Vannele
JF-Expert Member
- May 4, 2013
- 287
- 90
Ni kisa ambacho sitakisahau kwani kimenifanya nijifunze kitu maishani mwangu...
Kulikuwa na dada mmoja (tumuite Latipha) alikuwa ametokea kumpenda mvulana mmoja ( tumuite Ismail) lakini hakuweza kumwambia kutokana na mila zetu za kiafrika zilivyo ingawa alijitahidi kuonyesha hisia zake kwa vitendo lakini kijana alijifanya haoni wala haelewi kinachoendelea...
Kumbe wakati huo Ismail alikuwa anapendana na msichana mmoja(tumuite Rey)
Basi siku moja katika pitapita ya Latipha akaona vurumai kwa mbali na kila mtu aliyekuwa karibu alikuwa anakimbia kunusuru roho yake...
Alipokaribia eneo la tukio akatahamaki kumuona Ismail akiwa anapambana na chizi aliyekuwa ameshika kisu kikubwa...na kadri muda ulivyokuwa unaenda Ismail alionekana kuelemewa na kuishiwa nguvu...
Cha ajabu hakuna aliyejitolea kumsaidia kila mtu alisimama mbali akiangalia akiwemo Rey...
Maskini Latipha... Kutokana na mapenzi makubwa aliyokuwa anayahisi hakuweza kushuhudia mtu anayempenda akiuawawa mbele ya macho yake, akajitosa mzima mzima kumsaidia Ismail...
Kumbe maskini bahati haikuwa upande wake, hakuwa na nguvu za kutosha kupambana na yule chizi, matokeo yake aliishia kujeruhiwa vibaya...
Mbaya zaidi alipokuwa anagala gala kwa maumivu hakupata msaada wowote wa haraka kutoka kwa watu waliokuwepo eneo la tukio hivyo alipoteza damu nyingi...
Akiwa kwenye hatua za mwisho za kupigania uhai wake alishuhudia Ismail akimkimbilia Rey na kumkumbatia bila ya kujali kwamba kuna mtu aliyejitolea uhai wake kumnusuru yeye...
Maskini Latipha hakuchukua muda mrefu akafariki dunia bila hata kusikia japo hata neno ahsante kutoka kwa Ismail...
Nilichojifunza mimi ni kumpenda anayenipenda, asiyenipenda nampotezea...
Wewe je, umejifunza nini kutokana na kisa hiki?