CHURA: JKT Taarab walitisha sana enzi hizo ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHURA: JKT Taarab walitisha sana enzi hizo !

Discussion in 'Entertainment' started by Ms Judith, Jan 3, 2012.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Wapendwa,

  Hakuna ubishi kuwa huu wimbo ni wa zamani sana na sijui mwaka gani ulitungwa na kuchezwa ila kwa kweli naupenda sana maudhui yake!!

  Wakubwa wanasema umejaa mafumbo matupu, anayejua unafumba nini, naomba atujuze.

  WIMBO: Chura
  ALBUM: Sina hakika
  KUNDI: JKT Taarab  MASHAIRI

  1. Chura nakuulizia unipe jibu makini,
  kwa kila inyapo mvua wakimbilia bwawani
  Huna nguo za kufua na wala huna sabuni,
  nijibu yapate tua maji utayafanyani

  Chorus
  Chura punguza vituko na wako uhayawani,
  umezua sokomoko watu hawaeleni
  Ukivunjika mgongo, dawa atakupa nani?


  2. Mwenzenu nilikisia ni mlinzi kisimani,
  mtu utamzuia maji akiyatamani
  Akaja dada Rukia na ndooye mkononi,
  chura ukajing`atua ukajitosa pembeni

  Chura punguza vituko ………………………

  3. Chura bora kuamua wende kulima shambani,
  mazao kujipatia wende kuuza sokoni
  Nguo kujinunulia isitiri maungoni,
  au ukitaka ndoa nenda kaoe nyumbani.

  Chura punguza vituko ………………………

  Tuendelee kuburudika kwa raha zetu na tukifurahia na kumshukuru Mungu kuingia mwaka mpya 2012..

  Naomba mwenye audio clip, tafadhari atuwekee,

  Mbarikiwe sana wapendwa.

  Glory to God!!
   
 2. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,099
  Likes Received: 1,277
  Trophy Points: 280
  eeeh ...chura ..kibokooo

  wee chura wee.....

  Twende kazi
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,436
  Likes Received: 22,352
  Trophy Points: 280
  hizi ndio taarab zenye akili, nyepenyepe hawawezi kuzicheza
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mtu chake, tupe basi maana ya fumbo hilo la chura!!
   
 5. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kiharage.
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hata mimi kwa kweli naupenda sana wimbo huu
   
 7. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Naona Huu wimbo umeupenda sana na thread nyingine umeanzisha.hizi ndizo taarabu fumbo lake lahitaji kufikiri kwa kina!
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  take easy mpendwa. hiii iko entertainment kama burudani tu kwa mwenye interest na ile iko jukwaa la lugha na kuna tu vitu ninataka wajuvi wa kiswahili watusaidie

  ubarikiwe sana

  Glory to God!
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  whata are trying to say SOBY????
   
 10. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu ni mmoja wa nyimbo za Taarab nizipendazo. Nyingine ni Njiwa peleka salamu, Macho yanacheka moyo unalia, Kifo cha Mahaba, Sabalkheri mpenzi, Nahodha wa mashua, Nyuki, Mahaba ya dhati, Nimezama etc.
   
 11. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,099
  Likes Received: 1,277
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha...Fumbo hilo..we litegue tu...si ndio umeanzisha...ukishindwa watatusaidia
   
 12. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  chura.....................

  ni kijana wa kijiweni na asiye na kazi ambaye kutwa kuchwa hukaa akipiga soga................... bwawa ni setting yta mjini na maisha ya mjini kwa ujumla.............. pamoja na makeke yote kuwa najua maisha na starehe za mijini lakini ukweli ni kuwa hata yeye anazisikia kwenye bomba tu................. kwa sababu ya kukosa jeuri ya pesa............... wala hana kazi ya kumuingizia kipato.................. hawa ndio wale unaowakuta kandpo ya barabara wanajua kila gari ni la nani ila wao hawana japo baiskeli................

  maji ni starehe na anasa za za mijini.............

  dada rukia anawakilisha wenye pesa zao hapa mjini................

  anashauriwa arudi shambanmi alime na akipata nazao auze na kujinunulioa nguo zimsitiri................. manake anatia aibu kwa kuanza kutembea mtupu kwa uvivu wa kufanya kazi................ na kama anatafuta mchumba/kazi, basi hata huko shambani (nyumbani) wasichana (wachumba/kazi) wapo na ni bora akaoe huko (akafanye kazi za shamba) kuliko huku mjini............... for obvious reasons................
   
 13. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160

  Mkuu Ms Judith naona umeomba audio clip ya Wimbo wa Chura. Bahati mm ninao na link ni hii hapa chini.

  Hizi nyimbo ni adimu na mimi mwenyewe nimehangaika sana mpaka kupata audio zake - anyway kama unahitaji na nyingine kama Njiwa Peleka salamu & others just ask na ntakupatia Link.

  Nawatakia usikilizaji mwema

  Note: By the way, kundi ni JKT na siyo JWTZ  Audio clip: Chura - JKT Taarab

  http://dl.dropbox.com/u/52629254/dotworld/songs/T-Chura.mp3
   
 14. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  sijui nitumie maneno gani kukushukuru. kwa kweli nimeusave na ninaburudika hadi ma bone marrow zinatikisika! jamani, naona ngoja nikushukie kwenye PM manake hapa naweza hata kuambulia ban kwa sababu ya furaha ya hii burudani uliyonipa leo!

  Mungu akubariki sana mpendwa,

  Glory to God!
   
 15. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kinyozi
   
 16. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Wakuu, hizi nyimbo zote ntaziweka hapa Jukwaani muda si mrefu ili muweze kudownload & kuzisikiliza!

  Stay Tuned!
   
 17. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
 18. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
 19. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
 20. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
Loading...