Sifa kwa Rais Magufuli na dhana ya uungu inayojengea kwa kasi

Sam Naipenda

Member
Mar 1, 2018
97
720
1109723


## kuna dhana ya uungu inajengeka kwa kasi sana juu ya magufuli. mitume na manabii wa uungu huu wakiongozwa na manabii wakuu kama makonda, profesa kabudi, ndugai, shekhe kipoozeo, kibajaji, tulia aksoni, na wengine, wanafanya kazi ya ziada kuhakikisha utukufu na uungu wa magufuli unakua mkubwa kwa kasi na unamwingia kila mtu.

# kilichotokea kwenye safari hii ya afrika kusini na namibia ni udhihirisho mkubwa wa uungu anaojenga na kujengewa magufuli. ni mara ya kwanza katika taifa letu kiongozi wa nchi anakwenda nje ya nchi halafu habari kubwa hapa nyumbani inakua ni rais kushangiliwa huko alikokwenda. habari sio alichokwenda kufanya, sio diplomasia, au faida nchi inayopata kwa safari yake bali ni yeye kushangiliwa.

hadi mkuu wa mkoa na mtume mkuu wa uungu wa magufuli anadiriki kuliongea hili mbele ya taifa. watanzania hii ni hatari. miungu pekee ndio wana kiu kubwa ya kusifiwa. wanapenda sifa na utukufu toka kwa wanadamu maana inadhihirisha utawala wao juu yao. sasa unapokua na rais nayejenga hili, ujue ukengeufu umetuvaa kama taifa.
hebu tujiuliza mswali

#ni rais wa nchi gani aliyeingia pale uwanjani na kutajwa jina alipoingia ambaye hakushangiliwa na waliokua uwanjani? hebu akina msigwa na makonda watuoneshe video za tukio lile la kuapishwa Rhamaposa kwamba viongozi wengine wote walipofika uwanjani watu walikua kimya isipokua magufuli kwenye kauungu.

#pili, hebu tuchukulie ni yeye peke yake alishangiliwa. nani alisema wananchi kushangilia kiongozi wa nchi nyingine maana yake ni kupendwa au kukubalika? wale wananchi waliulizwa wote walikua wanashangilia nini? nani ana ujasiri wa kusema kwamba walikua hawashangilii kuona rais dikteta, mkatili, mshamba, na wa ajabu ajabu waliyekua wanamsoma mitandoani na kumsikia vyombo vya habari?

#tatu, walikua wanamshangilia kwa lipi haswa? maamuzi ya kienyeji ya korosho yaliyoletea nchi hasara? kupigwa kwa lissu? kupotea ben sanane? kukandamiza uhuru wa babari? kuonea wapinzani? kuharibu uchumi? kuahidi kutunyonya? kumteka MO na kumwachilia? lipi hasa waliwajulisha manabii wake kwamba walikua wanamshangilia?


Kumekuwa na utukufu sifa za ajabu sana anapewa magufuli. kila kitu na kila mahali anasifiwa magufuli. watu wako kwenye misiba ya familia magufuli anasifiwa na kushukuriwa. watu wako kwenye sherehe anafisiwa magufuli. watu wanatibiwa hospitali maguduli anasifiwa.

wananchi wakichimba hata kisima kijijini anashukuriwa magufuli. mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na hata wabunge wa ccm wakiongea na wananchi hawasemi tena serikali inafanya hili au lile. wanasema pesa za rais au rais atafanya. bunge linapisha bajeti ila miradi ikitekelezwa ni rais magufuli kafanya. hii ni hatari na itatugharimu.

Sifa zingine za wazi zinatolewa na viongozi wa dini nyuma ya mwemvuli wa kiimani. bila uoga wanamtukuza badala ya Mungu. akina mwanri wamefikia hatu ya kusema Mungu amshukuru magufuli. hii ni hatari kwa taifa. hatuna tena tofauti na nchi kama korea ya kusini na zingine kama hiyo ambopo kiongozi wa nchi anakua na hadhi ya kiungu pia na kuabudiwa na watu.

Jeshi nalo limeanza kuimba sifa za magufuli. mkuu wa majeshi siku hizi anasimama majukwaani kusema magufuli hoyee. haijawahi tokea hii tangu Tanzania iwe nchi. kama mumesikia kwa sasa kuna wimbo umetungwa na inaonekana ni JKT au moja ya majeshi yetu. kwamba wanatumia fedha zetu wanakaa chini kutunga na kufanya mazeozi ya nyimbo za kumsifia magufuli (tazama attachments).

Kinachoshtua kuhusu Magufuli ni kwamba hajawahi kumkemea yoyote hadharani kwa aina ya sifa anazopewa. hii anamaanisha anakubaliana nazo hata ile ya yeye kushukuriwa na Mungu. Sio hivyo tu bali magufuli mwenyewe amekua akionesha wazi kwa maneno na matendo kwamba watu wamashukuru au kumsifia kwa kazi anazofanya. akizindua ujenzi wa barabara kimara alimwambia mnyika asiongelee habari ya kodi kujenga barabara bali amsifu yeye kwa kujenga. alifika mbali kwa kusema kama ni kodi zilikuwepo miaka yote.

naendelea kuwakumbusha kuna mengi yanajengeka chini ya #MfumoMaguli au #MfumoJiwe ambayo yanaligharimu na yatalingarimu taifa.


Sam
 

Attachments

  • wimbo kumtukuza magufuli.jpeg
    wimbo kumtukuza magufuli.jpeg
    63 KB · Views: 26
  • wimbo kumtukuza JIWE1.mp4
    3.4 MB
#tazama manabii na mitume wa uungu wa magufuli wanavyotahiki kumtafutia sifa hata zisizo na maana. tunamsubiri Dodoma atuambie faida ya safari yake ila tunacholishwa akiwa huku nje kuaminisha kwamba anakubali. huu ni ujinga. huu ni upoyoyo. huu ni udhaifu. huu ni upofu. hii ni hatati kwa taifa.
 

Attachments

  • sifa za Jiwe SA.mp4
    4.5 MB
Simulizi ndefu lakini haina maana.umetunga Tunga tu maneno ambayo mtu asiye na UTAMBUZI atayakubali bila kuyapinga Wala kuyaboresha ili litimie ili neno linalosema wako waandishi pia wako wasomaji
 
Simulizi ndefu lakini haina maana.umetunga Tunga tu maneno ambayo mtu asiye na UTAMBUZI atayakubali bila kuyapinga Wala kuyaboresha ili litimie ili neno linalosema wako waandishi pia wako wasomaji
 
Hivi lissu angesifiwa na kushangiliwa huko anakozurula Ulaya na kwingineko, huu uzi wako ungeuandikaje?
 
Nlichokiona hapo ni kuwa Makonda kadhihirisha kuwa kuna mashaka makubwa juu ya rais wetu. Sasa wataanza hadi kuhonga ili aalikwe rais wetu aonekane anapendwa na mataifa ya nje. Ila isije akawa kituko maana watu wengi wanapenda v2 vya namna hiyo ila Ima letcha think watcha think and letcha know watcha know.
 
Ulaya watu hawasifiwi bali wanahehimiwa kwa michango yao. Mwambie Magufuli aende ulaya kama atashangiliwa. Ulaya watu wanajitambua.
Magufuli sio mtu wa kukimbilia wazungu kama akina nanihii....!!!!
 
Simulizi ndefu lakini haina maana.umetunga Tunga tu maneno ambayo mtu asiye na UTAMBUZI atayakubali bila kuyapinga Wala kuyaboresha ili litimie ili neno linalosema wako waandishi pia wako wasomaji
Watu kama wewe akili ndogo hamuwezi kuelewa, hata bungeni ni ndiyoooo.. Pumbavuuu
 
Sio kwamba hataki, bali wazungu sio watu wanaolewa habari za watu waongo.
Mwaka 2019 kubabaikia wazungu nikuwa na fikra za ujima, imefika wakati wafrika kujijengea natumanini yetu wenyewe kuliko kutegemea wazungu ndio watuambie wapi tunafanya vizuri na wapi tunafanya vibaya. Mfano mzuri ni ripoti feki ya IMF.
 
Mwaka 2019 kubabaikia wazungu nikuwa na fikra za ujima, imefika wakati wafrika kujijengea natumanini yetu wenyewe kuliko kutegemea wazungu ndio watuambie wapi tunafanya vizuri na wapi tunafanya vibaya. Mfano mzuri ni ripoti feki ya IMF.

Acha upotoshaji, hakuna anayesema kubabaikia wazungu bali kushirikiana na wazungu. Penda usipende mzungu hakwepeki, aidha umejipendekeza au vinginevyo lakini mzungu hakwepeki. We baki unalishwa maneno na mtu ambaye amefanya kazi za serikali kwa zaidi ya 25yrs na hajui lolote nje ya ajira. Mzungu ni habari nyingine zaidi ya asilimia 90 ya maendeleo unayoyaona wa ni wazo na ubunifu wa mzungu. Halafu huyo anayekuambua hajali mzungu anategemea hujuma kwenye box la kura ndio apate madaraka, kama sio wendawazimu ni nini?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom