Mbunge wa Bumbuli, January Makamba atishia kuifuta Halmashauri ya Bumbuli

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,832
8,623
Katika hali isiyo yakawaida ikiwa ni muendelezo wa migogolo inayoendelea ndani ya jimbo la Bumbuli, Mh January Makmba ametishia kuifuta halmashauri hiyo ambayo aliianzisha yeye mara tu baada ya kuwa mbunge.

Mh Makamba amefikia hatua baada ya sintofahamu ya muda mrefu inayoendelea baina yake kama mbunge na watendaji na madiwani katika halmashauri hiyo, kumekuwa hakuna maelewano wala masikizano baina ya viongozi wa halmashauri na mbunge wao, kwa kile kinachosemekana mbunge huyo kutaka kuwaamulia kila jambo kwa namna anavyotaka yeye.

Inasemekana jambo kubwa linaloleta mvutano kwa sasa ni juu ya ujenzi wa jengo la ofisi za halmashauri hiyo ambapo mbunge na halmashauri zimetofautiana katika sehemu ambayo jengo hilo linapotakiwa kujengwa.

Mbunge anataka jengo hilo lijengwe Bumbuli wakati halmashauri inataka jengo hilo liepelekwe kwehangala, itakumbukwa kwamba halmashauri ya Bumbuli ilinunua eneo hilo kwa ajili ya kujenga ofisi hizo na kupewa kibari na serikali na mpaka kufikia hatua ha kutangaza dhabuni ya kazi hiyo,
Kwa mujibu wa madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa halmashuri na mkurugenzi wa halmashauri hiyo mchakato wa kuamua ofisi hizo zijengwe wapi ulifanywa na wataalamu na kuafikiwa ofisi zijengwe Kwehangala kwakuwa eneo hilo ni kubwa na linafaa ukilinganisha na eneo analotaka mbunge ambalo halikidhi vigezo.

Wakiongea kwa sharti la kutotajwa majina madiwani walisema, mbunge wao amewadhalilisha sana mbele ya wananchi,"kulikuwa hakuna haja ya mbunge kuitisha mkutano wa hadhara na kututukana mbele za wananchi, angetuita tukakaa ili tumueleze hali halisi", alikuwa anaeelezea mkutano uliotishwa na mbunge wiki iliyopita ambao mbunge aliwahakikishia wananchi jengo hilo halitajengwa wanakotaka madiwani bali anakotaka yeye na kusema madiwani hawakufuata taratibu.

Katika mkutano huo ambao ulileta mpasuko sana wananchi waliokuwa wameandaliwa na mbunge waliwazomea madiwani wao kbaada ya kuambiwa hawakufuata taratibu.

Pamoja na mkurugenzi na madiwani kutoa ufafanuzi wa mchakato kamili uliopitisha jengo hilo kupelekqa kwehangala bado mbunge alishikilia msimamo wake wa kutofanya hivyo.

Baada ya msuguano kuongezeka, mbunge huyo amemuamulu mkurugenzi kusitisha dhabuni ya ujenzi mpaka hapo utaratibu utakapokamilika na maamuzi kufikiwa la sivyo mbunge huyo atalazimika kuifuta halmashauri hiyo au kuzuia pesa za ujenI zinazotolewa na serikali.

Haya yanatokea wakati kukiwa na maandalizi ya ziara ya Mh Raisi mwezi ujao na mkuu wa mkoa akiwa amekwisha kagua eneo hilo na kuridhika nalo na kupanga raisi aje kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo, hii inaweza kusababisha ziara ya raisi kusitishwa kwani kumeonekana kuwa na migogoro mingi ndani ya jimbo hilo, wapo wana intelijensia wanaofikiri mbunge anafanya makusu ili kuzuia raisi kufika jimboni humo ambapo anahofia atakuja kummaliza mbunge kwa utendaji wake kwani kuna mgogolo wa kiwanda cha chai ambao mbunge anahusika nao na mpaka sasa ni miaka zaidi ya mitano hakijafunguliwa.

Na Mwandishi wenu
Abdalah Shemboza
Lushoto.
 
!
!
Mbona anachelewa, si afanikishe ili DC mmoja awe hana kazi. Hatuna cha kupoteza
 
wakuu samahanini kwa swali langu

hivi kuna kautaratibu kokote au sheria kwamba kila mgombea wa nafasi yeyte awe anapimwa
mfano: akili, mkojo, damu, nk?
 
Sahivi ni mwendo wa kutisha tisha tu
 
..Mh January Makmba ametishia kuifuta halmashauri hiyo ambayo aliianzisha yeye mara tu baada ya kuwa mbunge..

Serikali hii ya awamu ya Tano kila mtu mwenye ka cheo Serikalini ni Kambare. Sasa huyu nae anawezaje kufuta Halmashauri? au anamaanisha ataenda kuchonga mdomo kwa boss wake Magufuli aifute..na ili iweje sasa?
 
Back
Top Bottom