Kariakoo nilikuta mchele "dizaini moja" lakini lebo mbalimbali.
Hali hiyo ilinisukuma kumuuliza mfanyabiashara pale, kwanini mchele ni "mmoja" lakini bei tofauti? Alichonieleza kilinishangaza sana, lakini baada ya kutafakari niligundua kuwa ni kweli na sahihi.
Alinieleza hivii? 'Mtu mwenye fedha zake hapendi vitu vya gharama nafuu'.
Kwa hiyo anachokifanya yeye ni kutengeneza lebo za gharama tofautitofauti kwa mchele uleule na kupata faida kubwa sana.
Nimechukulia mfano wa mchele kuonesha jinsi binadamu anavyopenda vitu ghali, vitu vya gharama hata kama uhalisia vitu hivyo viko sawa kiuthamani na vitu vingine.
Hivi, kwa mwanamke anayejitambua na kutambua uthamani wa wake aliojaaliwa na M/Mungu, anawezaje kujirahisisha kwa mwanamme kiasi hicho?
Ndiyo maana kizazi cha sasa wasichana hawaoleki, wanaishia kuzalishwa majumbani na kuletea kashifa wazazi na familia.
Sijadili uhawara au mapenzi nje ya mfumo, hapana.
Ninajadili mahusiano ya kindoa.
Mwanaume kakutongoza kiutanitani, tena kwa siku moja tu, tayari "unayeyema"
Mwanamke mzuri kwa mwanaume ni mwanamke mgumu.
Kataa mtongozaji, mtukane akukome, kamshitaki kwenye "uongozi" ili wamkanye asikufuatefuate, mwambie wazi haumpendi, mzungushe sana kumpima. Anayekata tamaa mapema si muoaji.
Hiyo mbinu ni chekecheo la kumpata mwanaume "mwenza".
Masimango na manyanyaso kwenye utongozaji ndiyo humuongezea thamani mwanamke na kumtofautisha kwa mbali kabisa na mwanamke "maharage ya mbeya" Waoaji hawapendi mwanamke wa rahisirahisi.
Onyesha uthabiti wako na msimamo kwa wanaume wakutakao ama uwatakao, watakuheshimu na ndiyo utapata mwanaume halisi wa chaguo lako. Vinginevyo utatumiwa kama karai la zege, ambapo baada ya kutumika hutupwa "stoo" bila kusafishwa.
Hata huyo wa nje, usiende, kwa sababu haujahalalishwa na wazazi kuweza kuishi nae.
Kama anakupenda, afunge safari aje akupose akuoe.
Vinginevyo mama " yeneyako".