Binti naona maisha yanakuchanganya hebu kaa tuliza akili, hujachelewa, usifikiri kuna kitu cha bure kwenye hii dunia, anaweza akachakaza papuchi yako na ukarudi Bongo na ndala. Kwanini usitumie akili ulizopewa na nguvu kujipatia kipato?
Hivi unajifunzaga kweli kwa watu waliofanikiwa kwa juhudi na nguvu walizotumia zikionekana wazi (ambao hawakutegemea kuchuna mabuzi).
Tulia tafuta kitu cha kufanya, na wewe uwe na maisha yako, na pia kama ndiye Mungu aliyekupangia atakua wako tuu. Hata bila kuchuna mwanaume (kama unavyowaza) unaweza kufanikiwa.