Mapendekezo Hospitali ya Taifa Muhimbili

Maleven

JF-Expert Member
Sep 8, 2019
624
2,772
1. Sehemu wanayokaa watu kusubiri kuingia ndani kuangalia wagonjwa hasa saa sita na saa kumi ningependekeza pajengwe/pawekwe mabenchi ya kukalia pamoja na banda, mfano wa lile duka la vinjwaji kule ndani karibu na mortuary (wanaopajua watanielewa) ili kusaidia wale ndugu zetu hasa kipindi cha mvua, jua kali, kuchafuka kwa nguo pia kuwa comfortable.

2. Sehemu wanayokaa/lala wale wenye kuuguza wagonjwa usiku pawekwe vifaa vya umeme kuua mbu (outdoor electrical mosquito repeller) kuwasaidia na kuwaokoa na adha ya mbu. nimesema hivi kwa kuwa fumigation yaweza kuwa disturbance.

Ahsanteni.
 
Mara ya kwanza kufika Muhimbili nilikataa hii ndo hospitali ya Taifa.

Bora ukatibiwe private tu.
 
pia waondoe mabadiko ukutani yanayowaita wagonjwa 'wateja'... unakuta wodini bango limeandikwa 'haki za mteja' au 'wajibu wa mteja', nani mteja? unadhani mimi napenda kulazwa hapo mpaka uniite 'mteja'? pumbavu kabisa!
 
Mimi mwenyewe mara ya kwanza kutoka pale nilijiuliza mara mbili mbili ndio hapa muhimbili au nimekosea.....
Mara ya kwanza kufika Muhimbili nilikataa hii ndo hospitali ya Taifa.

Bora ukatibiwe private tu.
 
Muhimbili haiko pale kwa ajili ya wanyonge. Kama unauguza mgonjwa unatakiwa ukalale hotelini.
Hatuna budget ya kujenga mabanda ya kusubiria pale. Waambie madiwani wa CHADEMA wakujengee.
Eti msiumwe na mbu. Hao mbu wakale wapi? Kwani huko Kigogo, Isevya, Wangilonga, Ibinzamata , Pasua na Kijenge mnakokaa kuna hivyo vifaa vya mbu?? Usituletee za kuleta hapa.
 
1. Sehemu wanayokaa watu kusubiri kuingia ndani kuangalia wagonjwa hasa saa sita na saa kumi ningependekeza pajengwe/pawekwe mabenchi ya kukalia pamoja na banda, mfano wa lile duka la vinjwaji kule ndani karibu na mortuary (wanaopajua watanielewa) ili kusaidia wale ndugu zetu hasa kipindi cha mvua, jua kali, kuchafuka kwa nguo pia kuwa comfortable.

2. Sehemu wanayokaa/lala wale wenye kuuguza wagonjwa usiku pawekwe vifaa vya umeme kuua mbu (outdoor electrical mosquito repeller) kuwasaidia na kuwaokoa na adha ya mbu. nimesema hivi kwa kuwa fumigation yaweza kuwa disturbance.

Ahsanteni.
 
Attachments

  • twitter_20191110_104727.mp4
    1.4 MB
Back
Top Bottom