Mapendekezo katiba mpya: Tunahitaji makamu wa rais?

Katiba mpya ni lazima iyakinishe vyeo vya watendaji wakuu wa serikali, suala la awepo makamu wa raisi ama la, litemegemee umuhimu wa kiutendaji, katiba ni lazima iweke majukumu kamili ya kiutendaji, kwa sasa yupo yupo tu kama kumwakilisha raisi kwenye mambo ya kiitifaki hana mamlaka kamili kiutendaji kiserikali hata kama yapo hayaonekani kwa madaraka aliyonayo sasa sidhani kama anaweza hata kumfukuza kazi mkurugenzi wa wilaya. Hii nafasi ina umuhimu wake sana kumsaidia raisi kiutendaji tatatizo lilipo ni kuwa raisi wetu si rahisi kukubali kupunguza madaraka yake, labda katiba iweke wazi kama makamu wa raisi ni lazima atoke Zanzibar, hivi sasa tuna mgongano wa katiba zetu iweje raisi wa Zanzibar awe waziri kwenye muungano? Je mkubwa kimadaraka ni nani; ni lazima siasa za kiccm tuweke pembeni na tuangalie maslahi ya Taifa, suala la mgombea mwenza atoke wapi viachiwe vyama vyenyewe viamue, ili kuboresha muungano wazinzibar wapewe nafasi ya kuujadili kama wanautaka au la; inaonekana tunawalazimisha wameshasema Zanzibar haitachangia gharama za katiba mpya; hiyo itakuwa ni jukumu la serikali ya muungano; sasa kama sio kujichanganya wao ni kitu gani? je wao hawamo kwenye muungano tunaoungelea?

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Rais ni mfumo,

kwahiyo watu wengi wanaangalia kwa macho dhahifu kuona kazi za makamo wa rais, kwakuwa wanaangalia kwa macho na fikra pana awaoni nafasi ya makamo wa rais ina umuhimu gani katika taifa letu.

Kwanza napenda kusema namchukia makamo wa rais lakini sichukii cheo cha makamo wa rais, kwani kikitumiwa vizuri ni moja vya taasisi za urais katika ushauri wa mambo mazito ya nchi, pia kutokana na yeye kutoingilia mambo mengi ya kiutendaji ya kila siku anajiweka katika nafasi nzuri ya kubobea katika tafiti na kuibua mambo mengi ya kuweza kumshauri rais yaingie katika mfumo wa utekelezaji pia ni mtu anayeweza kupima mwendo wa serikali kwani yeye ni mtendaji nusu asiyelimbikiziwa kazi nyingi.


Makamu wa rais kutojaziwa kazi nyingi za kufanya zinamuwezesha kuwa na muda wa kutafiti mambo mbali mbali na kufuatilia maagizo ya rais kwa watendaji wadogo, wengi wa watanzania tumekariri kuwa kazi ya mtu ni lazima kuwe na mlundikano wa mafaili katika meza ya mtu ndio tusema ana kazi ya kufanya.

 
- Wakati umefika wa kupunguza msururu wa Viongozi wa juu, na hasa gharama za kuwatunza waki-retire, I mean people naomba kuuliza hivi kweli tunawahitaji Waziri Mkuu na Makamu wa Rais katika Serikali yetu? kwa maoni yangu one has to go kwenye katiba mpya na hasa Makamu wa Rais, kama ni muhimu kuwa naye basi Waziri Mkuu ashike hiyo nafasi kama zamani.

- The idea kwamba hata Visiwani kunakuwa na Makamu wa Rais, tena wawili it does not make a sense at all, wanafanya nini? Hivi vinakuwa ni vyeo vya huruma tu, under whose expense? kodi yetu wananchi wakati ni sasa kwenye katiba mpya kuondokana na na huu msururu wa Viongozi wa juu, tuwe na huruma kwa Walalahoi kidogo jamani!

MUCH RESPECT PEOPLEs!

William @..NYC, USA: Mutuz Le Baharia!


Umenena vyema. Mimi kwa mtazamo wangu naona kama nchi hatuwahitaji wote wawili yaani makamu wa rais na waziri mkuu. Tuna rais mtendaji ana ndiye mkuu wa serikali. Waziri mkuu yupoyupo tu hana lolote analoweza kuamua bila rais kukubali. Ndio maana hata Lowassa amewashinda hoja wanaompinga kwenye vikao vya juu vya CCM kwa sababu kimsingi maamuzi yote kuhusu Richmond yalibarikiwa na baraza la Mawaziri likiongozwa na rais. Uhusiano wa Rais na waziri mkuu ni sawa na uhusiano wa mwalimu na kiranja wa darasa ambaye kimsingi hana anachoweza kuwafanya wanafunzi wenzake zaidi ya kuwashitaki kwa mwalimu.

Makamu wa raisi ni cheo ambacho sijawahi kuona manufaa yake tangu kilipoanzishwa. Siko zote huwa najiuliza hivi huyu jamaa job description yake ni ipi? je kila siku anapoenda ofisini anafanya nini ndani ya masaa nane anayokuwa ofisini? Labda wajuzi watakuja kutuelimisha.
 
Mkuu @ New york, mapendekezo yako ni mazuri ila mara nyingi nikiona Taifa kubwa kama Marekani linakuwa na makamu wa Rais basi hiyo nafasi ina umuhimu wake isipokuwa tu hapa kwetu hii ndio imekuwa maalum kwa ajili ya kuwafariji Wazanzibar kutokana na mfumo wa siasa uchwara.
Sasa basi mimi pendekezo langu kwenye katiba mpya ni kufuta kabisa cheo cha ukuu wa wilaya, hawa ni kundi la majobless ambao hawana tija kwa Taifa.
Mkurugenzi wa almashauri anatosha kabisa kuwajibika kwa ajili ya wilaya yake huku akiwa na makatibu tawala wa wilaya na mawaziri sio lazima wawe wabunge, maana kama una wabunge wa category ya Livingstone Lusinde sijui hilo baraza utaliundaje, maana ni afadhali uwe na mawaziri kama kina Joti wa ze comedy wanaweza kuwa na maana zaidi.


kaka nimeipenda hiyo ya kwenye red huyu jamaa ukimsikiliza unatamani hata kuvunja tv jinsi alivyo empty head hivi anakaaga anatafakari anachokizungumza? wenje alimwambie fulsa ya kusoma tulipewa wote mimi niilitumia vizuri mwenzangu hukuitumia lilikuwa ni tusi ambalo kwa watu tuliendea shule tulilielewa ila yeye maskini wa mungu hakupata kitu. eti ndio mtu anatunga sheria bungeni lol WILLIAM MALECELA what do u expect tutapata katiba nzuri kutoka kwenye kichwa kama hiki? viti maalum je wanaopiga makofi tu bungeni? look at vijana kama John mnyika, wenje, halima mdee!!
 
Tuandike katiba kwa kuzingatia kuwa sisi ni nchi masikini?... Tanzania ni nchi tajiri yenye watu masikini....
Nchi ni watu. Kumbe ni miti? Huwezi kusema Tanzania ni tajiri kama watu wa Tanzania ni masikini.

Ni muhimu tuunde katiba inayotambua kwamba sisi ni masikini. Itakayotutoa kwenye umasikini, sio tu jedwali zuri la mgawanyo wa "uwajibikaji" au madaraka. Hizo ni siasa. Tunapoteza muda mwingi kufikiria siasa, wakati kipaumbele chetu cha kwanza kinatakiwa kiwe kuondoa umasikini. Huwezi kutatua tatizo la umasikini kama unakataa ukweli kuwa, kwa kuanzia, wewe ni masikini.

Nchi masikini haiwezi kumudu mawaziri wakuu kibao, makamu wa marais kibao, maserikali kibao na mabunge kibao na wawakilishi kibao. Hatuwezi kufuta umaskini kama hatutumii mali zetu finyu kichumi.

Na kwa kuanzia, tungepunguza mzigo wa Zanzibar.
 
Mawazo mazuri sana mkuu wangu isipokuwa tu ktk mfumo huo rais atachaguliwa vipi? kutokana na 1. Popular vote; 2.Mwenye wajumbe wengi ktk Bunge la Muungano (Upper house) au 3.Matokeo ya chaguzi za majimbo ktk states mbili (Tanganyika/ Zanzibar) .

- Yapi majukumu ya rais tukisha kuwa na mfumo kama huu. Maadam kila state itakuwa na waziri mkuu wake, hawa watakuwa na madaraka juu ya uthibiti, usimamiaji na utekelezaji wa kila siku kazi na shughuli za states hizo ni nani atachukua nafasi ya waziri mkuu ktk serikali ya Muungano.

Samahani nimefanya editing baada ya kuona umependekeza makamu wa rais kuchukua nafasi ya waziri mkuu bunge la Muungano..

Mkuu huoni kaa huyu rais atakuwa - ceremonial President maanake sioni kazi ilobakia ikiwa kila state itajitawala na bunge la muungano kuna makamu wa rais, yeye rais atakuwa na madaraka gani haswa?
Mi nadhani ni mfumo au utaratibu kama ule unaotumika Marekani ya Kaskazini U.S.A
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye anakuwa Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, mkuu wa nchi. Kila Waziri Mkuu atateua Baraza lake la Mawaziri bila kuingiliwa na Rais. Rais wa muungano atateua Mawaziri kwa Wizara za Muungano tu - Nje, Ulinzi, Ndani, Union Treasury.

Ni kweli Rais na Mawaziri wakuu wataweza kutoka vyama tofauti. Huu ndio mfumo uliopo hata sasa kwamba WM anatoka chama chenye wabunge wengi na sio lazima kiwe chama anachotoka Rais.

Zitto hapo umenichanganya. Kama Rais atateuwa Mawaziri wa Nje, Ulinzi, Ndani na Union Treasury, ina maana watakuwa accountable kwa Rais, na Mawaziri Wakuu wa pande zote mbili can't question them. Hao mawazi walioteuliwa na rais, wataingia vipi kwenye cabinet ya bara na visiwani?
 
Muungano ufe kabisa. Hakuna faida yoyote ya muungano zaidi ya raia wa pande zote mbili kulalamika wanapunjwa rasilimali zao pamoja na kuongeza gharama za uendeshaji nchi kwa kuwa na lundo la viongozi wa muungano kwa gharama ya walipa kodi ambao wengi wetu ni watu wa kipato cha chini. Vyama vyote vya upinzani vinataka serikali tatu. Serikali ya tatu ifanye kazi gani wakati kila nchi itakuwa na serikali yake yenye mamlaka kamili kama si kufuja hela za walipakodi wachovu? Nini kitakachofanya kwamba raia wa pande hizi mbili wasilalamike kwamba upande mmoja una viongozi wengi kwenye serikali ya muungano kuliko mwingine? Kazi gani zitakazofanywa na serikali ya muungano bila kuingiliana na kazi za serikali husika za nchi?
Huu ni wakati mgumu kwa uchumi wetu kutokana na misukosuko ya dunia ya kiuchumi. Hatuna budi kufanya maamuzi yenye maslahi ya kiuchumi kuliko kun'gan'gania mfumo ambao hauna tija kwa mataifa yetu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom