kirefu cha hyo "AGF"
Habari ni habari, nini maana ya forum?...ni kujuzana yanayojiri, unataka kusema kuwa hoja hii haipaswi kufahamika kwa wadau? Au huwa hausafiri na kujifunza mambo?, USHAURI WA BURE: Tembea na ujifunze kwa watu, ili kujua wenzako wanafanya nini, kwanini, wapi na lini..hiyo itakusaidia sana.
Karibu Arusha, Mkutano ni wa delegates zaidi ya 3000, hakuna pa kulala kama sio mwenyeji wa Arusha labda uwe ulifanya booking mwezi uliopita( Mwezi April)
Haya ..niko Arusha,Mkutano wa Bank ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank) kwa hapa umekuwa hosted na Wizara ya Mkulo(nakumbuka tulikaa vikao vingi sana kuhakikisha mkutano huu unafanyika Afrika Mashariki, Mkulo akapiga debe kwamba "Tanzania Tunaweza Bila Kuwezeshwa"kweli ukaja Arusha... lugha tunayoitumia ni Kiingereza na Kifaransa....wafaransa wa kizungu na wa kiafrika...kiswahili NO, mimi naongea kiswahili,. nakutana na mmoja wa waandaaji wa mkutano huu wa kimataifa wa wachumi."votre nom siil vous plait?=Your name please? najitambulisha,naye pia anajitambulisha kwangu, ana uraia wa nchi mbili Ghana na Ufaransa, ni dada mcheshi, mzungu, na ni mara yake ya kwanza kuja Tanzania, tunasalimiana, lakini ghafla Magavana wanaanza kuingia, mnisamehe sijapiga picha..waandishi wa habari usiseme.
Msafara wa rais wa bank ya maendeleo ya Afrika anakaribia kuingia hapa...maafisa usalama kama kawaida.Askari wamejipanga kwa ajili ya kutoa heshima kwa Rais, wote wana silaha...wanapokea maelekezo. mkutano haufanyiki hapa hotelini, ni eneo la AICC(Arusha International Conference Center) hapa ni kula na kulala tu...na vikao vingine vidogovidogo(billateral meetings, working conferences na Launching of AGF, Mabenki yote yana uwakilishi hapa.Wawakilishi wa bank mbalimbali wako hapa, makampuni ya simu pia, TANAPA wanaongoza kwa kuutangaza utalii.
Naiona red carpet kutoka mlangoni hadi kwenye kambarau (lift)ya hotel....
Pikipiki za polisi ziko nne, zinaingia kwa mbwembwe, askari wa usalama barabarani wako hadi ndani ya hotel wanaelekeza magari kila mahali..haya zinaingia gari za polisi kama nne, Field Force Unit, Ambulance ya polisi, Magari aina ya PRADO hayana idadi...yote yana nembo ya kampuni ya ANGONI. Magari madogo madogo na yale ya kukodi hayana idadi. La mheshimiwa silioni,..huyu hapa anashuka, ni mtu wa makamu kidogo, amevaa shati la rangi ya kijivu, suruali nyeusi, na miwani ya jua,. tunampokea anatupa mikono mmoja baada ya mwingine..anasema jambo karibu Tanzania, no anaongea kiswahili, jamani anaongea kiswahili safi...(nimerudi nyumbani,,,,anasema) ni mwafrika kutoka Africa ya...aaaaaaaaaaaaahh, kumbe ni Mheshimiwa Donald Kaberuka, Mnyarwanda anayeitumikia Bank hiyo kwa kipindi cha pili(Miaka Mitano).Anaelekezwa kwenda katika kambarau (lift)..anaingia...end of story. tuliobaki nje, raia na maafande wa usalama wote tunaelekea maeneo yetu muhimu.
Amesoma hapahapa Tanzania na Uingereza na Mwaka 1997 alikuwa waziri wa fedha wa Rwanda...Si tu anapewa salamu za ki-protokali, bali pia nimeangalia wingi wa askari eneo hili na aina ya ulinzi kwa mtu ambaye kwangu naona bora angepokewa kawaida kama viongozi wengine na sio mapokezi zaidi ya yale ya rais wa nchi...haya ngoja tuone mapokezi ya Kikwete kesho hapahapa katika hotel ya Mount Meru, Arusha
Rais anaongea , mawaziri, kibao, kila mtu mfaransa hapa....niko busy mniache kidogo ila Wizara ya Fedha imenunua TV aina SAMSUNG za inchi 65, ziko 60 na kila moja ni zaidi ya TSH 10M, zinazotumika ni 19 AICC, na Mount Meru Hotel 3 tu..mimi sijui zingine ziko wapi,eti wameamua kupotezea
Ni kweli, nafasi hakuna...zote zenye majina haya zimejaa pia ( INNS, RESORTS, GUEST HOUSES, MOTELS, DELUXES)nakwambia zote zimejaa. mkutano unaanza kesho, AICC, Simba Hall. Pia Kumbi za Mbayuwayu,Tausi,Mbuni na Manyara ziko booked hadi mkutano uishe.