Mapendekezo katiba mpya: Tunahitaji makamu wa rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapendekezo katiba mpya: Tunahitaji makamu wa rais?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Nov 26, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Wakati umefika wa kupunguza msururu wa Viongozi wa juu, na hasa gharama za kuwatunza waki-retire, I mean people naomba kuuliza hivi kweli tunawahitaji Waziri Mkuu na Makamu wa Rais katika Serikali yetu? kwa maoni yangu one has to go kwenye katiba mpya na hasa Makamu wa Rais, kama ni muhimu kuwa naye basi Waziri Mkuu ashike hiyo nafasi kama zamani.

  - The idea kwamba hata Visiwani kunakuwa na Makamu wa Rais, tena wawili it does not make a sense at all, wanafanya nini? Hivi vinakuwa ni vyeo vya huruma tu, under whose expense? kodi yetu wananchi wakati ni sasa kwenye katiba mpya kuondokana na na huu msururu wa Viongozi wa juu, tuwe na huruma kwa Walalahoi kidogo jamani!

  MUCH RESPECT PEOPLEs!

  William @..NYC, USA: Mutuz Le Baharia!
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu@ NYC, Mutuz
  Nafikiri suala hili tuliache kwa kamati kuu ya CCM, wao ndiyo wataamua katiba mpya ya CCM iweje kulingana na masilahi yao wao ya kugawana vyeo, sisi hapa tutakuwa tunatwanga maji tu na kupoteza muda kujadili mambo yasiyotuhusu na wala yasiyokuwa na faida kwetu zaidi ya CCM na wanachama wake wanaotarajia kuwania nafasi za ulaji.
   
 3. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  UMENENA VEMA; SI HAO TU; NAFIKIRI KUNA POSTS ZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA PIA SIONI KAMA WANA MAJUKUMU SANA HAPA NCHINI TOFAUTI NA KUFANYA KAZI ZA CHAMA. FIKIRIA KWENYE MIKOA NA WILAYA TUNA WAKUU WA POLISI HALAFU BADO TUNAAMBIWA PIA KWAMBA HAWA WAKUU NDIYO WENYEVITI WA USALAMA WKT WALIOVISOMEA WAPO. PIA UNASHINDWA KUDRAW LINE KWENYE KAZI ZA WAKURUGENZI WA WILAYA NA MIKOA NA WATU HAWA. PIA KWENYE MKOA NA WILAYA BADO KUNA MAKATIBU TAWALA, MAKAIMU WAKUU WA MIKOA,N.K. Ni hakika tuna Rundo kubwa sana ya Viongozi ambao wengine hawana cha maana wanachofanya.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Idadi ya wizara na namba ya mawaziri vitajwe ndani ya katiba.
   
 5. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280

  - Mkuu wangu mbona tena una underestimate nguvu ya JF, umesahau kamati ya Mkama kuhusu kupungua kura za Rais mwaka 2010, I mean sisi huwa ni kuwapa na kuwaachia waamue kusuka au kunyoa, halafu kuwahamasisha wananchi kwenye kupiga kura, kumbuka Wabunge wote wapya wa Chadema wametokea hapa JF!

  - Katiba ni ya taifa sio ya CCM, infact kwenye hili la katiba mpya CCM lazima ile bullet kwa the good of the Nation at large!


  William @....NYC, USA: Mutuz Le Baharia!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Mkuu William, nakuunga mkono sana kwenye hili la not to underestimate powers za jf. Kuna kubwa jingine litatokea Alhamisi asubuhi, ambapo tutamshauri mode aandae kukwaa la maoni ya wana jf kwenye katiba mpya. Tutampatia mwakilishi wetu kwenye tume ya kukusanys maoni (lazima atakuwepo) na kuyawasilisha!.
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Uwepo wa makamu wa Rais linajikita katika suala la Muungano. Tulipomuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamo tuliongeza tatizo,kero za muungano. Hili sijui ulilifikiria pia?

  Tutakapoondoa makamo wa rais wa Muungano, tutabakisha nini hapo?

  Nilivyofahamu wazo lako ni kuwa tuue/tuvunje muungano. Je nimekufahamu sahihi?

  Hili la CCM ile bullet limekaa vizuri. Je Mzee wetu bado ana ushawishi wowote kule CCM ili awaelimishe CCM wenzake kuwa sasa ni wakati wa CCM kutoka katika uccm katika hili la KATIBA MPYA na ilitizame hili la KATIBA MPYA kwa the good of the nation kama ulivyong'amua.

  I wish other Malecelas, Mwinyis and Mnauyes wapate ujasiri wa kuleta katiba Mpya ya Taifa na sio katiba ya CCM kwa Taifa. Hongera mkuu.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Umuhimu wa makamu wa Rais huonekana Rais anapokufa ghafla...
  kuna kuwa hakuna 'struggle for power' kwa sababu automatically makamu
  anakuwa Rais.....sasa ukisema Waziri mkuu peke yake unaweza kuleta
  'mvutano' kati yake yeye na Spika wa bunge' ikitokea Rais kafa ghafla....
  waliofuatilia 'mgogoro wa Ivory Coast ulivyoanza watakumbuka hili'

  mimi ningeshauri tungekuwa na 'Naibu Rais' kama South Africa.....lakini asiwe
  mtu wa upande wa pili wa muungano kama ilivyo sasa...
  awe mtu mwenye kumsaidia Rais tu moja kwa moja.....
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu kamanda wa zamani swali hapa utapata majbu tena ya maana ila nina wasi wasi sana na watu kama Anna Kilango na matusi yao bila kujali hata kanunu za Bunge .Mawazo yetu kwa sasa sijui kama ni msaada kwa mwendo ule wa kuwatukana wenzao kwa nguvu .
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Rais wa Zanzibar automatically awe Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri, na Waziri Mkuu awe Makamu wa Pili automatically, kuvunja Muungano hapana lakini Wananchi wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni kuamua kama wanataka Muuungano au hawataki, lakini waelezwe kwanza faida na hasara za kuwepo na kutokuwepo kwa Muungano bila vitisho, ninaamini kwamba wananchi wakielemishwa on that watachagua kuwepo kwa Muungano, hiyo ndio itakuwa nafasi pekee ya kuuimarisha Muungano kisheria, so far tunajifanyia mambo tu kisiasa!

  - Infact Muungano umegeuzwa kama tool ya kutafutia Madaraka ya katika Serikali ya Jamhuri ya Muuungano, zipo case nyingi sana on that ambapo Wajumbe wa Visiwani wametumiwa sana katika kuamua nani awe nani kwenye Serikali ya Muungano, that is wrong na tunahitaji kulisema hili tena wazi kwenye Katiba mpya!

  William @..NYC, USA: Mutuz Le Baharia!
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  Tunaweza kusema kuwa Rais wa Zanzibar awe makamu wa pili wa Rais kama zamani
  na tukawa na makamu wa Rais wa kwanza ambae sio lazima atoke Zanzibar....
  lakini hapo lazima nafasi ya waziri mkuu ifutwe.....makamu wa kwanza awe ndie msaidizi mkuu wa Rais....
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  Napingana na wewe kwa hili...
  Rais wa Zanzibar asiwe makamu wa kwanza automatically...awe wa pili..
  why? kwa sababu makamu wa kwanza ndie atakuwa Rais iwapo Rais anakufa ghafla
  na WAZANZIBARI wapiga kura wako wangapi mpaka Wachague 'The President in waiting'????
   
 13. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  Mkuu The Boss,

  - I have a problem na kuwa na Kiongozi wa Juu wa Taifa kwa maneno ya Muungano tu, lazima iwe more than that to the Nation!, ingawa you have a point!

  William @..NYC, USA: Mutuz Le Baharia!
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280

  - Ndugu yangu Lunyungu, heshima yako sana bro, wachana na siasa za majina ndio zimelifikisha taifa letu hapa tulipio, tufike mahali tuangalie taifa kwanza na kuamini kwamba hawa wanasiasa ni watu wa kupita tu, ila taifa lipo haliendi kokote!

  - By the way sina tena mawasiliano yako ya sasa, nipitishie mkuu wangu kwenye inbox tuongee siku nyingi sana bro, MUCH RESPECT!

  William @..NYC,USA: Mutuz Le Baharia!
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Si suala la ku-undermine JF ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Kama CCM itaweza kuleta katiba bora zaidi kwa watanzania ambayo itaweka masilahi ya watanzania mbele na kurudisha nguvu ya utawala kwa wananchi. Yaani kuwepo na mazingira ya wananchi kuwa waamuzi wa mwisho bila maamuzi yao kuingiliwa au kucheleweshwa kwa hila zozote, nitaamini kabisa kuwa CCM ni chama chenye kuweka mbele masilahi ya Taia na hivyo sitakuwa na sababu ya kuwanyima kura yangu for the good of the country.

  Ila ujasiri huo hawana na hili limejionesha mapema katika hatua muhimu ya kuelekea mchakato mzima. CCM inaweza cheza karata zake vizuri japo sidhani kama wana ujasiri huo endapo gamba tu limewashinda kulikoboa sasa wanataka lipaka rangi lionekane kivingine.
   
 16. T

  Taso JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Hizo faida za Muungano ni nini?
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  soi tu kutajwa,bali Rais asiruhusiwe kutangaza watu na kuwaapisha bila
  watu hao majina yao kujadiliwa na kupitishwa bungeni kwa kupigiwa kura...
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Mkuu @ New york, mapendekezo yako ni mazuri ila mara nyingi nikiona Taifa kubwa kama Marekani linakuwa na makamu wa Rais basi hiyo nafasi ina umuhimu wake isipokuwa tu hapa kwetu hii ndio imekuwa maalum kwa ajili ya kuwafariji Wazanzibar kutokana na mfumo wa siasa uchwara.
  Sasa basi mimi pendekezo langu kwenye katiba mpya ni kufuta kabisa cheo cha ukuu wa wilaya, hawa ni kundi la majobless ambao hawana tija kwa Taifa.
  Mkurugenzi wa almashauri anatosha kabisa kuwajibika kwa ajili ya wilaya yake huku akiwa na makatibu tawala wa wilaya na mawaziri sio lazima wawe wabunge, maana kama una wabunge wa category ya Livingstone Lusinde sijui hilo baraza utaliundaje, maana ni afadhali uwe na mawaziri kama kina Joti wa ze comedy wanaweza kuwa na maana zaidi.
   
 19. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tuangalie kazi za Makamu wa rais ambaye ndiye msaidizi mkuu wa rais kuhusu masuala yote ya Jamhuri ya Muungano.* Hususan anamsaidia Rais katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku za Muungano, kutekeleza kazi zozote atakazoagizwa na rais pamoja na kuchukua madaraka ya Urais wakati Rais mhusika hayupo madarakani au akiwa amesafiri kwenda nje ya nchi.
  Kazi za Waziri Mkuu ni kuongoza na ni mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, na amepewa mamlaka ya kudhibiti na kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  Sasa tuangalie, je mtu mmoja akivishwa kofia zote hizi, ataweza kutekeleza kazi zake ipasavyo?
  Kwa issue ya zanzibar kuwa na makamu wawili wa raisi, nafikiri wote tunaelewa kuwa ule ulikuwa ni usanii.By then, tusilaumu, tufuahie na tuzipongeze pande zote mbili zilifanya kazi ya ziada kufikia muafaka!
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  wakurugenzi wa halmashauri unawadhibiti vipi kwa wizi na ubadhirifu?
  maana waliopo sasa karibu wote ni majambazi wakubwa..
   
Loading...