Mapendekezo - Modulo ya hifadhi za jamii Igor mikopo Kwa watumishi

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,311
10,012
Wakuu salaam.

Nimeonelea nitumie ukurasa huu kutoa pendekezo ninaloona ni la manufaa sana kwa mustakabali wa taifa letu.

Imekuwa ni kawaida Kwa watumishi kuhangaika kutafuta mikopo kwenye mabenki Kwa riba kubwa sana na wakati mwingine watumishi wamekuwa wakipata mikopo inayowaumiza mitaani.

Wakati hali ikiwa hivi upande mwingine ni kuwa kuna mamilioni ya fedha za watumishi yapo mikononi mwa mifuko ya hifadhi za taifa Kama PSSF na mingine.

Mifuko hii imekuwa ikiyatumia mamilioni hayo katika uwekezaji wa Mambo ambayo wakati mwingine ni hasara tupu na mara kadhaa serikali hujichotea fedha kutoka mifuko hiyo na kushindwa kuzirejesha hali inayoathiri malipo ya pensheni Kwa wastaafu.

Badala ya fedha hizi kukaa na kupelekea kutumika katika uwekezaji usio faa au kuporwa na serikali ni bora ukawekwa utaratibu ufuatao:

Nimekaa na kuona zifanyike taratibu ili watumishi wachangiaji waweze kupatiwa fursa za kuchukua mikopo kutoka hifadhi hizi Kwa riba rafiki maana wao ndio wadau wakubwa wa mifuko hiyo hivyo inawezekana hata wakawa wanapata mikopo Kwa riba isiyozidi 10%.

Utoaji wa mikopo hiyo usiathiri taratibu za ukusanyaji na ulipaji wa pensheni za watumishi.

Likifanyika hili ninaamini kwamba tija ya uwepo wa mifuko hii itakuwa kubwa zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
 
Back
Top Bottom