Mapenzi ni kitu gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi ni kitu gani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Yona F. Maro, Sep 27, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nakuleteeni swali, wajuzi wa maarifa,
  Mlojaliwa akili, na bongo zisizokufa,
  Muwezao ona mbali, naombeni maarifa,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Mapenzi ni kitu gani, swali langu nauliza,
  Kwani yalianza lini, hadi leo yatatiza,
  Watu kuzama dimbwini, mbona yanawaumiza,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Ama kuna tofauti, na yale ya vitabuni,
  Yetu kizungumkuti, wengi wayalaani,
  Kwamba raha hawapati, tena humo mapenzini,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Niliyaanza zamani, nami pia nikapenda,
  Tena niliyaamini, nazo siku zikaenda,
  Pamoja nayo imani, mpenzi akanitenda,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Walisema kupotea, ndiko kuijua njia,
  Kidogo nikatulia, maumivu kupungua,
  Ni kweli niliumia, nikawaza mara mia,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Ikajatokea tena, mapenzini nikazama,
  Wengine sikuwaona, kwake moyo kutuwama,
  Nilimpenda kwa sana, sikujali wakisema,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Ikajatokea naye, kanifanya kuumia,
  Yule nimwaminiaye, ubaya kunifanyia,
  Nani sasa awezaye, swali akanijibia,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Huyu mwingine wa tatu, alinikata maini,
  Pengine hanao utu, kashindwa kunithamini,
  Kaona si malikitu, sipati jibu moyoni,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Kapasi kwenda chuoni, nikabaki mtaani,
  Hesabu zake kichwani, zikagoma abadani,
  Akaniona wa nini, basi kanipiga chini,
  Mapenzi ni kitu gani?
  Huyu kaenda Ulaya, akasema sasa basi,
  Kaniumiza vibaya, sitolipiza kisasi,
  Sikumfanyia baya, akaninyima nafasi,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Na huyu ile zawadi, kampa mtu mwingine,
  Akaivunja ahadi, kwa kuzaa na mwingine,
  Nadhani ni makusudi, sijiulizi jingine,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Nikaipata adhabu, mapenzi yakanitesa,
  Zingenipanda ghadhabu, dali wangu kumkosa,
  Sijapata bado jibu, ndani kuna nini hasa,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Wanasema yana raha, mi’ raha sijaipata,
  Wanasema ni furaha, machozi yangenifuta,
  Na kama siyo karaha, mbona mie nimesota,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Ya kutoka kwa mzazi, hakika nayaamini,
  Lakini ya kwa mpenzi, nimeona walakini,
  Nishafanyiwa ushenzi, nikazama majonzini,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Mapenzi ni raha gani, mbona wayasifia,
  Ama yamo nchi gani, watu wasikoumia,
  Hebu jifikirisheni, majibu kunipatia,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Nawauliza malenga, nami nitoke kizani,
  Haya watu wanalonga, kweli yapo duniani?
  Ama kunayo machanga, yaso na ladha kwa ndani?
  Mapenzi ni kitu gani?

  Kwani huwa vipivipi, hayo mapenzi ya kweli?
  Washayaonja wangapi, leo waseme ukweli,
  Tena siyo ya makapi, yaso na ubaradhuli,
  Mapenzi ni kitu gani?

  Semeni semeni jama, nahitaji kuelewa,
  Naogopa kuja zama, vile nilivyotokewa,
  Nifahamu kuyapima, nisipate kuchachawa,
  Mapenzi ni kitu gani?
  Swali nimewauliza.

  FADHILI M
   
 2. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Aha,Mapenzi...........!!!
   
 3. K

  KakaNanii JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2008
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  sijui ni kitu gani . Labda tumuulize amani misana wa 100.5 times fm
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Au brother chiko wa midnight magic
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Mapenzi ni "Emotional" Banking.

  Sasa wewe tafuta maana ya Kiswahili hilo neno Emotional, kisha tafsiri;

  'ukifungua akaunti benki, unapoweka na kutoa fedha, unajiskiaje?'.
   
Loading...