Tetesi: Mapokezi makubwa yamsubiri January Makamba jimboni mwake Bumbuli

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Imearifiwa wakati Mbunge wa Bumbuli Mheshimiwa January Makamba akitarajiwa kuwasili jimboni humo mwanzoni mwa mwezi ujao, wapiga kura wake wanajiandaa kumpa mapokezi ya kishindo.

Tuombe sana jeshi la polisi wasiwekee figisu zoezi hili kwani ni haki ya wana Bumbuli kupokea mwakilishi wao na kumtia nguvu.

Mapokezi hayo yatafuatiliwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni Bumbuli.
 
kuwa na panaldol karibu ili maumivu ya kichwa yakizidi ya kufikiri kilichowezekana unywe

Maandamano na mikutano ya kisiasa imepigwa marufuku!
 
Hivi anashindwa nini kuiga "busara" za wenzake waliokuwa mawaziri na kisha kutumbuliwa na kukaa zao kimya?....akikubali huu ushauri wa "kuandaliwa" mapokezi basi lazima awe na plani moja kati ya hizi....(i) Kuhamia upinzani au (ii) kuachana kabisa na siasa za awamu hii nakwenda zake "masomoni"
 
Maandamano na mikutano ya kisiasa imepigwa marufuku!
Mngekuwa na akili,mngejiuliza ni kwanini kila uchaguzi kura za wagombea uraisi wa CCM zinashuka sambamba na idadi ya wabunge wa CCM huku upinzani ukijiongezea kura za wagombea wake wa uraisi na kuongeza idadi ya wabunge wake.

Kwa sasa chama chenu kina-survive kwa msaada wa dola tu kwani kimeshapoteza political legitimacy kwa kiwango kikubwa kuliko Mlima Kilimanjaro!!

Endelee na kiburi chenu na ulevi wenu wa madaraka na ndio maana awamu hii imekuwa ni mateso karibu kwa kila kundi katika jamii kuanzia watumishi wa umma,wafanyabiashara,wavuvi,wanasiasa mpaka na wawekezaji kutoka nje ya nchi!!

Tegemeni majeshi yalinde masilahi ya CCM kama alivyosema mwenyekiti wenu tena hadharani!!!
 
Imearifiwa wakati Mbunge wa Bumbuli Mheshimiwa January Makamba akitarajiwa kuwasili jimboni humo mwanzoni mwa mwezi ujao, wapiga kura wake wanajiandaa kumpa mapokezi ya kishindo.

Tuombe sana jeshi la polisi wasiwekee figisu zoezi hili kwani ni haki ya wana Bumbuli kupokea mwakilishi wao na kumtia nguvu.

Mapokezi hayo yatafuatiliwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni Bumbuli.
Mwambie pia asisahau kukanyaga migongo ya kina mama kama alivyofanya Nepi kule Lindi jimboni kwake. Sisi Hapa Kazi Tu.
 
Mngekuwa na akili,mngejiuliza ni kwanini kila uchaguzi kura za wagombea uraisi wa CCM zinashuka sambamba na idadi ya wabunge wa CCM huku upinzani ukijiongezea kura za wagombea wake wa uraisi na kuongeza idadi ya wabunge wake.

Kwa sasa chama chenu kina-survive kwa msaada wa dola tu na kimeshapoteza political legitimacy kwa kiwango kikubwa kuliko mlima Kilimanjaro.

Endelee na kiburi chenu na ulevi wenu wa madaraka na ndio maana awamu hii imekuwa ni mateso karibu kwa kila kundi katika jamii kuanzia watumishi wa umma,wafanyabiashara,wavuvi,wanasiasa mpaka na wawekezaji kutoka nje ya nchi!!
Kura zipi mkuu? Mbona kila uchaguzi Chadema wanaingia gizani?
 
Tunakoelekea watatajana mabaya yao yote...hata hizo kura za urais 2015 kuna watu wanajua mchezo mzima ulivyofanyika hopefully.

Kumpata mtu msafi ndani ya CCM ni kazi kubwa; ni bora upewe kazi ya kutenganisha punje za sukari na mchanga toka kwenye gunia la kilo 100.
 
Inatakiwa a keep low profile for his own good na hasa kama anatamani kurudi katika vitabu vizuri vya JPM !
 
Imearifiwa wakati Mbunge wa Bumbuli Mheshimiwa January Makamba akitarajiwa kuwasili jimboni humo mwanzoni mwa mwezi ujao, wapiga kura wake wanajiandaa kumpa mapokezi ya kishindo.
Tuombe sana jeshi la polisi wasiwekee figisu zoezi hili kwani ni haki ya wana Bumbuli kupokea mwakilishi wao na kumtia nguvu.
Mapokezi hayo yatafuatiliwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni Bumbuli.
Hahaahahaa...

Huu sasa ni uchochezi kabisaa
 
Back
Top Bottom