Mapenzi Haramu ya Kaka na Dada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi Haramu ya Kaka na Dada

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Jun 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280


  [​IMG]

  Mwanaume mmoja nchini Ireland amejikuta akimzalisha dada yake bila kutarajia baada ya kuangukia kwenye mapenzi bila kujua kuwa mwanamke huyo ni dada yake. Ameamua kufunga naye ndoa ili waweze kumtunza mtoto aliyezaa naye. Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Mark wa nchini Ireland alijikuta akizaa na dada yake wa baba mmoja mama tofauti, baada ya kuanza naye uhusiano bila kufahamu kuwa ni dada yake.

  Wazazi wa Mark waliachana wakati Mark akiwa mdogo sana ambapo kwa jinsi ndoa hiyo ilivyovunjika kwa mgogoro mkubwa mahakamani, Mark alipewa jina tofauti la baba na mahakama iliamuru mtoto huyo asiambiwe baba yake anaitwa nani.

  Kasheshe liliibuka baada ya Mark kukutana na mwanamke disco katika mji tofauti na anaoishi. Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Maura naye alienda kwenye disco hilo akitoka kwenye mji mwingine tofauti.

  Mark alianza uhusiano wa kimapenzi na Maura wakati huo. Miaka miwili baadae Maura alipopata ujauzito ndipo wawili hao walipoamua kuishi pamoja.

  Baada ya Maura kujifungua, Mark aliamua kumtambulisha Maura kwa mama yake na ndipo ukweli ulipofichuka.

  Mama yake Mark alimuuliza Maura baba yake anaitwa nani, alipolitaja jina lake ndipo mama huyo alipomwambia Mark "Mwanangu huyo ni dada yako".

  Matokeo ya vipimo vya DNA yaliyotolewa mwezi uliopita yalithibitisha kuwa Mark na Maura ni mtu na dada yake.

  Hata baada kugundua kuwa uhusiano wao ni haramu, wawili hao wameamua kuuendeleza na wamepanga kuzaa watoto wengi zaidi.

  "Najua watu watatufikiria vibaya, kama tusingekuwa na mtoto tungeweza kufikiria kusitisha uhusiano wetu lakini kwakuwa tuna mtoto mmoja, tutafunga ndoa tuzae watoto wengi zaidi", alisema Mark.

  Mark na Maura wanatoa lawama zao kwa mfumo wa sheria ambao ulizuia Mark kumjua baba yake.

  Wamepanga kumfungulia kesi ya fidia jaji aliyeamuru Mark asijulishwe baba yake.

  WAZUNGU KWA VITUKO HATUWAWEZI JAMANI KAZI KWELI IPO KWA WATU WEUPE.
   
 2. M

  Makanyagio Senior Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Imetulia hiyo. Damu kwa damu hakuna ugomvi ndai ya hiyo familia. Kuna mbaya gani hapo??
   
 3. d

  damn JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  good, I mean in red
   
 4. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni kwetu hawa jamaa wanalishwa nyama ya mbwa tena wanakaa juu ya paa la nyumba, wakishuka chini kila mmoja na lwake.
   
 5. senator

  senator JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hakuna ubaya wowote mana hawakuwa wakijua..ni sawa na muislam swafi akaenda kwenye sherehe bahati mbaya akakandamiza Mnyama haramu( Ze kitizzz) pasipo kujua then baadae akaja sifia aisee ile nyama ya sherehe ilikuwa nzuri sana..kumbe kala kitimotoz sidhan kama itamdhuru au kuharibu uislamu wake mana alikula pasipo jua..ni sawa na Mark alitenda pasipojua..hizi zipo sana huku kwetu uswazi vidingi vinamwaga makojo kila sehemu baadae mitoto inakuja kuwowana pasipokujua inatokea kwa baba mmoja!!
   
Loading...