Mapigano Wakulima na Wafugaji yaibuka tena Mvomero-Morogororo

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la "Mwanu"

Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu hekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya Kimasai

Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.

Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .

Chanzo: Star Tv Online

mwigul.jpeg
mwig.png
mwigu.jpg
Mwigulu.jpg
 
hivi kwanini hili gogoro haliishagi au ni kaini na abeli wanaishi hapo mvomera?imasikitisha sana
 
Dah! Huku Songea kitoweo kinapanda bei ilhali huko mvomero inaonekana ni takataka! Please Waziri Mwigulu na Lukuvi chukueni hatua kumaliza migogoro ya aina hii
 
Duuu huu mgogolo unanyamazaga kimyaa.. Ila ukiibuka ni balaaa.. Mwigulu please maliza huu mgogolo
 
Nimesoma na kutafakari. Nimebaini hakuna mapigano hapo. Bali wananchi walikuwa na hasira ya mifugo kula nusu ekari ya mazao. Hebu fikiria mifugo inakula mazao kiasi hicho na wafugaji wanaangalia tu. hao si wauaji? Ila nawapongeza wakulima kwani wangemuua binadamu ingekuwa habari nyingine
 
Yanapotokea mapigano baina ya wakulma na wafugaji, mara zote wafugaji ndo chanzo
Simple and clear, mashamba yako stationary wakati mifugo inatembea kufuata mashamba. Wamasai hawa watiwe adabu. La sivyo wananchi wawashughulikie kadiri wanavyona ni sawa. Hakuna namna.
 
Waziri Mwigulu nchemba hawa watu hawafai kabisaaaaaa na hawana huruma kwanini wakate miguu na wengine kuwauwa hawa wanyama kwa nini wasiwakamate tu na kuwasaka wamiliki

Haikubaliki waliouwa pia wakamatwe nakuchukuliwa hatua

upload_2016-2-9_13-56-51.png
 
Yaani huu mgogoro ni wa aiku nyingi sana. Naamini utamalizwa na uongozi wa awamu ya Tano
Kamwe serikali ya CCM haiwezi kutatua mgogoro wa wakulima na wafugaji au mwekezaji ye yote kwani ndiyo silaha wanayoitumia kupata kura kwa kuendeleza umaskini!
 
nilikuwa na shama maeneo hayo Masai kaingiza ng"ombe wake shambàni kwetu namuuliza ananiambia ikale wapi lakini Wa fugaji ni wamasai peke yao mbona wama ng"ati hawana ugomvi wapo pia wasukuma kule Kilombero mbona hakuna mapigano hawa wamasai Wa Dogo ,kiteto, Mvomero, sunya leiseri mbona wagomvi sana
 
Back
Top Bottom