Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,079
- 9,245
Alberto bana sema ukweli. You never liked zitto kwani ulikuwa unastrategize againgst him kila usiku! Ulikuwa unakusanya evidences againgst him hadi alipotoka madarakani. Problem was, you never liked Ruge either so ulikosa strong insider backing.
Lakini at the end baada ya zitto kutoka madarakani na kufanikiwa kusambaratisha mpango wake wa kumrithisha demu wake madaraka, tofauti zilitoweka. Zitto mwenyewe alijivuna kwamba hana marafiki/maadui wa kudumu bali interest ya kudumu. Huyo Omar by then alikuwa mvuta bangi tu ndo maana hata wakamchana viwembe pale Nkuruma wakati wa kumnadi shemeji yake, Mary mugurusi. Nobody took him serious na ndo maana watu walipuuza human right chapter ya udsm wakati ule kwa sababu tu iliongozwa na Omar.
Hivi yule Yank alietimuliwa na Government eti ni Mganda hafai kuwa kiongozi pale UD anaitwa nani
0767 533 433
0785 533 433
Alberto
Nakumbuka nlikuwa first year msando ulikuja nkruman na kauli ya bora kuishi siku moja kama simba kuliko ... Pale zitto,kule mary mugulusi,you guys were rocking,please remain good for Tanzanians na hasa upinzan dhidi ya ccm,you were born to influence
Nakumbuka akina Kervin Njunwa walifukuzwa chuo kwa muda! Duu long tym agoNakumbuka wakati niko Mlimani, mwaka 2002/3 kulitokea Mapinduzi yalishindwa dhidi ya Serikali Halali ya Wanachuo iliyokuwa chini ya Rais Francis Kayombo!
Najiulizaga what was the Motive Behind that mapinduzi na nani waliokuwa Nyuma ya yale Mapinduzi(Ambayo hata hivyo hayakufanikiwa)? Mkuu Waberoya nadhani ulikuwamo katika ile Serikali iliyokoswa koswa kupindulia naomba unitoe Kizani
Wee kweli tulikuwa wote! Ahhaaaaaa haa
H.C Dk. Kikwete hakuwahi kuwa Rais wa DARUSO
Kipindi munachozungumzia ni chenu na hakikuwahi kuwa na impact yoyote kwa mTZ wa kawaida. Hayo yote musemayo was just part of your student politics commonly geared by money need, sexuality or even blind imitation of life. Then, nini sababu ya kuleta topic kama hii hapa jukwaa la siasa. Au hata JF! is this a forum of lost and found? Do you assume everyone of us to be interested with UD bussiness? wengine hatukusoma hapa nchini na tunaona kama mulikuwa watotot hadi chuo kikuu! pAre you forcing to be something you can't be anymore?
Ktk historia ya nchi hii vipo vipindi viwili tu ambavyo UD ilitikisa nchi kwa leadership na moral reasoning. Ni kipindi cha Kuikataa JKT ya Nyerere na Kipindi cha utawala wa mwinyi yaani DARUSO ya Bw. matiko. Hivi ni vipindi viwili ambavyo siasa ya wanafunzi iligeuka kuwa ni ajenda ya nchi.
Siwakatishi tamaa lakini poleni kwa kudhani kwamba you did your best. Haitoshi na ninachokiona kwa uhakika. Hii siyo topic ya kuleta Jf maana haijawahi kuwa mjadala wa kutamaniwa na wa Tz wengine. Hayo ni yenu.
so, Mod., can you shift this trd to mambo mchanganyiko?
Maybe we should discuss facts and not who went out with who ? Dada wa. FOE
Aaaaaaawapi! Wewe utakuwa kati ya wale ambao watu walikuwa wakipanga mkakati wa kuandamana kesho yake unajidai either mama yako yuko Muhimbili au eti unatangulia town tutakukuta huko...... na mimi nilikuwa UD kipindi hiki ila nilikuwa too busy kubalance academic na ujasilimali hivyo sikushiriki kabisa politics za Daruso..."
...my honest opinion niliwaona wanavugu vugu karibu wote wa Daruso kama vi puppets fulani hivi, huku wengine wakiitumia Daruso kuganga njaa.
...guys,may I know a little bit about Introduction of HELSB during your university era!? And the trip to SA!?
lakini hebu tafakari, kundi lile la udsm kipindi kile kuanzia kunji la 2001 hadi 2005, ndilo linalo drive mapambano ya mabadiliko tz kwa sasa.
Pamoja na kusikitishwa na habari hizi mbaya za kifo cha Kaishozi, nimesikitishwa zaidi na habari kwamba mpiganaji Harun Kimaro naye ni marehemu kwa sasa. Huyu alikuwa mpiganaji wa kweli na ndiye aliyeongoza maandamano pamoja na Prof. Shaba kwenda Ikulu kuitaka serikali ifute mpango wake wa kuchangia elimu na kuwaachia madaktari wanafunzi kadhaa waliopakiwa kwenye basi moja na kudai walikuwa wanapelekwa makwao. Yalikuwa ni maadamano ya kwanza ya bila kibali cha serikali kufanyika na yakafanikiwa.
Kuna uzi uliwekwa humu na Waberoya, "Esoteric: Uhusiano wa Zitto, JK, Salim AS, Ridhiwan, Omar Ilyas..." Japo ulifungwa, ukiupitia waweza pata picha halisi ya hawa waungwana.huyu Omary Lyas ni nani?
usaliti wa zitto upo damuni
Agreed lakini pia inawezekana waliopita UDSM kabla ya hapo ndiyo waliopigania mazingira kuendesha hayo mapambano ya mabadiliko sasa. Wengine tumezeeka na kuwa wazee wa busara tuu, wengine ni marehemu kwa sasa na wengine wameamua kuachana kabisa na siasa kutokana na misukosuko waliyokumbana wakati ule wa mfumo wa chama kimoja.
Kama alivyosema David Djumbe, "changamoto zinazojitokeza wakati wa uongozi vyuoni huwa ni mtihani sana na ndio maana wale wanaomaliza migogoro hiyo vizuri huwapa ujasiri zaidi na hatimaye wengi wao huweza kuwa viongozi wazuri...lakini wale wanaoumizwa na changamoto hizo wengi hukosa ujasiri wa kuongoza tena na hivyo kupotea kabisa kwenye siasa..."
Kuna mpaka wengine walishawahi kuwa Rais wa Duruso kwa siku tatu tuu kabla ya kufukuzwa chuo. Cheki hii post ya Kashaijabutege, "Jasson Kishozi (RIP) alikuwa Rais wa DARUSO (Overall-Mlimani na Muhimbili) kwa kipindi cha siku tatu 6-9 Februari 1992. Alifukuzwa Chuo Kikuu na wenzake 9 ambao walisimama kidete kupinga mfumo mbovu wa uchangiaji wa gharama za elimu ya juu na kutetea uanzishwaji wa vyama vingi. Wanafunzi hao 10 walifukuzwa tarehe 10 Februari 1992. Waliofukuzwa tarehe hiyo ni hawa:
1. Mh. James Mbatia (Electrical Engineering-4th year)-Mwenyekiti NCCR-Mageuzi
2. Dr. Harun Kimaro (MD 5th year)-Marehemu (Alikuwa mshauri wa MDC Zimbabwe)
3. Fabian Lutalemwa (Pharmarcy 4th year)
4. Rwekamwa Rweikiza (B.com Marketing-2nd year)-Alikuwa Rais wa Daruso Mlimani siku 3.
5. Idrissa Alnoor Ruta (Engineering Civil 4th year)-Mrehemu
6. Ludovick Kashaju Bazigiza (BA Ed 4th year)-Marehemu
7. Mosena Nyambabe (Engineering-Civil)
8. Dr. Kelivin Mmari (Electrical Engineering-2nd yr)-Ni lecturer wa IT Oregon University, USA
9. Jasson Kaishozi (BA Ed-2nd yr)-Marehemu
10.......Kimweri (BA Economics 3rd year)-Marehemu
Baada ya kufukuzwa Kaishozi alikaa mtaani na baada ya miaka mitano alirudi kusoma sheria [inasemekana baada ya Generali Ulimwengu kumwombea kwa Prof. Luwanga na Luwanga kumkubali on the condition kuwa hatajihusisha tena na siasa za chuo]. Alipomaliza alipata kazi kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, kama wakili wa serikali. Kesi iliyompa umaarufu ni ile ya ZOMBE, ambapo yeye ndiye alikuwa mkuu wa jopo upande wa mashitaka (serikali)."
Chanzo: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/87973-ulimjuaje-marehemu-jasson-kaishozi-wakili-kesi-ya-zombe.html.
Kwenye uzi huo huo, Tiba nae anaongezea,