Mapinduzi yaja Tanzania

Wanangoja nini? si wampe kitu ya panya a rest in piece amen
 
I wish it to be soon. Wasiwasi wangu ni kwamba kama hii katiba haitabalika ni kwa tusitegemee CCM kuanguka, pili lazima tuwe na tume huru ya uchaguzi ambayo si mali ya Chama chochote. Failure to this nothing can be done!!! Nchi ya ajabu sana hii jamani, uchumi unaporomoka hata kwa watoto wanaliona wazi. Lakini utamkuta MPUMBAVU aliepewa dhamana na wananchi akidanganya jukwaani kuwa uchumi unakua, cjui anamdanganya nani. Watanzania, kwa uhakika ni wakati muafaka wa kuamua. Tuachane na hawa vilaza ambao wanafikiria mitumbo yao tu!! Hawana uchungu na Taifa kabisa. Lets change our mind coz your pain is my pain!
 
naandika haya kyk rangi hii si kwa kupenda bali nashinkizwa na hali ngumu ya maisha ktk nchi hii, juzi ktk kusoma magazeti ili nipate habari nili bahatika kupitia kibonzo wakati si kawaida yangu na haya ndiyo aliyo andika mtunzi wa kibonzo hicho ( mwalimu ame chola bendera ya tanzania, ubaoni kisha ana uliza maana ya rangi zilizopo ktk bendera husika, alipo uliza rangi nyeusi ina maanisha nini?. Mwanafunzi akajibu....(rangi nyeusi ina maanisha giza). Je tunalazimika kukubari kuwa kadiri giza linavyo zidi mapazuko hukaribia?, wenzetu wa malawi wame amka kutoka katika usingizi mzito wa kifikra, na sasa wanadai mabadiriko. Je ile dhambi ya mohamedi bouazizi ina itafuna africa?
 
Ndugu watanzania wenzangu!! Tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia jinsi nchi yetu yenye neema zote ambazo taifa lolote linaloweza kuclaim kama limejaaliwa tunazo, jinsi inavyoendeshwa; Huku ikiwaacha wananchi wengi tukiishi katika lindi kuu la umasikini linaloendelea kuwa compounded na
1. Unprecedented power shortage - Ni full kiza, shughuli zinazotegemea umeme hazifanyiki tena kwa uhakika, watu wamekosa kazi kwa kutokana na hilo
2. Bei Za nishati zipo juu, Petroli bei juu, mafuta ya taa bei juu, gesi bei juu, gunia la mkaa ni zaidi ya elfu 35
3. Bei za vyakula zimepanda kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji
4. Wabunge wetu walioteuliwa kutuwakilisha, wamejkalia kuwakilisha vyama vyao na si maslahi ya taifa, hoja inayolenga kumkomboa mtanzania ikitolewa na mtu ambaye si chama cha waliowengi bungeni kinachofuata ni kuzomewa na kejeli, huku watanzania tunaendelea kuumia na hali ngumu ya maisha.

Jamani ndugu watanzania wenzangu, tutaendelea kunung'unika mpaka lini, ni lazima tutangaze mwisho wa hii hali kwa faida yetu na watoto wetu na vizazi vijavyo.

Je ni nini kifanyike ndugu watanzania wenzangu???. Ninaomba tujadiliane mpaka tupate Muafaka. EWakati ni huu.
Kuna mwanafalsafa alisema, Mwenye kosa si anayefanya uovu, bali ni yule anayekaa kimya wakati uovu unafanyika!!
 

Many thanks!
 
wandugu hii thread mbona inaishia kwenye screen za computer tu? shime wa-tz, twendeni bara barani sasa, hakuna wakumuogopa, shimbo alikuwa anaabudiwa na wanajeshi, asaivi wana hasira naye watatu support by any means, nao wanadhulumiwa, tuwaache hao manjuka wa IGP mwema, tukiingia ikulu tutawapotezea mbali, nafasi zao zitachukuliwa na mgambo wa city.
 
Tz uoga umewazidi,hawajui kuwa ni haki yao kuishi maisha bora kwa kodi wanazolipa!
One day itakuwa kama misri tuendelee kuwaelimisha
 
Tz uoga umewazidi,hawajui kuwa ni haki yao kuishi maisha bora kwa kodi wanazolipa!
One day itakuwa kama misri tuendelee kuwaelimisha

Jamani huko kwa mitaani bado vuguvugu letu litafanyika humu humu kwenye jamvi mpaka shina na mizizi itafikiwa.
 
hili la kukosekana kwa mafuta naweza kulihusisha na Lowasa
 
Imekuwaje leo unafufua uzi za mchungaji usiku wa manane(bongo)? nimeona ile ya ku win mapauni ya malikia.
hahhah.. Nduka wewe mafuta unanunulia wapi na sisi tuje?
naona unaenda kinyume na signature yako mara zote..nafurahi sana nikiisoma
 
Yard ya serikali Kurasini, ila unakwenda usiku wa manane, lita ni 1100/-. leo kwa sababu ya crisis wanataka buku mbili. Kama unaroho ya paka nikupe mtu wangu wa hapo yadi
hii ndio nini? japo nashukuru kwa ofa yako ila tutapeana watu hadi lini..? ccm mmekaa kifisadi fisadi tu mda wote.. nadhani unanielewa sana..wananchi wanapata shida mwambie mkulu hatumtaki na mapinduzi yanakuja soon na ataondoka
 
hii ndio nini? japo nashukuru kwa ofa yako ila tutapeana watu hadi lini..? ccm mmekaa kifisadi fisadi tu mda wote.. nadhani unanielewa sana..wananchi wanapata shida mwambie mkulu hatumtaki na mapinduzi yanakuja soon na ataondoka

Mapinduzi kwa mtindo huo yataendelea tu kuninufaisha, naomba hata kesho asubuhi nikiamka niyakute. wewe subiri hadi rais atakapo amua upate mafuta.
 
Mapinduzi kwa mtindo huo yataendelea tu kuninufaisha, naomba hata kesho asubuhi nikiamka niyakute. wewe subiri hadi rais atakapo amua upate mafuta.
Rais atakapo amua au Lowasa atakapo amua..hawa ccm ovyo kabisa..hata kama mnaiba ibeni lakini kuna huduma za muhimu sana msizibe hivi jamni..kuweni na aibu mbele ya mwenyezi Mungu
 
Rais atakapo amua au Lowasa atakapo amua..hawa ccm ovyo kabisa..hata kama mnaiba ibeni lakini kuna huduma za muhimu sana msizibe hivi jamni..kuweni na aibu mbele ya mwenyezi Mungu

Sasa hapa na mimi si ni CCM, mbona sio hovyo bana, hili ni suala la usalama wa taifa usiwe na wasiwasi serikali imara ya CCM inakuja na suluhisho kabla haujaamka kwenda kazini kesho. Endeleeni kutuunga mkono.
 
Sasa hapa na mimi si ni CCM, mbona sio hovyo bana, hili ni suala la usalama wa taifa usiwe na wasiwasi serikali imara ya CCM inakuja na suluhisho kabla haujaamka kwenda kazini kesho. Endeleeni kutuunga mkono.
offcoourse serikali yenu ni imara kuanzia ndani ya cc hadi nje...mshashindwa nchi hi haihitaji kuwa na tochi kumulika kuwa mkuu uwezo wake wa kufikiri umeshafika mwisho
 
Ubavu wa kuleta mapinduzi nyie hamna na Wabongo waliyo wengi hawana. Ukweli ndiyo huo. Nyie endeleeni kupiga domo na kupongezana kwa kauli hewa, ilhali mkijua wote ni waoga wakubwa.
 
uwezo wake wa kufikiri umeshafika mwisho

Siku uwezo wake ukishuka hata kufikia level za wale wahuni pale kinondoni, mtajua serikali nini. Huyu ni genius hajapata kutokea kiongozi mahili baada ya Nyerere kama JK, ni kwa busara yake tu hadi leo mnaweza kuendelea kumtukana, ila Mungu anawaumbua kila siku, na ninyi mnalifahamu hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…