Mapitio ya wimbo: JKT Taarab - Chura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapitio ya wimbo: JKT Taarab - Chura

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ms Judith, Jan 4, 2012.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  nimeweka wimbo wa CHURA wa JKT Taarab kwenye lik hii hapo chini:

  https://www.jamiiforums.com/entertainment/208761-chura-jkt-taarab-walitisha-sana-enzi-hizo.html

  naomba tujadili usahihi wa maneno hayoo yaliyokolezwa rangi nyekundu

  1.
  mimi nafikiri badala ya kusema nilikisia, ilipaswa kusemwa nilidhania au nilifikiria, manake makisio ninayoyajua mimi ni "estimates" kwa kiingereza na haiwezekani kwa vyovyote vile kuwa dhana iliyoko kwenye hilo shairi ni "estimate"

  2.
  na hapo kujing'atua, ukiachilia mbali msuala ya vina na mizani, tusema mwalimu nyerere aling'atuka au naye alijing'atua madarakani??

  3.
  kuhusu "kujitosa pembeni", hapo pembeni ni wapi, ni kisimani au nje ya kisima, na kama ni nje ya kisima, inawezekana kitu au mtu kujitosa nchi kavu? au kujitosa lazima iwe majini (kisimani/mtoni/ziwani/baharini nk)?

  4.hiyo sentensi nadhani iko sawa kisarufi, ila kimantiki ni suala la tafsiri ya neno nyumbani na wakati tu kwamba kwa wakati wa sasa, haisisitizwi kuwenda kuoa nyumbani na kwa wakati huu mtu aweza kuoa popote hata nchi za ng'ambo.

  pia baadhi ya mila haziruhusu kuona nyumbani (close relatives). japo kishairi inaeleweka kuwa ililenga kubalance vina na mizani, isipokuwa kama dhana ya neno nyumbani kama inavyotumika, imelenga dhana sawa na "home town/city/country" nk vinginevyo kama ni close relative itakuwa jambo lisilowezekana kwa mila nyingi za kiafrika

  nyie mnaonaje wapendwa?

  mbarikiwe sana

  Glory to God
   
 2. c

  chama JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Lugha ya kishairi mara nyingi hainyooki la ujumbe hufika kama inavyotakiwa, pamoja na yote umemwelewa Chura?

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 3. mtemiwaWandamba

  mtemiwaWandamba JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 536
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hii ni fasihi. Na katika fasihi watunzi hutumia maneno anuai hata ya lugha za kigeni ili mradi wapate vina muafaka katika mpangilio wake. Na katika muktadha huo inafika wakati wanaweka maneno kimakosa, sasa hapo hunabudi msomaji ufahamu nini maudhui ya Mtunzi au Mwandishi. Lugha ni Fasihi . Lakini umelielewa Shairi maana yake?
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Mjadala uendelee...
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,948
  Likes Received: 23,830
  Trophy Points: 280
  Mkuu chama wa Gongs,

  Hebu fanya maarifa hapo, huyu chura ni nani? mi mpaka leo bado kumjua

  Natanguliza shukrani

  Asprin
  Boko Basihaya, DSM.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,948
  Likes Received: 23,830
  Trophy Points: 280
  Mkuu mtemiwaWandamba,

  Tafadhali saidia mimi kujua maana ya huu ushairi. Huyu chura ni nani anazungumziwa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #7
  Nov 3, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Ms Judith katika thread yako ya kwanza nimeona umetoa like kwa SOBY kuwa ni kiharage
  kila mahali kiharage huwa kipo km hakiukung'olewa na kinakaa karibu na kisima kwa vile hudhaniwa huwa ni mlinzi kinatisha sana kwa umbo lakini si lolote hadi hii leo hakizuii lolote na ukitaka kuteka maji chenyewe huondoka na kushangilia mafuriko
  Ubeti wa 2.
  Mwenzenu nilikisia ni mlinzi kisimani,
  mtu utamzuia maji akiyatamani
  Akaja dada Rukia na ndooye mkononi,
  chura ukajing`atua ukajitosa pembeni
  Hizi ni lugha za kughani mashairi na hazifuati kina ila maana huwa nyingi na ndio maana huona watu wengi wanazishobokea
  Fuatilia wimbo wa TOT katika Rapping anaposema
  anakalia KIGOGO na si MBURAHATI
  AU
  Gonga mbele x 3 kama mwenyewe hayupo zunguka
  Nyuma gonga x 2 km hayupo mwaga mzigo


  Kwa hiyo ni kazi kwelikweli km mke wangu akianza kushobokea Taarabu na nyimbo hizo naona km ataniacha?
  Na mara nyingi naona 80% ya wapenda Taarabu ndoa zao ..............
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,164
  Trophy Points: 280

  Churaaaaa...... churaaaaaaaaaaa...........ni


  [​IMG]
   
 9. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Jf is never boring. Haya twendeni kwa mrisho mpoto sasa
   
 10. Magwangala

  Magwangala JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 2,005
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Maana ya Chura?naogopa ban!
   
 11. Interest

  Interest JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2016
  Joined: Apr 11, 2015
  Messages: 934
  Likes Received: 1,258
  Trophy Points: 180
  Aaah! CHURAAA..
   
 12. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2016
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Sizonje.............hii ndiyo nyumba yetu......milango ipo ila wanapita madirishani....
   
 13. naiman64

  naiman64 JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2016
  Joined: Nov 22, 2013
  Messages: 3,726
  Likes Received: 1,285
  Trophy Points: 280
  CHURA ni me ambaye kukipambazuka, yeye hukaa vipembezoni(chobingo) kutongoza mabinti, mtunzi anamuuliza CHURA kwamba ni hohehahe hana a wala be huyo binti (maji) akimpata atampeleka wapi.
  Beti ya pili ameendelea kumuonya aache tabia hiyo maana tayari ni kama wanamvizia watamuumiza atahudumiwa na nani wakati hana mke.
  Ubeti WA tatu umejitosheleza. Pia rekebisha hapo si mgongo ni ukivunjika ugoko
   
Loading...