Mapenzi halisi toka kwa mwanamke

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,712
58,377
images.jpeg

Zama za leo wanaume tumekuwa tukilalamika kukosekana kwa mapenzi halisi toka kwa wanawake! Ni dhahiri zama zimebadilika,ule upendo halisi umefifia Ila haujapotea!. Kilichopotea ni kile ambacho hakipo kabisa! na kilichofifia ni kile kipo Ila kwa uchache.

Hatuwezi kuzungumzia mapenzi bila kuiweka pesa! Ndio mapenzi bila pesa hayaendi kwani tafsiri ya pesa imebeba mahitaji yetu. Yenyewe ndio kinunuzi cha mahitaji yetu na huduma tuzitakazo. Mapenzi bila mahitaji ni sawa na mshumaa uulazimishe uwake pasipo na oksijeni!!.

Pesa imekuja kufubaza mapenzi halisi toka kwa viumbe hawa watamu.. kupenda imekuwa ni kwa kufuata mahitaji kuliko mapenzi, ndio wanahitaji kusurvive ndio maana wanafuata wanapoweza kusurvive!.

Mapenzi halisi ni kupenda sifa za mtu husika ama kimuonekano, kiutendaji n.k. Unaweza kuwa na kanuni zako za kutaka mtu kwa sifa uzitakazo lakini hisia zikaanguka kwa mtu mwenye sifa mbili tu kati ya kumi uzitakazo!.
Kupenda hakupangiwi, kupenda hakutajiwi.. kupenda kupo tu natural.

Kwa wepesi mada yangu inazungumzia kauli hii "Sometimes don't chase a woman they'll chase you"
Kuna vitu tunahitaji kuvifahamu kutoka kwa wanawake ili twende sambamba.. kwanza usije kujidanganya kuwa hakuna upendo halisi!.. kila binadamu anao upendo ila ni vile tu upendo huo unahitaji nini ili ukurupuke huko ulipojificha!..

Upendo halisi kwa hawa viumbe wanawake hauji tu bure!.. vipo vitu unavyotakiwa kuwanavyo ili uweze kulindimisha mawimbi ya upendo ndani ya viumbe hawa tuwapendao.

Ipo hivi wanawake hupenda mtu ambae anajali.. kiumbe hichi ni Kama mtoto,ujali huwa na maana kubwa ndani yao!.. wanaume tusikariri kuwa kutongoza ni lazima tutumie maneno au pesa.
Kutongoza na kupata upendo halisi kunatoka kwenye muonekano,matendo,ujali,uanamme wetu n.k

Viumbe vya kike hupenda kuwa comfortable hasa wakiwa na wawapendao hivyo ni juhudi yako kukifanya kiumbe hicho kuwa comfortable kwako.

Wanawake hupenda mtu mcheshi na serious.. mcheshi kwa maana ya kuwa na furaha awapo nawe na serious kwa maana ya mtu unae focus kwenye malengo na kuyatekeleza.

Mwanamke ni kiumbe kinachohitaji usiri wako na sio mpayukaji mtu usie na koromeo.

Ni dhahiri mwanamke anahitaji kiumbe kitanashati.. ipo hivi wanaume wengi tumekuwa hatujijali kimuonekano hii ni Kama asili yetu..😅

Ni vyema kujali muonekano Kama unahitaji hivi viumbe vikufuate!.. only smartness sio inatosha.

Wanawake wanapenda mtu simple na muelewa. Hizo ni sababu chache tu zinazoweza kuwafanya hao viumbe wapende kiuhalisia.. kwa tafsiri nyengine naweza sema ili we need to be gentleman ili tuweze kuibua mapenzi halisi toka kwa hao viumbe.

Guys let's be a gentleman na sio kila siku kuwa watu wa kulalama.
 
NILIFANYA VYOTE HIVYO NIKAISHIA KUBWAGWA... MAPENZI HAYANA FORMULA NA HAYASHAURIKI
Ulitakiwa uyafanye kabla kuingia kwenye Mapenzi na sio umetongoza huko ndo ukaanza no hivi huchanua Kama ua ili kumvuta nyuki kutua na sio nje na hapo..
 
Labda sampuli ya watu kama hao kwenye picha uliyoambatanisha ndio wanaweza kuendana na huu ujumbe.

Unajua kuna baadhi ya protocol hatuwezi ku-share na wenzetu hata iweje so tuwe makini sana kufanya mlinganyo kwenye hizi jumbe zakuhamasisha upendo kwasababu nyingi sio compatible na sisi waafrika hizo zinafanya kazi huko asia nk.

Huku demu ukimpata katika mazingira marahisi bila usumbufu anafunguliwa hadi uzi kua kaliwa kimasihara.

Hii inaonyesha kua hata jamaa hakutegemea kua ishu itakua nyepesi mno kiasi hicho.

Na kwa wengine kabisa akikutana na mwanamke katika mazingira hayo bila kusumbuliwa anajijengea fikra kua demu lazima atakua ni malaya

Ukimpata demu ambaye haombi hela ni aibu hata kuwaambia masela kwasababu aitomatically utaonekana tu kua unabebewa, fikra zetu ni lazima nyuma ya pazia kuna boya anagharamia

Na ukimpata mwenye anaomba pesa ikatokea kakuomba siku ambayo huna lazima utamind kua unachunwa shes after your money and she doesnt love you anymore
 
Smart..
 
Mimi ni conservative ambae anaamini kupo kukubali kutokubaliana ni Jambo la kawaida na, kukiwa na zuri, left, right, middle, far right, far left napokea.

Mimi dereva ukondakta kwenye mapenzi hapana, nikivaa ukonda ni kudonyoa kinafiki huyo nampigia salute Betina, maana alitusumbua wakati anasoma, sasa hivi kamaliza skuli, ana watoto, wajukuu na vitukuu wote visu na wakarimu, Betina wa gazetini sikuizi yupo live, Mbu salaleee!!
 
Mapenzi bila pesa ni Kama umepanda bus siti nzuri ila tairi vipara, muda wwte inaacha njia.
 
Thamani ya matendo yake inanifanya nimpende Zaid nae anipende Zaid juu ya matendo yangu

Tatizo changamoto kubwa watu weng tunakutana na watu tulio na matendo tofauti na mahtaji tofauti Sasa inafikia kipind mwanamke/mwanaume anaangalia pesa ili maisha yake yaende ila huko nje ana yule anaendana nae

Thamani ya matendo yake inanifanya nimpende Zaid nae anipende Zaid juu ya matendo yangu
 
Mapenzi bila pesa ni Kama umepanda bus siti nzuri ila tairi vipara, muda wwte inaacha njia.
Kuna watu mtapata tabu kujua nimeandika nini.. sijui nikisema gentleman sijui mnaelewa gentleman ni mtu tu au jinsia ya kiume tu bila kuwa na hela au vipi..

Mbona mnapata ugumu kuelewa hivi tatizo lipo wapi ndugu..
 
Back
Top Bottom