Mapigano makali yaibuka mpakani na Israel. Makombora ya Hamas yatua miji ya kusini ya Israel huku makubaliano mapya kuhusu misaada ikifikiwa

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,186
10,924
Ikiwa ni siku ya 110,zaidi ya miezi 3 tangu vita vianze mapigano makali yameripotiwa kwenye mpaka wa Israel na Gaza na kupelekea Israel kuamua kurudisha baadhi ya vikosi ilivyokuwa imeviondoa kaskazini ya Gaza.

Katika mapigano ya jana Hamas ilifanikiwa kurusha makombora kadhaa kulenga maeneo ya kusini ya Israel jambo lililoishangaza jeshi hilo la IDF.Baadhi ya makombora hayo yalidakwa na mfumo wa Iron Dome wa Israel.

Kwa upande mwengine Israel imefikia makubaliano mapya kati yake na Hamas kuhusiana na upelekwaji wa misaada maeneo tofauti ya Gaza.

Katika makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Qattar na Ufaransa sharti kubwa la Israel ni kwamba misaada hiyo iwafikie mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas.

Gaza combat surges anew as Israeli tanks storm back into areas they left

1705464820911.png
 
Tukiacha na ushabiki hawa HAMAS wanatisha Sana sidhani kama kuna kundi lingine wanaweza KUPIGANA huku wameshikia mateka kwa zaidi ya miezi 3.

Kwasababu eneo ambalo wanapigana vita ni dogo sana kama wilaya ya kigamboni lakini Israel anahangaika nao mwanzo mwisho
 
Tukiacha na ushabiki hawa HAMAS wanatisha Sana sidhani kama kuna kundi lingine wanaweza KUPIGANA huku wameshikia mateka kwa zaidi ya miezi 3... kwasababu eneo ambalo wanapigana vita ni dogo sana kama wilaya ya kigamboni lkn Israel anahangaika nao mwanzo mwisho
walijipanga mapema

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Hawa hamas mipango yao waliipanga vipi, kaeneo kadogo kama gaza, jeshi kubwa la israel imeshindwa kupata mateka mpaka leo.
Mji umegeuzwa kifusi lakini bado unasikia wanashambulia.. Wapo gaza kweli hawa.!?
Wapo hapo hapo ghaza mzeee
Ila jamaa wameamua tu liwalo na liwe yaani mpaka idf wenyewe hawaamini kinachoendelea

Mossad na wengine kadhalika kina CIA wote wanashangazwa na anachokifanya Hamas

Wanaume kama hamas na mimi tumebakia wachache sana yaani
 
Vita ni mbinu na mikakati Leo hii kundi ambalo lilikuwa linaonekana si lolote si chochote, linamtoa jasho moja ya majeshi bora kabisa duniani.

Hili la Hamas linanikumbusha jinsi Wasomali walivyo wafurusha majeshi ya USA katika ardhi yao.
Ila kinachoendelea ghaza sitaki kuamini kama israhell jeshi bora kama tulivyokua tunaambiwa

Watu wamejaribu kila namna kuwatetea israhell ila ukweli unabakia pale pale kwamba israhell wakawaida sana

Yaani israhell wametumia mpaka uongo kisa kupambana na hamas tu

Mwanzo walitudanganya wameigawa ghaza kusini na kaskazini kumbe uongo mara wameikalia jumla kaskazini ya ghaza kumbe uongo

Ukweli pekee ambao ukiambiwa unatakiwa uuamini hata kama hujauona ni kwamba israhell inaua watoto na watu wasio kua na hatia na kuripua tu majengo yasio husika na lolote

Maana kwa takwimu rasmi zinasema kwamba 70% ya makazi yote ya ghaza yamaeharibiwa na israhell hasa kule kaskazini ila sasa hamas wanatokea huko huko kulikpo haribiwa zaidi na wanashambulia ndani ya israhell

Jana nlimskiliza mtangazaji mmoja wa aljazeera anakwambia inaonekana bado hamas wanauwezo wa kushambulia ndani ya israhell tofauti na wanavyo tangazia umma (anasema aliwanukuu raia wa israhell wenyewe wakisema haya)
 
IDF wameanza kurudisha vifaru tena Gaza baada ya HAMAS kuanza kuonyesha nguvu huko Gaza kaskazini!

Bila msaada wa Marekani hawa Israel hawawezi kusimama hata na HAMAS hawa
Nlichogundua nikwamba hamas walijipanga na vita ya muda mrefu kama walivyotangaza

Maana kwa kile walichokifanya jana nidhahiri walijua kabisa kama israhell lazima wataregesha baadhi ya wanajeshi wao waliowatoa

Kuna namna naona hamas wamegundua kwamba idf wanaudhaifu mkubwa hasa kupitia vita ya ardhini

Binafsi nategemea ghaza kuharibiwa zaidi na watu wasiokua na hatia kuzidi kupoteza maisha ila nategemea idf wanaoingia front watachinjwa zaidi

Mwisho kadri israhell inavyochukua muda mrefu bila kuimaliza hamas na kuimaliza vita yake kule ghaza inazidi kuuonesha watu hasa jirani zake kwamba israhell ni over-rated sanaaa
 
Back
Top Bottom