Unaonaje katika Katiba mpya tuwe na Parliamentary system kwa Zanzibar and Tanganyika governments and Presidential system kwa Union Government? Kwa hiyo Mkuu wa Serikali ya Tanganyika awe Waziri Mkuu na atokane na chama chenye Wajumbe wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika, Mkuu wa Serikali ya Zanzibar awe Waziri Mkuu wa Zanzibar na atokane na chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mkuu wa Nchi awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la Muungano liwe ni kama upper house ambapo litakuwa na wajumbe sio zaidi ya 100 watakaochaguliwa na kila mkoa (kila mkoa wabunge 2 na idadi inayobakia wanatokana na uwiano wa kura). Mkuu wa shughuli za Serikali ya Muungano katika Bunge la Muungano anakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano.
Nadhani mfumo huu utahakikisha muungano wa Serikali 3 bila kuathiri muungano, utaongeza uwajibikaji kwani Serikali za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na Executive PMs na watawajibika moja kwa moja Bungeni, tutaepuka kuwa na marais 3 (Rais wa muungano, Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar). Migogoro yeyote itakayotokea kuhusu muungano itakuwa resolved na Baraza la Muungano ambao litakuwa na wawakilishi wa pande zote mbili. So Presidential system at Union level, Parliamentary system at States levels. Unaonaje pendekezo hilo
Mkubwa, na wewe pia unachemka.
Impeachment does not necessarily "imply that a crime has been committed by the President." Angalia articles of impeachment kwenye katiba uone ni vitu gani vitatu vinavyoweza kutumika kuleta mashitaka bungeni.

Ibara ya 46 ambayo ndiyo hasa inaeleza namna ya kuleta mashtaka dhidi ya rais is very theoretical! It is practically impossible kum-impeach rais kwa kufuata vifungu hivyo kwenye hali tunayoishi sasa.Impossible. Nadhani hiki ni kilelezo kingine kwa nini tunahitaji mjadala mpana kwenye hii katiba mpya maana ukisoma hiyo ibara ya 46 haingii akilini wabunge walipitishaje? Labda kwa sababu ilikuwa na enzi za 'zidumu fikra za mwenyekiti' hivyo hakukuwa na mjadala juu ya vipengele vya hii ibara. Mfano 46A (4) (a) kinahusu kuunda kamati maalum ya bunge kuchunguza madai dhidi ya rais. Kifungu kinasema hivi "Judge mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati".
Judge mkuu anateuliwa na rais, kwa mazingira yetu leo hii Judge Othman Chande anaweza kumchunguza Rais Kikwete? Hata kama katiba inasema hivyo lakini kwa mazingira tunayoishi sasa hili linawekezana kweli, na akatoa impartial results? Kwa kifupi katiba tuliyonayo inapwaya sana!
Hahahahahahahahhaaaa ha ha hahaaaaaa.........Nilivyosema "crime" sikuwa na maana ya "crimes" unazozifikiria. I meant a "crime" for the purpose of ....
Pasco,
Nimekusoma mara nyingi lakini naomba niseme kitu kimoja. Sometimes, huwa unapotosha sana kwa ku-cite a wrong law. Kama hapa unajaribu kupotosha kuwa kwenye Katiba kuna ibara inayowezesha Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais. That is not true. Kama hiyo ibara ipo, tuwekee hapa tafadhali. Bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lakini sio Rais. Insted, Bunge linaweza kupitisha tuu azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais.
Nafikiri utakuwa ni mmoja wa wale wachache ambao mnashindwa kutofautisha kati ya vote of no confidence na impeachment. The two phrases mean different things. Impeachment implies that a crime has been committed by the President whilst a vote of no confidence does not imply that the person under vote has committed a crime.
Kwa hiyo BAK yuko right kabisa kutaka kuwepo kwa kipengele cha kutokuwa na imani na Rais kwenye Katiba mpya kwa sababu hakuna kipengele kama hicho kwenye Katiba ya sasa.
- Katiba ni ya taifa sio ya CCM, infact kwenye hili la katiba mpya CCM lazima ile bullet kwa the good of the Nation at large!
Unaonaje katika Katiba mpya tuwe na Parliamentary system kwa Zanzibar and Tanganyika governments and Presidential system kwa Union Government? Kwa hiyo Mkuu wa Serikali ya Tanganyika awe Waziri Mkuu na atokane na chama chenye Wajumbe wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika, Mkuu wa Serikali ya Zanzibar awe Waziri Mkuu wa Zanzibar na atokane na chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mkuu wa Nchi awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la Muungano liwe ni kama upper house ambapo litakuwa na wajumbe sio zaidi ya 100 watakaochaguliwa na kila mkoa (kila mkoa wabunge 2 na idadi inayobakia wanatokana na uwiano wa kura). Mkuu wa shughuli za Serikali ya Muungano katika Bunge la Muungano anakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano.
Nadhani mfumo huu utahakikisha muungano wa Serikali 3 bila kuathiri muungano, utaongeza uwajibikaji kwani Serikali za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na Executive PMs na watawajibika moja kwa moja Bungeni, tutaepuka kuwa na marais 3 (Rais wa muungano, Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar). Migogoro yeyote itakayotokea kuhusu muungano itakuwa resolved na Baraza la Muungano ambao litakuwa na wawakilishi wa pande zote mbili.
So Presidential system at Union level, Parliamentary system at States levels. Unaonaje pendekezo hilo
Mfumo anaoupendekeza Mh. Zitto, at least at Parliamentary level unafaa, suala kubwa ni namna ya kumuaccomodate President. Siungi mkono hoja ya kuwa na wajumbe 100, ambapo kila mkoa utatoa wajumbe 2. This again is the misuse of our resources, which we can not afford. Mfumo wowote tunaoutaka lazima uzingatie jambo moja muhimu kuwa sisi ni nchi masikini!
Mh Zitto ..mfumo uliopendekeza ni mzuri...lakini muhimu hapo ni tujuwe atakayekuwa na mamlaka juu ya vyombo vyote vya dola.....kwa kifupi amiri jeshi mkuu awe ni rais wa muungano...
Pia hapa Zanzibar itabidi wabadili tena katiba Yao iendane na katiba ya muungano.....of which naona Kama Zanzibar factor ni ngumu ...kwa kifupi wao ndio Wenye veto kwenye huu mchakato....na sidhani kama tunawatendea haki watanganyika kwenye hili....
Umeongelea kuwa waziri mkuu atokane na chama cheenye wabunge wengi kwenye lower house....?.....Kuna uwezekano hapa wa waziri mkuu na rais kuwa vyama tofauti ....na rais atakuwa na dola....hapa panaweza kuwa na tatizo...wakitofautiana.....
Jambo lingine la jumla ambalo ningependa tujadili ....mnaonaje tuwe na serikali za majimbo au mikoa zenye nguvu zaidi na kuwajibika kwa wananchi .......kuleta maendeleo badala ya mfumo wa sasa wa wakuu wa mikoa au wilaya ambao ni Kama viranja tu wa kisiasa na wengi wao hasa wa mikoa ya pembezoni wanashinda Dar kila siku.....hawana uchungu kabisa na wananchi.....
Tukiimarisha local gorverment inaweza beba jukumu hili......yaani chama chenye wabunge wengi wilayani ...Kitatoa meya ambao yeye na wao ndio watakaoendesha serikali ya wilaya kwa ujumla....watendaji wataendelea kutoka serikali kuu kwa dhana ya umoja wa kitaifa.....
Nafasi ya meya (wamkoa) au Gavana Itatokana na chama chenye overal majority ya madiwani kwenye mkoa .....
Sioni tija peyote sasa ambako kuna watendaji wa halmashauri na wilayani ....it is dupilication of posts.....serikali inaweza kupunguza nusu ya watendaji wake kwa mfumo huuu na kazi zitaenda haraka zaidi....watakaopunguzwa watasaidia kusukuma sekta binafsi...sio lazima kila mtu aajiriwe na serikali.......tunahitaji waondoke ,ili tupate nafasi za Kuajiri walimu zaidi....,polisi etc...
- Wakati umefika wa kupunguza msururu wa Viongozi wa juu, na hasa gharama za kuwatunza waki-retire, I mean people naomba kuuliza hivi kweli tunawahitaji Waziri Mkuu na Makamu wa Rais katika Serikali yetu? kwa maoni yangu one has to go kwenye katiba mpya na hasa Makamu wa Rais, kama ni muhimu kuwa naye basi Waziri Mkuu ashike hiyo nafasi kama zamani.
- The idea kwamba hata Visiwani kunakuwa na Makamu wa Rais, tena wawili it does not make a sense at all, wanafanya nini? Hivi vinakuwa ni vyeo vya huruma tu, under whose expense? kodi yetu wananchi wakati ni sasa kwenye katiba mpya kuondokana na na huu msururu wa Viongozi wa juu, tuwe na huruma kwa Walalahoi kidogo jamani!
MUCH RESPECT PEOPLEs!
William @..NYC, USA: Mutuz Le Baharia!
Mimi si Mwanasiasa, na si mtu wa kupigia debe haya mambo ya siasa za Kiafrika... Lakini kuna mambo ambayo uwa nayaona kama si lazima sana yawepo na haswa kwenye safu ya uongozi wa nchi.
Haya mambo ya kuwa na Wabunge wa viti maalum , Wabunge kuwa Mawaziri, Wakuu wa mikoa kuchaguliwa n a Rais... Mikoa kuwa na Meya hapo hapo kuna Mkuu wa Mkoa... Yote haya ni maswala ambayo yanapaswa kuangaliwa upya.
Kwa sababu mtu akigombea ubunge kisha anachaguliwa tena kuwa Waziri, kunapunguza uwakilishi wake Bungeni. Na kama wabunge kubaki kuwa wabunge kutaondoa tamaa ya Wabunge kujipendekeza kwa serikali ili wachaguliwe kuwa mawaziri....
Kuhusiana na muda au vipindi vingapi kwa maoni yangu mimi as long as wananchi wanakupenda na uwezo wa kuwakilisha na kutatua matatizo ya wananchi unayo basi endelea kugombea... Hii ni kwa ngazi ya ubunge... Na wanapaswa kuwa na ofisi kwenye majimbo yao au hata ofisi ndogo uko vijijini, na iwe lazima mbunge kutembelea jimbo lake na vitongoji mwake kila mwaka, na hakishindwa basi hawajibishwe na atumie pesa au posho anazolipwa uko bungeni (yaani kusiwe na pesa za ziada kutoka serikalini wala asiombe kwa wananchi, labda wananchi wapende wenyewe kumchangia au chama chake kifanye utaratibu wa kumpatia)
Vilevile kwenye Ukuu wa Mikoa ingependeza zaidi kama hawa wakuu wa mikoa nao wakagombea au kupigiwa kura kama wanavyo pigiwa kura wabunge.... Hii kutawalazimisha kuwajibika kwa raiya zao... Au hao wabunge wa Mkoa au jimbo ndio wanapaswa kugombea nafasi ya Ukuu wa mkoa, hapa ina maanisha kuwa Wabunge wakishirikiana na mkuu wao wa mkoa (ambaye naye ni mbunge) wanakaa katika baraza ambalo wao pamoja na viongozi wachache wa kiraiya, wakiwemo wakuu wa wilaya na raiya waliochaguliwa kuingia kwenye kamati ya kujadiri matatizo ya wananchi, ndio wataamua nini kipelekwe uko bungeni na ikiwezekana miswaada ya bunge inapitia ngazi hii kwanza na kupata maamuzi wa kila mkoa na kisha ndio uko bungeni kunapelekwa mapendekezo au maamuzi ya kimkoa, kwa sababu wananchi washa shirikishwa na uwamuzi ushatolewa.
Kama haiwezekani basi iwepo serikali ya majimbo, ambayo itakuwa na uwajibikaji mkubwa wa majimbo...
Mfano:
Dar Es Salaam, Pwani na Morogoro, linaweza kuwa ni jimbo Moja.
Kagera, Kigoma, na Mara,
Singida, Dodoma na Iringa
Rukwa, Mbeya
Ruvuma, Mtwara na Lindi
Kilimanjaro, Manyara na Tanga
Zanzibar
Pemba
Au ikachaguliwa mikoa yenye kupakana na yenye ukaribu zaidi.
Mawazo mazuri sana mkuu wangu isipokuwa tu ktk mfumo huo rais atachaguliwa vipi? kutokana na 1. Popular vote; 2.Mwenye wajumbe wengi ktk Bunge la Muungano (Upper house) au 3.Matokeo ya chaguzi za majimbo ktk states mbili (Tanganyika/ Zanzibar) .Unaonaje katika Katiba mpya tuwe na Parliamentary system kwa Zanzibar and Tanganyika governments and Presidential system kwa Union Government? Kwa hiyo Mkuu wa Serikali ya Tanganyika awe Waziri Mkuu na atokane na chama chenye Wajumbe wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika, Mkuu wa Serikali ya Zanzibar awe Waziri Mkuu wa Zanzibar na atokane na chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.