tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Nimerudi tena Hospitali ya Taifa ya Muhimbnili baada ya kwenda mara ya mwisho mwaka 2010 ni takribani miaka 8 sasa toka nikajage pale kwa mara mwisho.
Hakika kuna mabadiliko makubwa sana kwa kila nyanja ukianza na taratibu mbalimbali zilizozowekwa hapo hospitali.
USAFI: Suala la usafi ni la hali ya juu sana ukilinganisha na miaka 8 iliyopita ukianza na nje usafi ni safi sana zile sehemu zote za bustani ni safi sana huwezi kuona vitu vimetupwa ovyo ovyo kama hapo awali maua na majani yamekatwa vizuri na wafanya usafi wakiwa na mavazi yao rasmi ya usafi na vitendea kazi bora kabisa.
Ukiingia ndani ya wodi za wagonjwa na ofisi za madaktari na wauguzi ni safi sana, kiukweli usafi ni wa hali ya juu sana mashuka meupe sakafu kavu na safi hakuna vumbi kuta zimepakwa rangi safi hakuna madao wala rangi rangi za ajabu ajabu hakuna harufu kabisa kama ilivyokuwa zamani na hata watumishi wenyewe wanang'aa kwa mavazi yao.
HUDUMA: Kuhusu huduma kwakweli kuna mabadiliko makubwa sana hasa katika kutoa huduma moja kwa moja kwa mgonjwa...Madaktari na Wauguzi na wataalam wengine kila muda na dakika mawazo yao yako kwa mgonjwa tu na si kwa ndugu au jamaa za mgonjwa kama ilivyokuwa zamani.Mgonjwa anapata huduma zote bila ndugu au jamaa wa mgonjwa kusumbuliwa kabisa kwa maana kila dawa inayotakiwa pale kwakweli asilimia 98 mgonjwa anapata tofauti kabisa na zamani ukiingia tu kumuona mgonjwa aidha asubuhi mchana na ile jioni lazima Muuguzi akuite na kukupa kakaratasi kwa kwenda duka la dawa au famasi kununua dawa au vifaa vinavyohitajika kwa mgonjwa.Na pia round za wodini za kuwaona wagonjwa kwa madaktari na wauguzi zimeongezwa tofauti na zamani na imesaidia hata kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika.
MAADILI: Kuna maadili ya hali juu sana kwa wato huduma kwani zile lugha za zamani kwa mgonjwa au hata ndugu wa mgonjwa siku hizi hatuzisikii kabisa mgonjwa anahudumiwa kwa upendo wa hali ya juu sana na kupewa taarifa zote sahihi anazopaswa kupewa wakati akipata huduma kama vile kuhusu dawa,vipimo au hata operation kama inahitajika.Nawapa hongera sana wato huduma kwa kutenda kulingana na viapo vyao.
MALIPO: Kuhusu malipo hapo ni changamoto kwa baadhi ya wagonjwa hasa wale ambao hawana BIMA kwani kila baada ya muda fulani mgonjwa anapritiwa bill yake ili ndugu wajue kuhusu malipo na kuanza kupunguza kidogo kidogo na wapo ambao hushindwa kupata malipo yote hivyo wengine wamekuwa wanapata msamaha wa kupunguziwa kutoka kwa Maafisa wa Ustawi wa jamii kwa vigezo ambavyo wanaona vifaa kwa mgonjwa huyo kupata punguzo la bill yake.Lakini bado wengi wanajitahidi sana kulipa na kuondoka na mgonjwa baada ya kuruhusiwa.
UTAWALA: Utawala wa sasa wa hospitali umepangilia mambo mengi sana kwa taratibu nzuri mfano kuhusu usafi naona kuna kampuni ya usafi wa ndani na nje kuhusu ulinzi kila kona kuna ulinzi na kuelekeza wageni wa wagonjwa kufuata utaratibu,hakuna ndugu kupiga kambi ovyo nvyo ndani ya hospitali bila sababu zozote zile hakuna watu wanaozagazaga tu katika mazingira ya hospitali.
PARKING ZA MAGARI:Utawala umetenganisha parking za magari kwa watumishi na ndugu wa wagonjwa hivyo kupunguza wizi wa magari au vifaa vya magari kwa watumishi.
MAONI :Kwanza hongereni sana watoa huduma kwa kazi ngumu inayofanywa kwa wagonjwa kwani ni huduma za viwango vya juu sana pia ushauri kwa wananchi wajitahidi kujiunga na huduma za BIMA kwani zinasaidia pale unapokuwa huna pesa na unahitaji huduma ya afya.Tatu ni muhimu sana kwa ndugu wa wagonjwa kufuata tartibu zilizowekwa na utawala wa hospitali ili huduma ziwe katika viwango vya kimataifa kwa maana kufuata muda wa kumuona mgonjwa ili kutoingiliana na muda wa kutoa huduma.