Wataje tuwafahamu walalamishi? kuna tofauti ya kudai kuna kero za muungano na kulalamikaHakika yashangaza !
Naona kuna moja hapa kana katabia hapa ka katoto kachanga kama alivyowahi kusema Mwalimu - ukikapata kanakunyea, ukikaacha kanalia. Nafikiri kuna janja ya nyani hapa - walalamishi wanajua sana faida za Muungano, wanauhitaji ati. Wakati Zenji wanahitaji Muungano, Bara ni muungano unawahitaji.
- Wale ambao hawaishi kulalamika kuhusu Muungano ndio hao hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga kuvunjika kwake !
- Wale ambao hawaoni faida ya Muungano hawalalamiki lakini wapo mstari wa mbele kuunga mkono kuvunjika kwake !
Muungano hauwezi kuendelea kwa lazima, kwani haziungani ardhi bali watu.Muungano njomba haufi ,hilo nakuhakikishia ila Chama Cha Mashetani ndio kitakufa na kipo njiani ,haiwezekani vyama vyote vione umuhimu wa Muungano isipokuwa Chama Cha Makamati.
Na yeyote yule utakaemsikia kuwa bora muungano ufe huyo atakuwa ana agenda ya siri na ni mmoja katika wafuasi wa Chama Cha Sultani CCM pengine anaona ukifa serikali iliyotokuwepo itaendelea na kuzidi kuwazuga Watanganyika kwa mikakati ya baada ya miaka mia.
Ujasiri wa Maalim Seif wa kwenda hadharani na kuwapa taarifa nzito wanachama na wapenzi wa CUF, juu ya kumtambua Rais Karume ilibidi upongezwe na Taasisi zote kuu na watanzania wote kwa jumla. Katika mazingira yeyote yaliyopo, bila ya kujua hatima ya safari hiyo ndefu, lakini hiyo ilikuwa ni hatua moja kuelekea katika kupunguza mvutano wa kisiasa kati ya CUF na CCM Zanzibar.
Kwa mshangao mkubwa ni zaidi ya mwezi sasa hivi toka tukio hilo litokee, lakini si Pengo, Kilaini, Askofu Shayo au viongozi wa KKKT waliodiriki kutoa pongezi zao kwa tukio hilo. Baraka za viongozi hawa ni muhimu sana, hasa ukizingatia kuwa huko nyuma katika matukio tofauti walijitokeza ni kutoa maoni yao. Kwa mfano wakati wa machafuko ya Mwembechai, Pengo alisikika katika Radio Tumaini akiipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua katika kudumisha amani. Nilitarajia katika tukio hili kubwa la kihistoria la kumtambua Rais Karume vile vile kuwa Pengo angetoa pongezi.
Lakini hasa nini maana ya ukimya huo? Hili ni swali ambalo nafikiri kila mtanzania anajiuliza. Sihitaji kuja na mawazo yangu kwa hili, lakini ingekuwa vyema kama viongozi hawa wenyewe wangetjitokeza hadharani na kueleza sababu za ukimya wao. Aidha ningewaomba wanJF wenye upeo mkubwa wakuwaelewa viongozi hawa pamoja na wale waliobahatika kujiwa na Roho Mtakatifu watueleze sababu ya ukimya wao.
Amani ya Zanzibar ni Amani ya Tanzania nzima, hivyo si siri kuwa mapatano ya CUF na CCM Zanzibar ni ushindi kwa watanzania wote. Na hatua iliyochukuliwa na Rais Karume na Maalim Seif ni kwa faida na maslahi ya Tanzania nzima. Tuwaombee waendelee vizuri.
Amani ya Zanzibar ni Amani ya Tanzania nzima, hivyo si siri kuwa mapatano ya CUF na CCM Zanzibar ni ushindi kwa watanzania wote. Na hatua iliyochukuliwa na Rais Karume na Maalim Seif ni kwa faida na maslahi ya Tanzania nzima. Tuwaombee waendelee vizuri.
Jamani,
Mwungano hauhitaji marekebisho. Mwenyezi Mungu kisha take care. Mmesikia global warming? Zanzibar itazama baharini kwa muda usiotimia miaka 50 ijayo. Hawa tunawakaribisha bara bila visa. Na mafuta yatakuwa yetu sote.
sI UONGO, ni vyema atutake radhi.JAS-WISSU tutake radhi,,chonde chonde tutake radhi ndugu yetu kabla hatujakusomea HALBADIRI....Zanzibar haitoweki milele,,WELA mafuta hatugawani,,,yetu wenynnnnyewe,,hata kama nusu kifuniko tutajipaka mwilini tung'ae
zawadi: Cuf - ccm ni vyama vya siasa.
Machafuko ya mwembechai yalikuwa ni mambo ya dini.
Elezea connection iliyopo hapa, cuf - ccm, pengo na mwembechai; au tayari ndiyo huo utafiti wako!
I can't see logic here!
Hili la mpaka ni la muhimu sana. lakini limejificha machoni mwa watu wa kawaida na wenyewe wanasiasa hata hawataki kuligusia hili. Nafurahi kuwa wewe umelidokeza hapa. Mpaka sasa umefutwa kwa kisingizio cha Tanzania na hivyo Tanganyika inafaidikika kwa mengi tu- kiuchumi . kiulinzi, kiutamaduni, na katika mstakabala na mtizamo wa Kimataifa -mambo ambayo kama mpaka pale Chumbe utarudishwa Tanganyika itayakosa hayo. Kumbuka kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Bahari, Tanganyika hawana Bahari Kuu -wanayo hivi sasa (na wanatamba) kwa vile tu imefuta ule mpaka kati yake na Zanzibar.Jengine ambalo Tanganyika inafaidika ni mipaka, ujue muungano ukivunjika basi upande wa bahari ya mashariki litakuwa ni eneo la Zanzibar na hiyo ni nchi nyengine.Kuna complication nyingi hapo za boarder crossing.
Ha ha ha nimerudi baada ya kifungo ambacho kilinipunguzia matatizo ya macho yanayosababishwa na mwangaza wa monitor.
Hapa hapategemewi kiungo cha mboga wala mchuzi,kwani walipopongeza mapolisi na majeshi na mausalama hivyo ni vyombo vya wapi na uongozi wa Karume na Seifu ni wa wapi ,kama ni mambo ya dini bila ya shaka yeyote yalihisisha amani ya nchi na ndio hivyohivyo Ya Karume na Seifu ni kwa usalama wa nchi iwe huko kwa akina Bulicheka na mkewe au huku Zanzibar kwa waungwana.
CUF ni chama chenye nguvu Tanzania nzima hilo halina mjadala wala mbadala ,ikiwa busara waliyonayo viongozi wa CUF wataiweka kando na kuamua ya akina Savimbi na CHE basi Tanzania nzima itawaka moto ,hawa wanaoshughulikia machafuko ya mwembe chai na pale Pemba na sehemu za Unguja ,kusema la haki hawajajua ni namna gani machafuko yanatokea.
Wanachokipata na kufadhiliwa kama wametenda kazi nzuri ni simple job ambayo inakuwa inatokea kwenye sehemu maalum tena kaeneo kadogo tu ,weka kando chukulia mji kama Dsm unachafuka na riots za uhakika zinaibuka unafikiri polisi watakweza kuzuia ? Maana zikicharuka aliekuwa CUF na asiekuwa CUF wote watakuwa kitu kimoja kuhakikisha mambo yanapotulia tayari amejaza akiba ya mwaka mzima ndani ya nyumba yake.
Hivi choma kiwanda cha mafuta vamia airport weka moto ,vamia makao makuu ya bunge piga mawe magari ya serikali choma majumba ya serikali na ya viongozi maofisi na kila kilichokukalia mbele yako unavuburuga tu ,hivi polisi huyo atakwenda wapi ,kutakuwa hakunamaandamano ya kukusanyika kwenye kiwanja vya jangwani mambo ni kila kona.
Tatizo mawazo yenu ni mafupi na hayaoni zaidi ya kuta za vyumba.
Hili la mpaka ni la muhimu sana. lakini limejificha machoni mwa watu wa kawaida na wenyewe wanasiasa hata hawataki kuligusia hili. Nafurahi kuwa wewe umelidokeza hapa. Mpaka sasa umefutwa kwa kisingizio cha Tanzania na hivyo Tanganyika inafaidikika kwa mengi tu- kiuchumi . kiulinzi, kiutamaduni, na katika mstakabala na mtizamo wa Kimataifa -mambo ambayo kama mpaka pale Chumbe utarudishwa Tanganyika itayakosa hayo. Kumbuka kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Bahari, Tanganyika hawana Bahari Kuu -wanayo hivi sasa (na wanatamba) kwa vile tu imefuta ule mpaka kati yake na Zanzibar.
Fuata link http//www.un.org/Depts/los/convention-agreements/texts/unclos/closindx-uangalie vitu hapo kuna mengi kuhusu hiyo sheria ya Bahari -internal waters and territorial waters. uone kwa kiasi gani Tanganyika inafaidika kwa kutokuwepo kwa mpaka wa Chumbe. Hayo ya mkiani kule Mtwara na Lindi -mimi nayajua -please angalia ramani yako vyema ya Tanganyika, na wapi Visiwa vya Zanzibar vipo. Angalia wapi Bays and Channels zipo ambazo ni vikorombwezo muhimu katika kunufaika na hiyo Sheria ya bahari. Hapo utaona pumba!!!!!Hizo unazoita Sheria za Bahari umezipatia wapi eti bila Znz Tanganyika haitakuwa na Bahari kuu? Ina maana hiyo Znz imefunika hadi Mtwara na Lindi? Acha pumba hizo ndugu!
Hiyo link imekufa!Fuata link http//www.un.org/Depts/los/convention-agreements/texts/unclos/closindx-uangalie vitu hapo kuna mengi kuhusu hiyo sheria ya Bahari -internal waters and territorial waters.
Law of the Sea said:where the coasts of two states are opposite or adjacent to each other, neither of the two states is entitled, failing agreement between them to the contrary, to extend its territorial sea beyond the median line every point of which is equidistant from the nearest points on the baselines from which the breadth of the territorial seas of each of the two states is measured. The above provision does not apply, however, where it is necessary by reason of historic title or other special circumstances to delimit the territorial seas of the two states in a way which is at variance therewith.
museveni said:mwalimu nyerere and late mzee karume, together with the tanganyika national union (tanu) and afro-shirazi party (asp), created tanzania in 1964. Both of them are now dead. Who is benefiting from the union? It is the tanzanians of this generation. If tanganyika and zanzibar had remained separate, there would be a lot of complications which sometimes we do not think about. Take the example of the exclusive economic zones in the ocean according to the law of the sea which is supposed to be 200 nautical miles. How would tanganyika and zanzibar handle that as separate states being so entertwined? The union of tanganyika and zanzibar in 1964 obviated those problems.
Muungano muungano my ass?????!!!
WaTanganyika watafurahi sana muungano huu ukivunjika.
Hatutapoteza chochote, zaidi hasa tutakuwa tume-epuka kero na majibizano na watu vichwa maji.
Zaidi ni mzigo kwa Tanganyika,mzigo usiiyo na faida yeyote uile,lazima tuutue.
Hawa wazenj ni watu wa ajabu sana, mambo yao yakiwa mazuri hawautaki muungano; kama wakati walipodanganywa kuwa mafuta yamegunduliwa huko kwao; lakini mambo yanapowachachia ndio wanakumbuka kuwa kuna big brother[ muungano] kwamfano sasa wanapopata taabu ya umeme. Nyiewazenj mkumbuke kuwa YOU CANNOT EAT YOUR CAKE AND STILL HAVE IT!!
Kwa mujibu wa Museveni Tanganyika na Zanzibar ni Nchi zinazohitajiana. Kufutwa kwa mpaka pale Chumbe kueleweke kwa mantiki hii na siyo favour kwa Wazanzibari. Nanyi Mnatuhitaji Bwana. Hilo analolizingumza Museveni peke yake linawachachafya-achilia mengine mengi yaliyopo. We are partners and not subbordinates..Sheria za bahari zinasema...
..
..Raisi Museveni naye anazungumzia jambo hilohilo...
Jamani,
Mwungano hauhitaji marekebisho. Mwenyezi Mungu kisha take care. Mmesikia global warming? Zanzibar itazama baharini kwa muda usiotimia miaka 50 ijayo. Hawa tunawakaribisha bara bila visa. Na mafuta yatakuwa yetu sote.