Mapenzi Matamu Lakini Yana Madhara Makubwa

Mapenzi Matamu Lakini Yana Madhara Makubwa

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
[TABLE="width: 491"]
<tbody>[TR]
[TD="colspan: 3"]Mapenzi Matamu Lakini Yana Madhara Makubwa[/TD]
[/TR]
[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
[TD]
6737398.jpg

Sanjay akiwa juu ya mti[/TD]
[TD]Mwanaume Moja nchini India ameamua kuishi juu ya mti kwa muda wa miezi 9, baada ya mke wake kukataa kuhama mjini na kuishi kijiji, kula kunywa na kulala juu ya mti[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi ni matamu sana pale panapokuwa na maelewano na maridhiano baina ya wapendanao lakini mapenzi hayo hayo huwa sawa na sumu kali inayodhuru pale mambo yanapokuwa kinyume, mfano halisi ni huko nchini India

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Sanjay (25), amefikia uwamuzi wa kuishi juu ya mti kwa muda wa kipindi cha miezi 9 baada ya kukataliwa na mke wake mwezi Machi kuishi kijijini.

Sanjay alikua anakaa kijijini na alimuacha mke wake kwa kipindi fulani katika mji wa Mumbai, na alipoamua kumfuata mke wake mjini Mumbai, ili waishi pamoja kijiji kwao, mke wake alikataa kufanya hivyo na kuendelea kuishi Mumbai.

Mwanaume huyo alishikwa na hasira na kuamua kupanda juu ya mti na kufanya ndiyo makazi yake, Sanjay amekuwa akiishi juu ya mti, anakula, kunywa na kulala juu ya Mti kwa kipindi kisichopungua miezi 9 sasa tangia mwezi Machi mwaka jana (2012) alipokataliwa na mke wake kuishi kijijini, "Kila mara tunapojaribu kumshusha anatishia kujiua anakula na kulala juu ya mti" alisema Mama Sanjay.

Sanjay aliwambia watu wanaomtaka ashuke juu ya mti, kwamba yeye hatoshuka chini hadi mke wake aje kumuomba msamaha.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3, align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[/TR]
</tbody>[/TABLE]
 

Attachments

  • Muhindi.jpg
    Muhindi.jpg
    10.2 KB · Views: 970
Hahaha. Inabidi kwenye vituo vya kupima hiv waweke na mpimaji wa akili aisee. Chizi fresh huyo!
 
mkuu "MziziMkavu"hivi haya ma 'nyuzi'na mapicha unayapatiaga wapi lol!
 
Jmaa amejikunja kama vule ndio alikua anapata mhemuko wa mwisho,mwisho
 
Back
Top Bottom