Mapenzi ni matumizi ya akili na siyo pesa wala vitu!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,530
34,358
Kwa vijana (wa kike na wa kiume) ni kawaida kuwaza kuwa nguvu ya mapenzi ni kwa mtu kuwa na mwili wenye kuvutia ama kuwa na pesa au vitu vya thamani vinavyotamaniwa na wengi. Lakini ushahidi unaonesha kwamba, mapenzi yaliyodumu na kuwapa raha wahusika, yalijengwa zaidi kwa akili na siyo kwa Pesa ama Vitu.

Ukiwa hujui jinsi ya kutumia vizuri akili zako, mapenzi yatakushinda hata uwe na pesa ama vitu vya thamani vya dunia nzima.
 
Mapenzi bila pesa ni ushogaa
Kwa uzowefu wangu nimegundua kuwa, siku hizi vijana wa kiume hata uwezo wa kujenga hoja ni kwa nini wakubaliwe na wanawake hawana. Kisa ni kwa kuwa wanawaza thamani yao inapimwa kwa muonekano wao ama pesa na vitu wanavyomiliki.

Pesa za kuendeshea maisha zinazotokana na akili ndiyo ndoano ya kunasa mwanamke na kudumu naye. Si mlimsikia K-lyn alivyokuwa anasifia akili za Mzee Mengi??

Wewe kila siku una "Mipango" inayotokana na matumaini ya kushinda Bet, unadhani mwanamke atakaa kwako asubirie ushinde Bet?
 
Ni kweli ila akili pekee bila pesa sio kweli
Neno "Pekee" umeliunda wewe . Ukiwa na pesa ama vitu bila akili utaachwa. Ukiwa na akili hata pesa kidogo ulizo nazo zitakuwa na thamani kwa mwanamke. Wakati wewe unadhani kila mwanamke anawaza hela, wanawake wenyewe huwaza kupata mwanaume mwenye akili za kuendeshea maisha.

Nilichoandika mimi ni hiki; Ukiwa hujui jinsi ya kutumia vizuri akili zako, mapenzi yatakushinda hata uwe na pesa ama vitu vya thamani vya dunia nzima.
 
Back
Top Bottom