Yafahamu magonjwa 20 ya mlipuko mabaya zaidi katika historia ya dunia

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,668
13,237
Awali ya yote napenda kutoa pole nyingi kwa Watz walioathirika na hili gonjwa kwa namna moja ama nyingine huku wakiendelea kupambana na Ugonjwa wa Corona kila mtu kwa staili yake tukiwa tumepoteza mwelekeo hasa baada ya wataalamu na wanasiasa nchini kutofautiana katika mbinu za kukabiliana na janga hili. Mungu aendelee kutunusuru na kadhia hii. AMINA.

Leo nawaletea orodha ya magonja ya mlipuko yaliyowahi kutikisa eneo Fulani la dunia ama dunia nzima (yaani Epidemics and Pandemics). Nyakati za nyuma inaonesha mababu zetu walishambuliwa mara kwa mara na ugonjwa wa Tauni. Hii ni kukumbushana na kutiana moyo kua haya tunayopitia yamewahi kuikumba dunia huko nyuma kwa hiyo Corona sio ugonjwa wa kwanza hatari wa mlipuko.

1. Prehistoric epidemic: Circa 3000 B.C
Huu ni ugonjwa hatari wa TAUNI uliotokea huko Kaskazini Mashariki mwa China na kuangamiza kijiji kizima cha Prehistoric. Inasemekana ugonjwa ulikuja ghafla yaani kwa haraka sana kiasi kwamba haikuwezekana hata kufanya taraibu nzuri za mazishi kwa waliofariki, wengi wao wakizikwa katika makaburi ya pamoja.

2. Plague of Athens: 430 B.C
Huu ni ugonjwa mwingine wa Tauni uliolipuka huko Athens Ugiriki na kutesa kwa miaka 5 ukiua zaidi ya watu 100,000. Watu wenye afya zao walishambuliwa na joto kali la ghafla, macho kuwasha sana, na kujaa na kutoka damu kwenye koromeo na mdomoni,

3. Antonine Plague: A.D. 165-180
Hii ni Tauni nyingine iliyojitokeza na kujizolea umaarufu wa kuua watu wengi wakati wanajeshi waliporejea kwenye Himaya ya Rumi wakitoka vitani. Inasemekana hili gonjwa liliua zaidi ya watu milioni 5.

4. Plague of Cyprian: A.D. 250-271
Tauni ya wakati huu ilitikisa kiasi cha kuwaibua viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini. Hapa ndipo Askofu huyu Cyprian wa Tunisia (Hatimaye jina lake kupewa ugonjwa) aliuelezea ugonjwa wa Tauni kama dalili za wazi za MWISHO WA DUNIA. Inaaminika uliua watu 5,000 kila siku kwa mji wa Roma pekee.

5. Plague of Justinian: A.D. 541-542
Hii Tauni ilipewa jina la Justinian Mtawala wa Himaya ya Byzantine. Hili lilikua ni eneo mashariki mwa Roman Empire ambayo ni maeneo ya Instanbul ya sasa. Inakadiriwa kua 10% ya watu duniani kote walikufa wakati huo.

6. The Black Death: 1346-1353
Ugonjwa huu uliosababishwa na bacteria na ulisambaa kutoka bara la Asia mpaka Ulaya. Inasemekana uliua 60% ya watu wote Ulaya yaani iliua takribani watu milioni 65 Ulaya nzima ndani ya muda huo wa miaka 7.

7. Cocoliztli epidemic: 1545-1548
Huu ni ugonjwa uambao dalili zake zilikua homa kali, homa ya matumbo na kutokwa damu. Hii ilitokea huko Mexico na Amerika ya kati ikiua watu zaidi ya milioni 15.

8. American Plagues: 16th century
Ni Tauni inayosemekana ililetwa na Wapelelezi kutoka Ulaya. Inakadiriwa kua 90% ya Wamarekani asili upande wa magharibi walipoteza maisha.

9. Great Plague of London: 1665-1666
Baada ya Black Death ikaja tauni nyingine iliyoshambulia England. Vijidudu vya Ugonjwa huu inasemekana vilibebwa na panya huku takataka na uchafu hasa maeneo ya watu masikini ikiwa ndio chanzo kikuu cha kusambaa kwa ugonjwa. Mji wa Landon ukiwa ndio kitovu cha maambukizi walikufa watu wengi sana na kupelekea wale wenye uwezo km Madaktari, Wanasheria, Wafanyabiashara akiwemo Mfalme Charles waliikimbia London wakiwaacha watu masikini. Huu ugonjwa uliua 15% ya watu wa London huku jumla kuu ya vifo ikiwa watu 100,000. (Hii ya kukimbia London imenifanya nimkumbuke MEKO).

10. Great Plague of Marseille: 1720-1723
Kumbukumbu za kihistoria zinaonesha kua ugonjwa huu ulijitokeza pale meri iliyokuwa ikiitwa Grand-Saint-Antoine ilipotua pwani ya mji wa Marseille Ufaransa ikiwa imebeba shehena ya mizigo kutoka mashariki mwa Mediterania. Kwa haraka kabisa Tauni ikasambaa kwa kasi ya ajabu na nadni ya miaka 3 ikawa imeuma watu takribani 100,000 huku mji wa Marseille pekee ukirekodi 30% ya raia wa mji huo walikua wamefariki.

11. Russian plague: 1770-1772
Hii Tauni ilishika moto kwa kasi zaidi katika mji wa Moscow baada ya watu waliowekwa karantini kuanzisha vurugu na kukimbilia nje. Hii ikapelekea hadi kuuwawa kwa Askofu mkuu Ambosius ambaye alikuwa akishawishi watu kutokukusanyika kwa ajili ya sala. Mpaka ugonjwa unakoma ulikua umeua takribani watu 150,000.

12. Philadelphia yellow fever epidemic: 1793
Wakati homa ya manjano ikiwa imeisha pale Philadelphia Marekani, viongozi walifikia hatua ya kudhani kua watumwa hasa weusi walikua na kinga imara dhidi ya magonjwa. Kutokana na Imani hiyo wakawaita watu wenye asili ya Afrika ili kufanya kazi ya kuuguza wagonjwa. Hii ilikua kama kuwasha moto wa petroli. Ugonjwa huu uliokuwa unasambazwa na mbu ukalipuka kwa kasi sana na kuua watu 5,000.

13. Flu pandemic: 1889-1890
Visa vya awali kabisa vya haya mafua viligundulika Russia. Ugonjwa ukasambaa kuanzia St Petersburg kabla ya kusambaa kwa haraka kuelekea Ulaya na dunia nzima. Hii ni pamoja na ukweli kwamba usafiri wa anga ulikua haupo kipindi hicho. Ndani ya miezi michache tu ukawa umepiga dunia nzima na ilichukua wiki 5 tu kufikia kilele cha maambukizi ukiua watu milioni 1 dunia nzima.

14. American polio epidemic: 1916
Ugonjwa wa Polio uligundulika katika jiji la New York City ukisababisha watu 27,000 kuugua huku vifo vikiwa 6,000 ndani ya U.S. Huu ni ugonjwa ambao wahanga wakuu ni watoto. Polio iliendelea kuwatesa Wamarekani mpaka chanjo ilipopatikana mnamo mwaka 1954.

15. Spanish Flu: 1918-1920
Inasemekana huu ni moja kati ya milipuko ya magonjwa mibaya zaidi kuwahi kuikumba dunia ambapo inakadiriwa kuwa watu milioni 500 waliathirika kuanzia Bahari ya kusini mpaka kizio cha kaskazini huku ikikadiriwa kua 1/5 ya watu walioathirika walipoteza maisha.

16. Asian Flu: 1957-1958
Hii Flu ilikua ni aina nyingine ya ugonjwa hatari ukiiathiri dunia. Ulioanzia huko Asia hususani nchini China ambapo zaidi ya watu milioni 1.1 waliuawa na ugonjwa huu huku vifo 116,000 vikitokea Marekani pekee.

17. AIDS pandemic and epidemic: 1981-present day
Tangu UKIMWI ulipogundulika kwa mara ya kwanza unakadiriwa kua umeshaua zaidi ya watu milioni 35 mpaka sasa. Inaaminika kwamba ugonjwa huu ulitengenezwa kutoka kwa nyani na kupandikizwa kwa binadamu huko Afrika Magharibi mnamo mwaka 1920. Kwa sasa 64% ya watu milioni 40 ambao wanaishi na virusi vya ukimwi wanatokea kusini mwa jangwa la Sahara.

18. H1N1 Swine Flu pandemic: 2009-2010
Hii flu ya 2009 ilisababishwa na H1N1 (H na N ni aina mbili za protini zinazounda kirusi kinachoshambulia cell za mwili) ambayo iligundulika huko Mexico kabla ya kusambaa sehemu nyingine za dunia. Ndani ya mwaka mmoja ilikua imeathiri jumla ya watu milioni 1.4 duniani huku ikiua watu takribani 500,000 kwa mujibu wa CDC.

19. West African Ebola epidemic: 2014-2016
Ebola ilipiga Afrika kwa mara ya kwanza kati ya 2014 na 2016, ambapo watu 29,000 waliathirika huku 12,000 kati ya hao wakipoteza maisha. Kisa cha kwanza kabisa kiligundulika Guinea mnamo Desemba 2013, baadae ugonjwa ukasambaa kwa kasi na kiwango kikubwa kabisa kuelekea Liberia na Sierra Leone. Kiasi kikubwa cha maambukizi kilitokea katika hizo nchi tatu huku nchi zingine chache zikiwa na visa vichache vya maambukizi na vifo. Inasemekana asili ya virusi hivi ni kutoka kwa POPO.

20. Zika Virus epidemic: 2015-present day
Madhara ya mlipuko wa Zika huko Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini bado hayajajulikana bayana mpaka sasa. Virusi vya Zika vinasambazwa na Mbu ambao wanapenda Zaidi hali ya hewa na joto na unyevunyevu mwingi na hivyo kuifanya Amerika Kusini, Kati na sehemu ya Kusini mwa Marekani kua kitovu cha maradhi haya.

JE, KUNA CHA KUJIFUNZA KATIKA HIZTORIA HII? NIAMBIE UMEJIFUNZA NINI.

Imeandaliwa na Jile79, Kwa msaada wa mtandao.

Note: Babu yangu angekuwa hai ningemshirikisha na kumhoji ili kupata angalau picha waliishije wakati wa majanga haya makubwa.
 
6. The Black Death: 1346-1353

Mkuu huu kwanini uliitwa kwamajina Haya Msaada Kama Unauelewa Wasababu zake zakuitwa hv.....

Sent using My COVID-19
 
6. The Black Death: 1346-1353

Mkuu huu kwanini uliitwa kwamajina Haya Msaada Kama Unauelewa Wasababu zake zakuitwa hv.....

Sent using My COVID-19
OK. Hii ni kwa sababu ilikua Bacteria wakiingia kwenye ngozi walikua wanatengeneza manundu yalivovimba na kubadirika kuwa meusi
 
The Black Death: 1346-1353

Ugonjwa huu uliosababishwa na bacteria na ulisambaa kutoka bara la Asia mpaka Ulaya. Inasemekana uliua 60% ya watu wote Ulaya yaani iliua takribani watu milioni 65 Ulaya nzima ndani ya muda huo wa miaka 7.
Huu inasemeka uliua karibu nusu ya watu duniani kipindi hicho watu takr mil200
 
Hapo kwenye Nr. 1. "Kaskazini Mashariki mwa China na kuangamiza kijiji kizima cha Prehistoric", pana hitaji kusahishwa kidogo. Prehistoric inamaanisha "kabla ya historia" na sio jina la Kijiji. Otherwise asante kwa tujuza mengi kuhusu milipuko.
 
Uko sahihi kwa kiasi fulani hasa kuhusu translation ya neno/jina Prehistoric ila kumbuka hapakua na jina la hilo eneo wkt huo ndio maana wakaita tu prehistoric village ambao in the modern China panaitwa Hamin Mangha jina lililokuja kutungwa baadae
 
Asante mkuu, lakini ingefaa zaidi kama ungesema "kijiji cha kale huko China"!

Halafu mkuu, listi yako mbona haijataja smallpox, ambayo Wikipedia inasema:
"Smallpox is estimated to have killed up to 300 million people in the 20th century[15][16] and around 500 million people in the last 100 years of its existence.[17] As recently as 1967, 15 million cases occurred a year.".

Kwa sasa tumshukuru Mungu imekomeshwa kabisa, (imekuwa eradicated)
 
Uko sahihi ingeleta maana zaidi kuandika "Kijiji cha kale huko China" Thanks
Ni kweli kabisa hapo hujaona smallpox wkt ni moja kati ya magonjwa 10 hatari ya kuambukiza kuwahi kutokea duniani. Kuna mwingiliano kidogo wa hivi virus na utoaji wa majina ya virusi husika mfano kabla ya kuitwa smallpox uliitwa Great Pox. Majina mengine ya ugonjwa wa smallpox ni km pox, speckled monster, and red plague. Kwa hiyo kwenye andiko langu ugonjwa wa hapo juu Antonine Plague na American Plagues yalikuwa related na smallpox....
 
Bwana Bossi!!! Hii smallpox ni ya juzi juzi tu na Antonine Plague ulisema ni ya A.D. 165-180 na American Plague ni ya 16th Century!.
Bado nakupongeza kwa kutuletea hoja fikirishi na kutufanya tuwe wajambuzi ili tuelimike zaidi!
Big up, kwako mkuu!! Asante.
 
Ahsante! Nadnai labda kun akity hujaelewa,,,Fuatilia vizuri kaka smallpox ilikuwepo tangu zamani sana na imekua ikipewa majina kulingana na ni wkt gani ilitokea ama jina gani litafaa zaidi. Kwa taarifa yako watu wa kwanza kuanza kufanyavaccination na smallpox ni China mnamo 1,500 na hapo iliishakuwepo kitambo sana kabla ya kuanza kufanyika hayo majaribio ya kinga.......
Unasemaje ya juzijuzi tena...

Anyway ahsante kwa kuendelea kufuatilia zaidi
 
Bwana Bossi!!! Hii smallpox ni ya juzi juzi tu na Antonine Plague ulisema ni ya A.D. 165-180 na American Plague ni ya 16th Century!.
Bado nakupongeza kwa kutuletea hoja fikirishi na kutufanya tuwe wajambuzi ili tuelimike zaidi!
Big up, kwako mkuu!! Asante.

Sijui unafuatiliaje mkuu jaribu kufanya ufuatiliaji kwa utulivu na ufasaha utaelewa vizuri hii iko bayana kabisa:

The origin of smallpox is unknown.[13] The earliest evidence of the disease dates to the 3rd century BCE in Egyptian mummies
 
Back
Top Bottom