masuala ya ukabila ni stereo types haimaniishi
ni kweli asilimia 100
ni imani tu iliyojengeka......
wapo watu wastaarabu mno na wanatoka makabila yanaonekana yako ovyo
Sijakusoma vizuri ila naomba tu niseme kwamba Kama ingekua ni kweli walengwa wasingejali...na kwasababu sio kweli ndio maana inabidi ipingwe!!

Munabisha nini ukweli kuwa wanawake wa kichaga hawajui kupenda magogo na mungu hajawatia progamu ya kupenda ushauri wa bure bora uoe simba na ulale nae kuliko kuoa _fill the blanks_
Hivi kuna mtu yeyote anaeweza kujitosa hapa akasema na kuthibitisha kwamba kwenye UKOO wake wote hamna wezi..wadada wanaojiuza... wadada warahisi kupatikana...watu wakorofi...wavivu...wambea...wasiojua mapenzi..wanaojali/kupenda pesa (as if hao wapondaji wenyewe hawapendi) ...wahuni ...matapeli...wenye viburi...wenye dharau... wenye sura na mumbo unayoona wewe ni mabaya...wabahili...wachoyo...wanaopenda/oa/olewa kwa pesa n.k achilia mbali kwenye KABILA lake?!Kama wapo ningependa kuwajua ili na sie tusioisha kusemwa kila siku tujifunze toka kwao.
Ukweli na kwamba tabia ya mtu haitakiwi kuwa defined na wapi alipotoka (hata familia yake) bali na vile alivyo.Stereotypes hua zipo kwaajili ya wale waliotofauti na wanaokua stereotyped...kuwasaidia wale wa nje kuwalebel wenzao vibaya ili wao wajione/hisi kwamba ni bora hata kama sio kweli.Ndio maana hata wazungu (sio wote) bado wanatuona Waafrika kama wanyama..wanaamini hatuna akili japo wapo waaAfrika wenye akili kuliko wazungu wengi tu.Ila hili wazo linawafanya wao wajione wako juu.Kama ambavyo sisi wenyewe tunafanyiana kwanzia nchi na nchi..mkoa na mkoa...kabila na kabila..ukoo na ukoo na hata familia hii na ile.Kwenye swala zima la mapenzi naamini kabisa kwamba kabila haiplay role yoyote...kwahiyo achaneni na habari za sijui kabila hili hivi na lile lile.Kama unamjua mtu personally unaweza kumjudge yeye kwa vile unavyomjua na sio zaidi ya hapo.Pili....kama wewe hukupata experience nzuri na mtu wa sehemu fulani haina maana itakua hivyo hivyo kwa wengine wote.Ndio maana hata mwanamke /mwanaume unayemuona wewe kwamba hafai bado anakutana na mtu mwingine na anapendwa utadhani yeye ndio kila kitu.Kwahiyo waache wenzio nao wapate experience zao....kama wewe hukufanikiwa mwache mwingine nae ajaribu bahati yake.
Nasema yote haya maana hili swala la kuchambua makabila ya watu humu limezidi na linaboa kwakweli.Sijali kama ni langu au la mtu mwingine....ishu ni kwamba inachosha!!Mbaya zaidi ni kwamba yote mnayosema yanaweza kufanywa na yeyote hata anaetoka nchi nyingine achilia mbali wa kabila tofauti!
Alafu hivi hamchoki maana pamoja na sifa zote za ajabu ajabu mnazoyarushia haya makabila bado wadada wake wanaolewa SANA na wakaka wake wanaoa SANA ndani na nje ya makabila yao.Bado tu hamjagundua kwamba haisaiidii muachane nayo?!Maana kama ingekua inasaidia for the past few years usingesikia watu wa haya makabila wameoa wala kuolewa!
Mwisho...kama umempenda mtu na tabia yake inaendana na wewe upendavyo endelea nae...kama makabila ni muhimu sana tafuta wakwenu ili tabia zenu zifanane badala ya kuanza kuchambua ya wengine visivyo.Mapenzi kila mtu anaweza akayajua na kila mtu anaweza asiyajue...yote inategemea wawili wapendanao wanavyoyachukulia.

Aliyeanzisha hii thread akipitia posts zake za nyuma, atagundua kuwa hata yeye amewahi kuwa-stereotype wanaume ktk masuala ya mahusiano. Hii ndio kawaida ya binadamu, ubongo wetu uko programmed kuweka watu kwenye makundi. Tunajisikia vizuri tukiwatenga "wao" na "sisi". Hata hivyo, nakubaliana na hoja, ila tusiishie hapa tu kwenye makabila, twende mbele zaidi ktk aspects zingine za maisha. Hili la ku-stereotype makabila lina wa-potray kina dada vibaya na hawalipendi, lakini kila siku zikianzishwa thread za kuponda "tabia za wanaume", wanakuwa wa kwanza kunoa panga!

Munabisha nini ukweli kuwa wanawake wa kichaga hawajui kupenda magogo na mungu hajawatia progamu ya kupenda ushauri wa bure bora uoe simba na ulale nae kuliko kuoa _fill the blanks_

Mwembe wenye matunda ndo hurushiwa mawe!

Hizo mada za makabila haziwezi isha humu!

Tena mda sio mrefu utaona thread ya kabila humu
Duh ni mbaya ila halikwepeki kabisa, nahisi lingeanzia somo kwa wazazi wetu kwanza , maana wao ndio wanaotujaza hii kitu mu kichwa zetu