Mapatano ya CUF na CCM Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapatano ya CUF na CCM Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Dec 13, 2009.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ujasiri wa Maalim Seif wa kwenda hadharani na kuwapa taarifa nzito wanachama na wapenzi wa CUF, juu ya kumtambua Rais Karume ilibidi upongezwe na Taasisi zote kuu na watanzania wote kwa jumla. Katika mazingira yeyote yaliyopo, bila ya kujua hatima ya safari hiyo ndefu, lakini hiyo ilikuwa ni hatua moja kuelekea katika kupunguza mvutano wa kisiasa kati ya CUF na CCM Zanzibar.

  Kwa mshangao mkubwa ni zaidi ya mwezi sasa hivi toka tukio hilo litokee, lakini si Pengo, Kilaini, Askofu Shayo au viongozi wa KKKT waliodiriki kutoa pongezi zao kwa tukio hilo. Baraka za viongozi hawa ni muhimu sana, hasa ukizingatia kuwa huko nyuma katika matukio tofauti walijitokeza ni kutoa maoni yao. Kwa mfano wakati wa machafuko ya Mwembechai, Pengo alisikika katika Radio Tumaini akiipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua katika kudumisha amani. Nilitarajia katika tukio hili kubwa la kihistoria la kumtambua Rais Karume vile vile kuwa Pengo angetoa pongezi.

  Lakini hasa nini maana ya ukimya huo? Hili ni swali ambalo nafikiri kila mtanzania anajiuliza. Sihitaji kuja na mawazo yangu kwa hili, lakini ingekuwa vyema kama viongozi hawa wenyewe wangetjitokeza hadharani na kueleza sababu za ukimya wao. Aidha ningewaomba wanJF wenye upeo mkubwa wakuwaelewa viongozi hawa pamoja na wale waliobahatika kujiwa na Roho Mtakatifu watueleze sababu ya ukimya wao.

  Amani ya Zanzibar ni Amani ya Tanzania nzima, hivyo si siri kuwa mapatano ya CUF na CCM Zanzibar ni ushindi kwa watanzania wote. Na hatua iliyochukuliwa na Rais Karume na Maalim Seif ni kwa faida na maslahi ya Tanzania nzima. Tuwaombee waendelee vizuri.
   
 2. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  wewe nawe? ndo maana Tanzania hatuendelei.
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,399
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Zawadi: CUF - CCM ni Vyama vya siasa.
  Machafuko ya Mwembechai yalikuwa ni mambo ya dini.
  Elezea connection iliyopo hapa, CUF - CCM, Pengo na Mwembechai; au tayari ndiyo huo utafiti wako!

  I can't see logic here!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama kila Mtanzania anajiuliza hivyo
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha nimerudi baada ya kifungo ambacho kilinipunguzia matatizo ya macho yanayosababishwa na mwangaza wa monitor.
  Hapa hapategemewi kiungo cha mboga wala mchuzi,kwani walipopongeza mapolisi na majeshi na mausalama hivyo ni vyombo vya wapi na uongozi wa Karume na Seifu ni wa wapi ,kama ni mambo ya dini bila ya shaka yeyote yalihisisha amani ya nchi na ndio hivyohivyo Ya Karume na Seifu ni kwa usalama wa nchi iwe huko kwa akina Bulicheka na mkewe au huku Zanzibar kwa waungwana.
  CUF ni chama chenye nguvu Tanzania nzima hilo halina mjadala wala mbadala ,ikiwa busara waliyonayo viongozi wa CUF wataiweka kando na kuamua ya akina Savimbi na CHE basi Tanzania nzima itawaka moto ,hawa wanaoshughulikia machafuko ya mwembe chai na pale Pemba na sehemu za Unguja ,kusema la haki hawajajua ni namna gani machafuko yanatokea.
  Wanachokipata na kufadhiliwa kama wametenda kazi nzuri ni simple job ambayo inakuwa inatokea kwenye sehemu maalum tena kaeneo kadogo tu ,weka kando chukulia mji kama Dsm unachafuka na riots za uhakika zinaibuka unafikiri polisi watakweza kuzuia ? Maana zikicharuka aliekuwa CUF na asiekuwa CUF wote watakuwa kitu kimoja kuhakikisha mambo yanapotulia tayari amejaza akiba ya mwaka mzima ndani ya nyumba yake.
  Hivi choma kiwanda cha mafuta vamia airport weka moto ,vamia makao makuu ya bunge piga mawe magari ya serikali choma majumba ya serikali na ya viongozi maofisi na kila kilichokukalia mbele yako unavuburuga tu ,hivi polisi huyo atakwenda wapi ,kutakuwa hakunamaandamano ya kukusanyika kwenye kiwanja vya jangwani mambo ni kila kona.
  Tatizo mawazo yenu ni mafupi na hayaoni zaidi ya kuta za vyumba.
   
 6. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toka vianze vyama vingi vya siasa, kumekuwa na uhasama mkubwa kati ya ccm na cuf kwa upande wa znz. Kwa mtazamo wa wengi, uhasama huu umesaidia kwa upande wa bara kwa sababu wa znz badala ya kudai haki zao za msingi kutoka bara wamekuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe. Wakati Mwalimu Nyerere yuko hai, wa znz walikuwa wakimuogopa sana, lakini toka amefariki na hofu yao imeondoka. Nimesafiri nchi nyingi sana, watu wengi kutoka Europe, Asia na America hawaijui Tanzania, lakini wanaijuwa znz kutokana na historia yake. Watalii wengi wanakuja Tanzania kutokana na umaarufu wa znz duniani. Neema kubwa tunayopata Tanzania inatokana na kuweko kwa huu muungano. Hofu kubwa inayojitokeza ni kuwa endapo cuf na ccm wataelewana huenda ikapelekea wakadai haki zao nyingi ambazo upande wa bara wamekuwa wakiziminya, na hii inaweza pia ikaleta mvutano ambao ukasababisha kuvunjika kwa muungano!.. wana jf mawazo yenu yanakaribishwa
   
 7. m

  mdini Member

  #7
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muungano muungano my ass?????!!!

  WaTanganyika watafurahi sana muungano huu ukivunjika.

  Hatutapoteza chochote, zaidi hasa tutakuwa tume-epuka kero na majibizano na watu vichwa maji.

  Zaidi ni mzigo kwa Tanganyika,mzigo usiiyo na faida yeyote uile,lazima tuutue.
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Muungano wowote duniani sio kitu kibaya, hata kuungana kati ya mtu na mtu ni kitu chema, tatizo ni kwamba muungano wenyewe uliwahusisha watu wachache na ulifanywa kutokana na umuhimu uliokuwepo wakati huo. Mimi naogopa kusema nani atafaidika na kuvunjika kwa muungano lakini naamini bara wataathirika ki siasa zaidi lakini kwa znz kama mtoa mada unavyopenda itamkwe kuna athari za ki uchumi ambazo ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote duniani.

  Sababu za wakati ule tunaaminishwa kwamba zilikuwa za ki usalama, kwa znz yenyewe na hivyo TZ (Tanganyika wakati huo). Ki msingi siioni mantiki ya watu kuzungumzia jinsi ya kutengana saa hizi, ni rahisi kwa mfano mtu kuzungumzia kitu ambacho hajawahi kukutana nacho, inakuja jumuia ya afrika masharika sasa hivi nchi kama Rwanda,Burundi na hata Kenya kwao shirikisho lina maana kama wananchi wao watafaidika na ardhi ya Tanzania nyie Znz mnafikiria kuikimbia neema.

  Tunawaombea mfanikishe salama na kwa busara kwa sababu dhambi ya ubaguzi ni lazima itakutafuneni, mlishaambiwa kwamba kuna bara na zanzibara once mko ndani ya muungano, nje ya muungano hakuna iyo kitu na badala yake kuna pemba na unguja, kwa wanaodhani ubashiri huu ni utani fanyeni makeke mtakapo anza kuchapana bakora sijui mtakimbilia wapi?
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapo hapavunjwi Muungano kwani watu na vyama vyote vinahitaji uwepo wa serikali tatu isipokuwa Chama Cha Manyang'anyi ,hao ndio usiwambie kitu kuhusu serikali tatu ,mbona zipo nchi nyingi na serikali za aina hiyo ,wale wamanga kule nchi zao kama saba na kila moja ina serikali yake na ipo serikali kuu,hapo nakupa kufikiri na kama haitoshi ikiwa huelewi juzi tu nilifuatana na kigogo wa CCM katika ziara huko ya kibinafsi ,tulishangaa kwa pamoja baada ya kuambiwa kuwa serikali kuu ndani yake ina serikali saba na vile vile hakuna tatizo si kwa raia wala viongozi na yapo mambo ambayo yanaendeshwa kiumoja na pia ipo kusaidiana bila ya tatizo lolote lile na wananchi wala hawana malalamiko nchi ni shwari wala huwezi kujua kama kuna serikali saba ndani ya moja.

  Sasa la kujiuliza ni kwanini hiki Chama Cha Machangudoa hakitaki serikali tatu ? Mtu yeyote ambae mawazo yake ni free hahitaji msaada wa kusaidiwa mawazo anaweza kupekecha na kupata hisia na kwa hapa JF home of great thinkerz ,wanaweza kutoa mchango huo ni kwa nini wanakataa serikali tatu ?

  Napenda ufahamu tu kuwa hiki Chama Cha Matapeli maana hata shahada za viongozi wao zimekumbwa na balaa kama si matapeli tuwaiteje wamewatapeli wananchi kwa kusema wanamiliki shahada za ajabu ajabu uzamivu,tena international .aloo jamaa mwisho ni lazima uone ni kwanini wanalipinga suala la serikali tatu.ni utapeli tu.

  Nikiongezea kuhusu hiki Chama Cha Majambazi ,wameuza wamekopa wamechukua ,wamejinunulisha mali za serikali yakiwemo majumba,migodi ,mikopo na mengine mengi tu hata Ikulu wamefanya grocery na kuanzisha biashara hapo.Kumbuka tu hakuna Mzanzibari katika hao wakati nao wapo ndani ya serikali hio inayoitwa ya Muungano.

  Nikihitimisha na Chama Cha Mauzauza ambacho kimemfanya Mtanzania kuwa kama mwehu ndani ya nchi yake asieelewa kinachoendelea au kinachofanywa na Serikali iliyoundwa na chama chao kwa jaili ya kumletea maendeleo zaidi ni kwa serikali hii kuwafanya waTanzania kama wanaotazama cinema leo au kila baada ya muda kunakuwa na mchezo au igizo jipya ,michezo na maigizo yote hayo WaZanzibari hawahusiki ili kueleweka naweza kusema hayawatachi japo nao wamo katika hiyo serikali iitwayo ya Muungano.

  Ni kosa kusema CCM CUF maelewano hapana maelewano hayo yanaihusisha CUF na sio CCM kwani ilikwishatengwa zamani na sababu haswa ni hayo niliyoyaeleza juu kuwa WaZanzibari hawakushirikishwa na hawamo katika visa vitendavyo na baadhi ya walio katika hiyo iitwayo serikali ya Muungano.

  Namaliza kwa kusema hatari itakayotokea ni kuundwa upya kwa serikali hiyoya Muungano ambayo itabidi uwepo wa Tanganyika,jambo ambalo ni hasara kwa Chama Cha Manduli ambao wamekalia midomo wazi kuwameza WaTanzania na kuwafanya masikini wa kutupwa.Hasara ambayo itawabidi wapoteze nyadhifa zote zinazoiunda serikali hiyo ,kazi ambayo itafanywa ni kuwepo kwa transit government ya Muungano ili iitishe uchaguzi mkuu wa Tanganyika hapo CCM itaparaganyika maana hawakubaliki katika hali ya haki na usawa kwa uchaguzi ,ni kusema itapoteza sehemu nyingi na ndio utakuwa mwicho wa ukiritimba wa Chama Cha Majangili.
  Nakaribisha maoni.
   
 10. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,042
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  muungano na ufe,sie watanganyika tumeuchoka sasa,tuwaachie vijisiwa vyao tuone hayo maendeleo wanayoyaota period.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Muungano njomba haufi ,hilo nakuhakikishia ila Chama Cha Mashetani ndio kitakufa na kipo njiani ,haiwezekani vyama vyote vione umuhimu wa Muungano isipokuwa Chama Cha Makamati.
  Na yeyote yule utakaemsikia kuwa bora muungano ufe huyo atakuwa ana agenda ya siri na ni mmoja katika wafuasi wa Chama Cha Sultani CCM pengine anaona ukifa serikali iliyotokuwepo itaendelea na kuzidi kuwazuga Watanganyika kwa mikakati ya baada ya miaka mia.
   
 12. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,399
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Mwiba acha dini twende kwenye Siasa. Mambo haya ya dini yana wao.
  Kuhusu huo muafaka na sasa hivi kukiri kuwa Karume ni Rais ni mbadala kwa CUF. Sote tunakubali, lakini vilevile tukubali CCM ni mbabe. Ila kuanza kuwasakama watu wa dini ati vile au vile hizo ndiyo chokochoko. Mie nilifikiri zaidi wanasiasa, vyama, Diplomatic Corps ilibidi ndiyo wawe mstari wa mbele kushangilia maana haya yote ni sasa.
  Kwa kumalizia, hayo yote uliyoyasema, sijui yana uzito gani. Lakini ukweli ni kuwa CUF pamoja na kuwa ni Chama chenye nafasi kubwa imekwishafika ukingoni, Maalim Seif anajua kabisa wakati wake umekwisha. Lipumba popularirty imekwisha. Hawana strategy mpya, they have exhausted all means; na wanajua kuwa Chadema has emerged as their rivals to challenge CCM. Sasa hivi CUF wanachofanya ni ule usemi kuwa you can't beat CCM but better join their ideas and do things within. Hope kubwa ya CUF ni at least have to netralize other opposition parties forces by making love to their foes.

  But you are not realizing that you could have obtained such peace of mind by uniting with Chadema or others. Remember that in past elections you were partners with CHADEMA, now what is making Chadema your foes? and befiriending a devil which haunted you for all these years. Unasahau vile virungu alivyopigwa Lipumba. Maalim alikimbilia Denmark.

  But contratulations for Maalim for realising that our priority for this country is peace with CCM; long live MUAFAKA and KUDOS to CCM!!
   
 13. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Jambo hili linalohusu muungano linahitaji umakini sana kulishughulikia. Halitaki jazba wala haraka na zaidi halitaki umimi.
  Tunahitaji sana kufanya tathmini makini ya umuhimu wa muungano wetu. There is need for a critical analysis of the benefits, adavantages and disadvantages of this union to both parties, meaning Tanganyika and Zanzibar.

  Nina hakika kama hilo litafanyika na watu waelewa na walioelimika wataona kuna umuhimu wa kuundeleza huu muungano lakini siyo hivi ulivyo sasa. Kuna haja ya kuuboresha tu.

  Tunaweza kudhani kuwa serikali tatu ni suluhisho lakini tukajikuta tumeharibu hata maana yake. There will exist an unnecessary duplication of efforts, jambo ambalo litawagharimu pande zote. Kwa mfano tutahitaji kila upande uwe na Mabalozi wake halafu na ya tatu nayo iwe na mabalozi wake? Sarafu zitakuwa je? Tatu?. Waziri wa Ulinzi wa Zanzibar, wa Tanganyika na wa Tanzania? Bunge na Wabunge je?.

  Muungano ni sawa na ndoa nini? waliomo wanataka kutoka na wasiokuwemo wanapambana waweze kuingia?

  Katiba yetu, ..nadhani!..., ndiyo tatizo. Ufahamu wa wananchi wengi kuhusu huu muungano pia ni mdogo sana. Jambo hili linatakiwa kufanyiwa kazi. Ni jambo tunatakiwa kulishughulikia watanzania wote, hata tukilijadili sote kwa uwazi miaka kumi lakini muhumu ni tufikie muafaka. Tatizo kubwa pia tulilo nalo ni hiki chama cha wababe. Ambacho kila kitu hufanyika kwa kificho ficho, kwamba wananchi wasijue, kwa kulindana lindana. Hata yale yaliyo wazi kabisaa wanakuwa na ujasiri wa ajabu wa kujaribu kuyafunika tena wakisuburi wananchi wasahau, na mara nyingi tumeonekana kweli kusahau.

  Watanzania tunahitajika kuwa majasiri wa kupambana na matatizo yetu.
  We have more than enough of them including the one in question and we need to address them vertically! Hatuja jaaliwa uongozi wa kutupa mwelekeo huo.
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Yakhe hebu jiheshimu kidogo!
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jamani,
  Mwungano hauhitaji marekebisho. Mwenyezi Mungu kisha take care. Mmesikia global warming? Zanzibar itazama baharini kwa muda usiotimia miaka 50 ijayo. Hawa tunawakaribisha bara bila visa. Na mafuta yatakuwa yetu sote.
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Theory of climate change and global warming is fake! wanaharakti wanatafuta pesa za kufanya utafiti hakuna uhusiano wowote ule kati ya kuongezeka kwa joto duniani na co2...

  zenj itakuwepo vizazi hadi vizazi inshallah mpaka mwisho wa dunia

  muungano utakuwepo ila wa heshima mutual respect...and benefit...

  viongozi waliopo sasa hawawezi kuleta muungano huo (siyo JK, Karume wala seif) wote ni wabaguzi hawana maana yoyote

  muungano utaletwa na rika nyingine ya viongozi walio tembea duniani na wenye uwezo wa ku-negotiate kwa pande zote mbili bila kuogopana...enzi za mchonga za fikra sahihi na udikteta finito

  CUF na CCM huu umoja wao wa sasa ni fake..wala hautadumu..either ni donor funded (hidden) au ni kwamba wameona wote wawili (seif na karume) wameanza kuishiwa na peoples power which coming soon.
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Pengo na kina shayo wapo kwa maslahi ya kanisa tu na si vinginevyo.
   
 18. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Hata wakiwa kwa maslahi ya kanisa, bado AMANI ni muhimu hata kwa wao pia au sio.

  Tukubaliane kwamba panapokuwepo na amani hutunufaisha sote bila ya kujali dini dhehebu, matajiri, masikini wala kabila. Kwa hiyo ni mategemeo yangu kuwa pindi mti wa amani unapoota na kukuwa ni muhimu kwetu sote kwenda kuumwagilia maji na kuutilia mbolea.

  Sasa wako wapi akina Pengo na Kilaini katika jukumu hili la kuumwagilia maji na kuutilia mbolea mti huu mchanga wa AMANI?
   
 19. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  kUENDELEA KOKOTE KULE KWA NCHI KUNAHITAJI AMANI. KUKOSEKANA KWA AMANI ZANZIBAR KWAFAHAMIKA DUNIA NZIMA. VIPI LEO TOKEO HILI TULIPUUZIE? HATUKUMBUKI KUWA WAKIMBIZI WAKWANZA TOKA TANZANIA KULISABABISHWA NA KUTOKUELEWANA KWA CCM NA CUF?
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Hakika yashangaza !

  • Wale ambao hawaishi kulalamika kuhusu Muungano ndio hao hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga kuvunjika kwake !
  • Wale ambao hawaoni faida ya Muungano hawalalamiki lakini wapo mstari wa mbele kuunga mkono kuvunjika kwake !
  Naona kuna katabia hapa ka katoto kachanga kama alivyowahi kusema Mwalimu - ukikapakata kanakunyea, ukikaacha kanalia. Nafikiri kuna janja ya nyani hapa - walalamishi wanajua sana faida za Muungano, wanauhitaji ati. Wakati moja anahitaji Muungano, mwingine ni muungano unamhitaji.
   
Loading...