Mapenzi yamebeba vifo

Mapenzi yamebeba vifo

Hakika Mungu ni mwema na atakuonesha njia na kukusaidia mwanga wa kumulika maisha yako! Kamwe usihuzunike na kunung'unika kwani kila kitu hutokea kwa sababu maalum! Ipo siku utakuja kuipata furaha ya maisha yako zaidi ya unavyotamani kwa sasa.
Ila wanaume tupunguze ukatili kwa wanawake.....
 
pole sana dada....ila usikate tamaa. Mshukuru Mungu kwa kila jambo, pia fikiria kutengeneza maisha ya kiroho/ mbinguni, duniani tunapita, kwa wenye ukimwi na wasio na ukimwi....tutakufa tu, wenza utapata ukienda ktk nyumba za ibada na kujieleza, unaweza mpata mwenye positive au aliyetayari mtaishi vizuri na utasahau hayo yote. pole sana but all in all usimwache Mungu kwa maana huo ni mtihani kwko na inabidi ufaulu..usikate tamaa
 
Daaah kiukweli nimeumia nahisi kama nimm ila huyo aliekutenda hivyo mungu ipo siki atampiga bomu ambalo atalijutia maisha yake yt. mamy mungu ni mwema naamin hilo nijaribu na anajua mlango wakumaliza hilo ttzo dont give up mamy
 
Pole sana mwanamke mwenzangu, nimeumizwa na changamoto kubwa ulizokutana nazo katika ndoa yako,lakini nikwambie kitu kimoja tú kwamba kuna tofauti kati ya V. V. U na ukimwi. wewe umepimwa na kuonekana una V. V. U na sio ukimwi.ukimwi ni matokeo ya V. V. U kudhuru kinga ya mwili wako. Unashauriwa sasa mara tu unapogundulika na virusi hivyo ndani ya mwili kuanza kutumia dawa ARV mara moja ili kuzuia kinga ya mwili kushuka.na kukusababishia magonjwa nyemelezi ya mara kwa mara kitu kitakachodhuru utendaji kazi wako na kumuweka mwanao ktk wakati mgumu. Kadiri unavyoendelea kutumia dawa vizuri kabisa bila kuacha hata siku moja huvinyong'onyeza na kuzuia uzalishwaji wa virus hivyo na kama unapata chakula bora na muda mzuri wa kupumzika my sister your life will be better More than how your life was. Utakuwa na afya nzuri na maisha mazuri sana ila tu ukizingatia matumizi sahihi ya dawa.matokeo mazuri sana yatakuja baadae sababu ukitumia vizuri dawa zako pasina kuacha virusi huwa vinanyong'onyea mpaka infikia hatua vinashindwa kuonekana kwenye damu,( haimaanishi vimeisha)usikubali manabii wakudanganye please baki katika imani yako halisi huku ukiimarisha mahusiano yako na mungu. Kuhusu kupata mume wako wengi tu wanaohitaji wenza walio katika hali kama yako ni suala la muda tu. Jikubali kwanza kisha fanya maamuzi haraka ya kuanza kutumia dawa sasa.i wish ungekuwa karibu nizungumze na wewe kina sababu wewe ni wathamani sana H. I. V ni ugonjwa wa kawaida sana iwapo utazingati dawa NB: asikudanganye nabii au mchungaji yeyote uache dawa.
 
Back
Top Bottom