Mapenzi yamebeba vifo

Mapenzi yamebeba vifo

Story yako inafundisha sana hasa Kwa sisi wanaume,ngoja niimalize bia nilud Kwanza home nakachek familia.
 
Asante sana kwa ushauri wengi wamekuja inbox na wengi wamenishauri njia moja ya kupona ni kuamwua kuwa na yesu kama ni hilo tu mimi sioni kama nitashindwa ingawa najua kila jambo linachangamoto zake. nimekubali kuokoka uzuri mimi ni mkristo tangu tangu udogo wangu lakini sikuwa mwokovu ninachohitaji mimi ni kupona kama yesu mnae niambia ndio dawa basi mimi nitaitafuta hiyo dawa

Wokovu hauondoi virusi mwilini. Unakupa tumaini na sababu ya kuishi maisha ya ushindi.
 
Pole sana dada usijaribu kusita kuomba Dua na kumrudia muumba wako hakuna kinachoshindikana chini ya jua
 
Siku moja walipita watu ofisini wakiwa wanahamasisha tupime afya zetu mimi nilikua mmojawapo nilipima na ndipo majibu yangu yakaja am HIV POSITIVE ndugu zangu sina cha kuwaambia maana usiombe uambiwe una virusi vya UKIMWI
Ushauri wangu nenda ukapime sehemu nyengine tena, Kuna baadhi ya wakati vile vipimo huchanganya(chako akapewa mwengine na kipimo cha mwengine ukapewe wewe). Jaribu kwenda sehemu kama 3 tofauti kupima tena kama ukipata majibu sawa hapo kubali matokeo. Lakini kama ikitokea upo positive basi angalia dawa za kienyeji au za hospitali ziweze kukusaidi, kila maradhi yana dawa yake muhimu kuipata na kufata masharti yake tu. Nakutakia afya njema na maisha marefu ya furaha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole sana my dia. Mungu ndo mpangaji wa yote na ndio muamuz wa yote. Kubwa nikuamin tu.
 
Pole sana.
1. HIV siyo ukimwi
2. Nenda kapime sehemu nyingine upate uhakika usije jikondesha bure kumbe u mzima.
3. Anayekupenda kweli atakukubali kama ulivyo wapo wanandoa wanaishi mmoja ni HIV + mwingine hana na maisha yanaendelea.
Cha msingi ni kufuata ushauri wa wataalamu.
 
Kuna wakati sisi wanaume huwa tunakuwa kama shetani vile.

Usikate tamaa mapema dada, muombe Mungu akusaidie na kuwa faraja yako kuu ktk haya mapito yako.

 
Nimesoma mpaka nimetetemeka... dada pole sanaaa sanaaaaa huu sio mtihani ni kitu cha ajabu, inatisha sanaaa, nimeumia sanaa utazani wewe ni dada angu wa damu, ntakuombea na Mungu atakubariki.
 
Wazo la kupima tena naunga mkono.Kuna ndugu yangu alishawahi kuambiwa anaukimwi hospital ya wilaya magu wakamwanzishia na dozi na alionyesha kweli anaukimwi ukimuagalia kumbe alikua na maradhi mengine na vipimo vya awali walikosea mwanaye alipokwenda mkoa na kumpeleka hospital nyingine kupima akaonekana hana ukimwi akarudi tena magu hopital akaonekana hana ukimwi .....ikawa ajabu kumbe aliyempima sijui alikosea na magonjwa nyemelezi aliyokuwa nayo kutapika mara kwa mara ni wrong dozi ya pressure alikuwa amepewa...please jaribu kupima tena na mwenzi wako na kama utaonekana unao fuata masharti na utaishi muda mrefu tafauti unavyofikiria.
 
Nawaambiaga Wanawake achaneni kabisa na wanaume mnaowaona wana swaga ni majanga sana hao watu wakimbieni km ukoma ndani ya ndoa ni wazinzi wazuri sana

Pole dada hukustahili hayo
 
Huwa nina roho ngumu ya kibandidu ila kwa hapa kweli nimekosa machozi tu ila moyoni nimeumia.
Natamani hata nifunge na kuomba kwa ajili yako ili Mungu afanye kitu.
Ila amini, Mungu hutupatia kile kinachofaa kwa wakato unaofaa, hivyo katika safaro yako mruhusu Mungu atimize mapenzi yake kwako kwa ajili ya utukufu wa jina Lake.

Pole sana
 
Dah! Nimesikia uchungu sana. Pole sana na ujue virus vya ukimwi si hukumu ya kifo tumia dawa vile unavyotakiwa na humu huwa wanakuja wanaume ambao nao wana virus kutafuta wanawake wenye virus. Uwe unachungulia chungulia unaweza kupata bahati ya kukutana na mtu mkapendana. Pole sana.
 
Mimi pia nimewahi kuona kwenye TV mzungu kwa miaka mitano alikuwa anaishi akijua ana HIV virus na muda wote huo alikuwa anabugia madawa. Kumbe alikuwa mzima wa afya. Alipogundua hana baada ya kupima tena katika hospital tofauti akaamua kufungua mashtaka dhidi ya hospitali ambayo ilimpa majibu ya vipimo ambavyo vilikuwa si vya kweli.

Wazo la kupima tena naunga mkono.Kuna ndugu yangu alishawahi kuambiwa anaukimwi hospital ya wilaya magu wakamwanzishia na dozi na alionyesha kweli anaukimwi ukimuagalia kumbe alikua na maradhi mengine na vipimo vya awali walikosea mwanaye alipokwenda mkoa na kumpeleka hospital nyingine kupima akaonekana hana ukimwi akarudi tena magu hopital akaonekana hana ukimwi .....ikawa ajabu kumbe aliyempima sijui alikosea na magonjwa nyemelezi aliyokuwa nayo kutapika mara kwa mara ni wrong dozi ya pressure alikuwa amepewa...please jaribu kupima tena na mwenzi wako na kama utaonekana unao fuata masharti na utaishi muda mrefu tafauti unavyofikiria.
 
Back
Top Bottom