Mapendekezo ya nini cha kufanya Wizara ya Afya

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,749
Mapendekezo ya cha kufanya Wizara ya Afya

Niweke wazi tu kabla ya yote kuwa mimi kwa miaka zaidi ya 10 sasa nimekuwa nikifanya kazi kama consultant kwenye kampuni za Afya. Mwaka wa uchaguzi nitatumia muda kutoa mawazo yangu kwenye sehemu na wizara tofauti. Nianze na machache kwenye Afya

Mfumo:

1. Mfumo wa hospitali:
Tanzania kuna mfumo mchanganyiko wa Hospital. Kuna Hospitali za wilaya, binafsi na hizi kubwa kama Muhimbili, KCMC, na Bugando. Huu mfumo niseme tu ambao tunaufuata uliletwa na wakoloni. Wakoloni wetu wa EU walikuwa wametoka nchi ndogo hivyo kule kwao ni rahisi sana kuwa na hospitali moja kubwa ambayo ukiumwa unaweza kupiga simu mara moja au kuchukuwa gari na kukimbia hospitali.

Tanzania ni nchi kubwa na hatutaweza kuwa na hospitali kama muhimbili kila sehemu hivyo huu mfumo sio mzuri na hausaidii watu ambao wanakaa sehemu mbali sana na hizi hoapitali. Hopitali sio majengo pekee ni madaktari, vifaa, manesi, na huduma muhimu kama chakula .n.k

2. Watu: Watu ni muhimu kujua kwenye nchi zetu. Tunategemea sana ushauri wa wazungu kwenye Afya lakini Tanzania tuna watu tofauti. Afya inaendana sana na umri wa watu . Nchi yenye watu wazee mikakati haiwezekani ikafanana na chi ya vijana. Mfano umri wa kati wa USA ni 38.2 wakati umri kati wa Mtanzania ni miaka 17-18.

Ushauri unaotoa kwa mtu wa miaka 38 kwenye afya na kijana mdogo wa miaka 17 au 18 ni tofauti mfano ukiwa na umri wa miaka 38 unashauriwa upunguzi sukari mwilini au miaka michache ukaangalie tezi dume kitu ambacho ni tofauti sana na kijana mdogo. Hivyo zile sera mfano hapa wana list ya vitu ambavyo unatakiwa kufanya ukifanya ungalizi wako wa mwaka lakini ukiangalia vizuri hii list inatokana na ukweli kwamba umetengenezwa kutokana na ukweli kwamba umri wa kati ni huo miaka 38 hivyo serikali inasema ni lazima kampuni za bima kuhakikisha wanalipia vipimo Fulani kama kisukari.

Hivyo sera zinatokana na watu. Asilimia 64% ya watanzania kwa namba za mwaka 2018 ni miaka 24 na kwenda chini hivyo ni lazima tuje na sera ambazo zinalenga vijana wadogo. Nitaeleza mbeleni kwanini watu ni muhimu

3. Mtandao wa usambazaji: Lazima tuangalie mtandao wa usambazaji wa dawa na vifaa vya hospitali. Kwa Tanzania wana MSD (Medical Store Department). Hawa kazi yao ni kununua na kusambaza madawa. Hii ni step nzuri sana maana pamoja na mambo mengine wanaangalia ubora wa dawa lakini niseme tu ukweli hawana ubunifu wamekuwa nao wanafanya kazi kwa mazoea tu na kuomba pesa serikalini kila siku lakini hakuna ubunifu ambao wanakuja nao hivyo nitaeleza hapo mbele wafanye nini

4. Wahudumu: Tanzania kuna shule za madaktari na manesi. Lakini ni lazima tufikirie mbali zaidi ukiona nchi ambayo daktari analipwa sawa na karani wa benk ujue hiyo ni nchi masikini. Kuna daktari wawili Tanzania nimewapa vifaa vyangu mpaka leo tunadaiana daiana na sijarudisha pesa yangu niliyotumia kupeleka vile vifaa $23,000 na ni mwaka 2012!. Vifaa nilivyopeleka vilikuwana na gharama ya $90,000 kwa miaka ile lakini nimekubali kupata hasara

Lakini point yangu ni kwamba madaktari wetu bado wababaishaji sana na wengine wameweka utamaduni wa kuuza dawa badala ya kutoa matibabu kutokana na hali halisi mfano kiafya antibiotics hazitakiwi kutolewa bila kupimwa na kukutwa na bakteria sio hivyo tu unatakiwa uwe na homa maana mwili wako wakati mwingine unaweza kupigana na vidudu hivi lakini cha ajaabu antibiotic zinauzwa kiholela bila watu kujua ubaya wake ni u

Ukitumia nyingi kiholela dawa zinakuwa hazifanyi kazi vizuri maana mwili wako unakuwa na kinga kupita kiasi. Hivyo sitaongelea sana hili la wahudumu watu wengi wana lielewa lakini nitaongelea mengine
Tufanyaje

Mfumo wa hospitali na watu (1, 2)

1. Elimu: Kwasababu idadai kubwa ya watu ni vijana kuwe na jitihada za kutoa elimu ya afya maana ukiwa na vijana maana bado tuna muda mzuri wa kutoa elimu. Mazoezi na vyakula vya kula ni vitu muhimu sana kufundisha kwani haya mafunzo kwa vijana wadogo itabadilika na kuwa tabia. Magojwa yenye kuongeza gharama zana ni kisukari na pressure. Mara nyingi sio zote haya majogwa yanasababishwa na vyakula na hali za maisha. Hivyo tukitaka kupunguza gharama za magojwa mengine mengi ambayo yanaletwa na haya tuanze kutoa elimu.

2. Chanjo: Tuhakikishe kila mtoto anapata chanjo na tunaenda na wakati mfano siku hizi kuna chanjo za kifua kikuu na tetekuwanga

3. Usafi tufundishe usafi wa kunawa mikono na vyoo kupunguza magojwa ya kuambikiza

4. Tuhimize uangalizi wa afya kila mwaka angalau mara moja

5. Tunazishe mfumo wa mobile hospital: Yaani kuna magari ambayo yanakuwa ni hospitali kabisa. Sasa badala ya kuiga huu mfumo wa kujenga hospitali kila mahali ni vema tuwe nah ii system ambayo hospitali zinafuata watu hasa vijijini. Hivyo mnakuwa na kadaktari na manesi tofauti kwenye kila mobile hoapital halafu wanatembea kwa zone mfano kusini, kaskazini, kanda ya kati n.k. Wanatoa chanjo, kupima magojwa na kutoa elimu.

Hii itapunguza msomngamano wa wagojwa, inaongeza afya na kupunguza gharama kwa wananchi. Hakuna ambaye ata kosa/loose kwenye hili. Hii ni muhimu sana na kuna watakao uliza hii inafanyika wapi? Huta ona sehemu nyingi kwasababu wenyewe sio Tanzania nchi kubwa na watu wamesambaa lakini vifaa vipo na vinatumiakaga sana wakati wa vita.

Mtandao wa usambazaji 3

1. MSD ingetakiwa kuongea na Kenya, Rwanda na Uganda halafu wanunue dawa pamoja. Tofauti wa vitu vingine afya haichagui hivyo mtu yeyote anaweza kupata tatizo lolote bila kujali mipaka, rangi wala pesa. Hivyo basi hakuna sababu ya ubaguzi kwenye manunuzi. Wanatakiwa EAC wawe na kama MSD mbayo huku wanaita GPO (Group Purchasing Organization).

EAC wakienda kwenye kampuni za dawa na vifaa wakawaambia tutanunua $500M za dawa na vifaa wanaweza kupata punguzio kubwa sana la bei badala ya nchi mojamoja maana hizo kampuni zinzweza kutumia meli moja tu kutuma vitu nchi zote badala ya kutumia kidogo kidogo, kampuni zinapewa uhakika wa soko n.k. Lakini isitoshe kama mna soko kubwa mnaweza kutengenezewa dawa wakaweka nembo yenu ili dawa fake zijulikane.

2. Vifaa vya kimtaji/ capital equipments: Hivi ni vifaa kama CT, MRI na PET Scan. Hivi vifaa ni vya gharama sana na sio hositali zote zitaweza kununua. MSD au EAC ingeweza kununua vifaa hivi vya Mobile. Muhimbili wanahitaji pale lakini hivi vifaa vinauzwa vilevile ambavyo unaweza kuvitembeza mobile.

Sasa MSD ingeweza kuvipeleka sehemu mbalimbali mfano juma tatu hospitali Fulani, jumanne wanapeleka kwa nyingine na wanakuwa wanalipwa pesa ya kodi. Pesa hivyo inatumiaka kulipia gharama za uendeshaji na matengenezo ya mashine.

Sasa utaratibu wa kila hospitali kununua kifaa ni mgumu sana. PET Sscan mfano ya kiasasa ni $6M hii inatumiaka sana kusoma cancer sasa huwezi kununua Tanzania ikalipa kibiashara hata USA sio kila mahali ipo. Vilevile wataalamu huwezi kuwapata kila mahali na ndiyo maana nashauri vifaa MSD ndiyo wangekuwa wamiliki halafu waweke utaratibu wa mumodisha

Naomba wapelekeeni wahusika wa Afya haya mawazo
Zitto ,Mwigulu Nchemba
 
Eeenh, wewe ni 'consultant' wa mambo ya afya?

Sawa bwana!

Ukitaka tuchambue hii tutachambua. Sijaona mvuto popote.

Na usidhani Tanzania, au nchi yoyote ile wanajipigia tu bila utaratibu wa haya mambo. Wapo wataalam sana waliobobea katika maswala haya ya miundo ya utoaji huduma za afya. Wapo sana.
 
Nitaendelea kutoa dondoo polepole
Pascal Mayalla ,Zitto

Wizara nashauri ifanyieni kazi hasa MSD
 
Back
Top Bottom