Mapatano ya CUF na CCM Zanzibar

Hakika yashangaza !

  • Wale ambao hawaishi kulalamika kuhusu Muungano ndio hao hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga kuvunjika kwake !
  • Wale ambao hawaoni faida ya Muungano hawalalamiki lakini wapo mstari wa mbele kuunga mkono kuvunjika kwake !
Naona kuna moja hapa kana katabia hapa ka katoto kachanga kama alivyowahi kusema Mwalimu - ukikapata kanakunyea, ukikaacha kanalia. Nafikiri kuna janja ya nyani hapa - walalamishi wanajua sana faida za Muungano, wanauhitaji ati. Wakati Zenji wanahitaji Muungano, Bara ni muungano unawahitaji.
Wataje tuwafahamu walalamishi? kuna tofauti ya kudai kuna kero za muungano na kulalamika

Wataje tuwafahamu ambao hawaoni faida ya muungano?
 
Muungano njomba haufi ,hilo nakuhakikishia ila Chama Cha Mashetani ndio kitakufa na kipo njiani ,haiwezekani vyama vyote vione umuhimu wa Muungano isipokuwa Chama Cha Makamati.
Na yeyote yule utakaemsikia kuwa bora muungano ufe huyo atakuwa ana agenda ya siri na ni mmoja katika wafuasi wa Chama Cha Sultani CCM pengine anaona ukifa serikali iliyotokuwepo itaendelea na kuzidi kuwazuga Watanganyika kwa mikakati ya baada ya miaka mia.
Muungano hauwezi kuendelea kwa lazima, kwani haziungani ardhi bali watu.

Ikiwa watu hawataki muungano, vipi uwalazimishe.
Ni muhimu tufuate haki katika kipindi hiki cha Demokrasia.

Tanzania si ya kwanza kuungana, na wala haitakuwa ya kwanza kutengana ikiwa itabidi kufanya hivyo.
 
Ujasiri wa Maalim Seif wa kwenda hadharani na kuwapa taarifa nzito wanachama na wapenzi wa CUF, juu ya kumtambua Rais Karume ilibidi upongezwe na Taasisi zote kuu na watanzania wote kwa jumla. Katika mazingira yeyote yaliyopo, bila ya kujua hatima ya safari hiyo ndefu, lakini hiyo ilikuwa ni hatua moja kuelekea katika kupunguza mvutano wa kisiasa kati ya CUF na CCM Zanzibar.

Wapongeze nini na wakati context ya makubaliano hayo haya julikani mpaka leo? Sawa wame kubaliana na CUF imemtambua Karume lakini nini haswa wame kubaliana? Je hauoni itakua aibu kubwa watu wakianza kutoa pongezi halafu ikigundulika mambo waliyo kubaliana ni ndivyo sivyo? Kama kweli makubaliano yao ni kwa manufaa ya taifa watuambie wame kubaliana nini na wame ahidiana nini.

Kwa mshangao mkubwa ni zaidi ya mwezi sasa hivi toka tukio hilo litokee, lakini si Pengo, Kilaini, Askofu Shayo au viongozi wa KKKT waliodiriki kutoa pongezi zao kwa tukio hilo. Baraka za viongozi hawa ni muhimu sana, hasa ukizingatia kuwa huko nyuma katika matukio tofauti walijitokeza ni kutoa maoni yao. Kwa mfano wakati wa machafuko ya Mwembechai, Pengo alisikika katika Radio Tumaini akiipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua katika kudumisha amani. Nilitarajia katika tukio hili kubwa la kihistoria la kumtambua Rais Karume vile vile kuwa Pengo angetoa pongezi.

Kwa nini mashekhe nao wasitoe pongezi? Kwa nini mna lazimisha viongozi wa makanisa watoe matamko? Siku zote wakiongea mnasema wasiingilie siasa au Wakristo wana taka kucontrol mambo. Leo iweje mtake watamke chochote? Silence can never be misquoted na mimi nawa shauri viongozi hawa wakae kimya hivyo hivyo. Kwanza makubaliano yenyewe hawajui wame kubaliana nini kwa hiyo watoe pongezi za nini?

Lakini hasa nini maana ya ukimya huo? Hili ni swali ambalo nafikiri kila mtanzania anajiuliza. Sihitaji kuja na mawazo yangu kwa hili, lakini ingekuwa vyema kama viongozi hawa wenyewe wangetjitokeza hadharani na kueleza sababu za ukimya wao. Aidha ningewaomba wanJF wenye upeo mkubwa wakuwaelewa viongozi hawa pamoja na wale waliobahatika kujiwa na Roho Mtakatifu watueleze sababu ya ukimya wao.

Ache kugeneralize ndugu. Nani kakuambia kila Mtanzania ana jiuliza? Mawazo yako wewe umefanya mawazo ya kila mtu? Au nayo hii ni matokeo ya moja ya "tafiti" zako?

Amani ya Zanzibar ni Amani ya Tanzania nzima, hivyo si siri kuwa mapatano ya CUF na CCM Zanzibar ni ushindi kwa watanzania wote. Na hatua iliyochukuliwa na Rais Karume na Maalim Seif ni kwa faida na maslahi ya Tanzania nzima. Tuwaombee waendelee vizuri.

Tunacho takiwa kuomba ni kwamba hayo makubaliano hayata kua na vipengele vyo vyote vitakavyo ingiza taifa katika matatizo. Bado naendelea kuimba huu mwimbo. Bila kujua makubaliano ni yapi haswa lazima watu tujiulie mara mbili mbili. Hauwezi kufurahia mkataba kabla hauja usoma.
 
Amani ya Zanzibar ni Amani ya Tanzania nzima, hivyo si siri kuwa mapatano ya CUF na CCM Zanzibar ni ushindi kwa watanzania wote. Na hatua iliyochukuliwa na Rais Karume na Maalim Seif ni kwa faida na maslahi ya Tanzania nzima. Tuwaombee waendelee vizuri.

Yes, ya ngoso mwachie ngoso mwenyewe, hawa viongozi wawili wameamua kuwa Zanzibar ni ya wazanzibar wote na siyo CCM wala CUF, sasa wakaweka utaifa mbele na fasta fasta wamemaliza tofauti zao, ugomvi wa mtu na nduguye ukiingilia mwisho wa siku utaaibika, hayo maongezi ya muafaka chini ya makamba yamechukua miaka mingapi na yalifikia wapi? mbona hawa jamaa wamefanya fasta na kumaliza tofauti zao. ndugu ni ndugu bwana. Makamba umeona na umejifunza nini? tatizo huwa hupendi kukubali matokeo.
 
Jamani,
Mwungano hauhitaji marekebisho. Mwenyezi Mungu kisha take care. Mmesikia global warming? Zanzibar itazama baharini kwa muda usiotimia miaka 50 ijayo. Hawa tunawakaribisha bara bila visa. Na mafuta yatakuwa yetu sote.

JAS-WISSU tutake radhi,,chonde chonde tutake radhi ndugu yetu kabla hatujakusomea HALBADIRI....Zanzibar haitoweki milele,,WELA mafuta hatugawani,,,yetu wenynnnnyewe,,hata kama nusu kifuniko tutajipaka mwilini tung'ae
 
JAS-WISSU tutake radhi,,chonde chonde tutake radhi ndugu yetu kabla hatujakusomea HALBADIRI....Zanzibar haitoweki milele,,WELA mafuta hatugawani,,,yetu wenynnnnyewe,,hata kama nusu kifuniko tutajipaka mwilini tung'ae
sI UONGO, ni vyema atutake radhi.
 
Mukianza kujadili muungano kuna woga fulani ambao umo kwenye nyoyo za watanganyika, kuna wengine hapa kwenye thread hii wamejikaza kisabuni kusema ati Tanganyika hawataki muungano.Hivi mbona hata kipofu anaona kama Tanganyika ikiamua leo kesho haitaki muungano, basi unavunjika hapo hapo.Hizi ni hesabu za logic, kwamba idadi kubwa ya Tanzania ni Tanganyika na kijisehemu kiduchu ndio Zanzibar.

Kwa hiyo hapo haiwezekani ikawa Zanzibar ndio inalazimisha kuwepo kwa Tanzania, bali ni kinyume chake yaani Tanganyika ndio imeshikilia mpini na kung'ang'ania kuwepo kwa muungano.

Kuna sababu nyingi unapoona serekali inalazimisha kuwepo kwa muungano, kuna sababu za kisiasa.Politician siku zote wanataka mamlaka mingi, kwa hiyo Tanganyika inafaidika kwa kujiongezea mamlaka ya kuiburuza Zanzibar.Na hili liko wazi kabisa, sijuwi kwanini watanganyika munalikimbia na kufanya kama hamulioni.

Jengine ambalo Tanganyika inafaidika ni mipaka, ujue muungano ukivunjika basi upande wa bahari ya mashariki litakuwa ni eneo la Zanzibar na hiyo ni nchi nyengine.Kuna complication nyingi hapo za boarder crossing.

Tukiachana na hayo, pengine muanze kujiuliza Zanzibar inafaidika na nini kwa mfumo uliopo sasa?Mie naweza kusema hakuna, sababu hizo za kiusalama ni babaisha ***** tuu.Siku hizi nchi ikivamia nchi nyengine dunia nzima inakuja juu kupinga, tukitoa kesi ya Izraili ofcourse.

Kumalizia, naweza kusema muungano sio kitu kibaya ni mfumo tuu ndio mbovu.Mie nishaona miungano kibao ambayo watu wanafaidika, ukiwemo muungano wa EU.Ambapo ni raha sana, unatoka Germany kuingia Holland bila ya kuulizwa chochote, unaendesha gari tuu na kucross boarder bila ya hata kusumbuliwa na Immigration officers.Lakini hawa watu wameungana, na faida zinaonekana kabisa wala hakuna alipoteza utaifa wake.

Tatizo liliopo ni kuwa watanganyika hawataki utaifa wao, na hupenda waitwe watanzania tofauti na wazanzibari ambao hadi leo wanataka watumie utaifa wao.Jambo ambalo Nyerere hakulitaka, na alitumia kila mbinu kuhakikisha kuwa Zanzibar na Tanganyika zinakufa na inabaki Tanzania.Hilo ndio kosa liliopo, kwa hiyo turudi step mbili tatu nyuma turudishe mataifa yetu Tanganyika na Zanzibar, halafu tuunde muungano mwengine wa EAC.
 
zawadi: Cuf - ccm ni vyama vya siasa.
Machafuko ya mwembechai yalikuwa ni mambo ya dini.
Elezea connection iliyopo hapa, cuf - ccm, pengo na mwembechai; au tayari ndiyo huo utafiti wako!

I can't see logic here!

na pale kanisa linapoandika waraka wake, jee huu waraka ni wa dini na pale pengo anaposema muungano wa Tanzania usichokonolewe jee tuelewe kuwa muungano huu ni wa kidini?????
 
Jengine ambalo Tanganyika inafaidika ni mipaka, ujue muungano ukivunjika basi upande wa bahari ya mashariki litakuwa ni eneo la Zanzibar na hiyo ni nchi nyengine.Kuna complication nyingi hapo za boarder crossing.
Hili la mpaka ni la muhimu sana. lakini limejificha machoni mwa watu wa kawaida na wenyewe wanasiasa hata hawataki kuligusia hili. Nafurahi kuwa wewe umelidokeza hapa. Mpaka sasa umefutwa kwa kisingizio cha Tanzania na hivyo Tanganyika inafaidikika kwa mengi tu- kiuchumi . kiulinzi, kiutamaduni, na katika mstakabala na mtizamo wa Kimataifa -mambo ambayo kama mpaka pale Chumbe utarudishwa Tanganyika itayakosa hayo. Kumbuka kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Bahari, Tanganyika hawana Bahari Kuu -wanayo hivi sasa (na wanatamba) kwa vile tu imefuta ule mpaka kati yake na Zanzibar.
 
Ha ha ha nimerudi baada ya kifungo ambacho kilinipunguzia matatizo ya macho yanayosababishwa na mwangaza wa monitor.
Hapa hapategemewi kiungo cha mboga wala mchuzi,kwani walipopongeza mapolisi na majeshi na mausalama hivyo ni vyombo vya wapi na uongozi wa Karume na Seifu ni wa wapi ,kama ni mambo ya dini bila ya shaka yeyote yalihisisha amani ya nchi na ndio hivyohivyo Ya Karume na Seifu ni kwa usalama wa nchi iwe huko kwa akina Bulicheka na mkewe au huku Zanzibar kwa waungwana.
CUF ni chama chenye nguvu Tanzania nzima hilo halina mjadala wala mbadala ,ikiwa busara waliyonayo viongozi wa CUF wataiweka kando na kuamua ya akina Savimbi na CHE basi Tanzania nzima itawaka moto ,hawa wanaoshughulikia machafuko ya mwembe chai na pale Pemba na sehemu za Unguja ,kusema la haki hawajajua ni namna gani machafuko yanatokea.
Wanachokipata na kufadhiliwa kama wametenda kazi nzuri ni simple job ambayo inakuwa inatokea kwenye sehemu maalum tena kaeneo kadogo tu ,weka kando chukulia mji kama Dsm unachafuka na riots za uhakika zinaibuka unafikiri polisi watakweza kuzuia ? Maana zikicharuka aliekuwa CUF na asiekuwa CUF wote watakuwa kitu kimoja kuhakikisha mambo yanapotulia tayari amejaza akiba ya mwaka mzima ndani ya nyumba yake.
Hivi choma kiwanda cha mafuta vamia airport weka moto ,vamia makao makuu ya bunge piga mawe magari ya serikali choma majumba ya serikali na ya viongozi maofisi na kila kilichokukalia mbele yako unavuburuga tu ,hivi polisi huyo atakwenda wapi ,kutakuwa hakunamaandamano ya kukusanyika kwenye kiwanja vya jangwani mambo ni kila kona.
Tatizo mawazo yenu ni mafupi na hayaoni zaidi ya kuta za vyumba.

Hivi ukikaa kimya kuna hasara gani?
 
Hili la mpaka ni la muhimu sana. lakini limejificha machoni mwa watu wa kawaida na wenyewe wanasiasa hata hawataki kuligusia hili. Nafurahi kuwa wewe umelidokeza hapa. Mpaka sasa umefutwa kwa kisingizio cha Tanzania na hivyo Tanganyika inafaidikika kwa mengi tu- kiuchumi . kiulinzi, kiutamaduni, na katika mstakabala na mtizamo wa Kimataifa -mambo ambayo kama mpaka pale Chumbe utarudishwa Tanganyika itayakosa hayo. Kumbuka kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Bahari, Tanganyika hawana Bahari Kuu -wanayo hivi sasa (na wanatamba) kwa vile tu imefuta ule mpaka kati yake na Zanzibar.

Hizo unazoita Sheria za Bahari umezipatia wapi eti bila Znz Tanganyika haitakuwa na Bahari kuu? Ina maana hiyo Znz imefunika hadi Mtwara na Lindi? Acha pumba hizo ndugu!
 
Hizo unazoita Sheria za Bahari umezipatia wapi eti bila Znz Tanganyika haitakuwa na Bahari kuu? Ina maana hiyo Znz imefunika hadi Mtwara na Lindi? Acha pumba hizo ndugu!
Fuata link http//www.un.org/Depts/los/convention-agreements/texts/unclos/closindx-uangalie vitu hapo kuna mengi kuhusu hiyo sheria ya Bahari -internal waters and territorial waters. uone kwa kiasi gani Tanganyika inafaidika kwa kutokuwepo kwa mpaka wa Chumbe. Hayo ya mkiani kule Mtwara na Lindi -mimi nayajua -please angalia ramani yako vyema ya Tanganyika, na wapi Visiwa vya Zanzibar vipo. Angalia wapi Bays and Channels zipo ambazo ni vikorombwezo muhimu katika kunufaika na hiyo Sheria ya bahari. Hapo utaona pumba!!!!!
 
Fuata link http//www.un.org/Depts/los/convention-agreements/texts/unclos/closindx-uangalie vitu hapo kuna mengi kuhusu hiyo sheria ya Bahari -internal waters and territorial waters.
Hiyo link imekufa!
 
Suala la Viongozi wa dini uliowataja kutoa pongezi kwa Maalimu Seif kwa sababu eti sasa ndipo amemtambua Karume kuwa ni Rais wa Zanzibar ni suala ambalo linahitaji tafakari makini!. Mimi binafsi ninaona amechelewa mno! Amechelewa kwa sababu ya ubinafsi wake!. Mbona wakati alipokuwa akizunguka zunguka kule nje (Malekani nk), kutaka mataifa makubwa yaiwekee Tanzania Vikwanzo, viongozi hao uliowataja hawakujitokeza kumkemea? Iweje sasa hivi alipoona uchaguzi unakaribia ndipo anakurupuka kumtambua Karume? Pili alisema, wakati akiongea na wanachama wake, kwamba maongezi yao na Karume ni siri. Lakini tumemwona hivi karibuni akianza kumwaga hadharani yale waliyoyaongea na Karume! Sasa hapa unataka kusema nini? Bado kuna mambo mengi hayajawekwa wazi kutokana na Seif kumtambua Karume!. Kuna kila dalili kwamba amefanya hivyo kwa kuwapaka waTanzania mafuta kwa mgogo wa chupa!.

Kiongozi awaye yote, hasa wa dini, aliye makini, hawezi kukurupuka kutoa pongezi!
 
..Sheria za bahari zinasema...

Law of the Sea said:
where the coasts of two states are opposite or adjacent to each other, neither of the two states is entitled, failing agreement between them to the contrary, to extend its territorial sea beyond the median line every point of which is equidistant from the nearest points on the baselines from which the breadth of the territorial seas of each of the two states is measured. The above provision does not apply, however, where it is necessary by reason of historic title or other special circumstances to delimit the territorial seas of the two states in a way which is at variance therewith.

..

..Raisi Museveni naye anazungumzia jambo hilohilo...


museveni said:
mwalimu nyerere and late mzee karume, together with the tanganyika national union (tanu) and afro-shirazi party (asp), created tanzania in 1964. Both of them are now dead. Who is benefiting from the union? It is the tanzanians of this generation. If tanganyika and zanzibar had remained separate, there would be a lot of complications which sometimes we do not think about. Take the example of the exclusive economic zones in the ocean according to the law of the sea which is supposed to be 200 nautical miles. How would tanganyika and zanzibar handle that as separate states being so entertwined? The union of tanganyika and zanzibar in 1964 obviated those problems.
 
Muungano muungano my ass?????!!!

WaTanganyika watafurahi sana muungano huu ukivunjika.

Hatutapoteza chochote, zaidi hasa tutakuwa tume-epuka kero na majibizano na watu vichwa maji.

Zaidi ni mzigo kwa Tanganyika,mzigo usiiyo na faida yeyote uile,lazima tuutue.

Hawa wazenj ni watu wa ajabu sana, mambo yao yakiwa mazuri hawautaki muungano; kama wakati walipodanganywa kuwa mafuta yamegunduliwa huko kwao; lakini mambo yanapowachachia ndio wanakumbuka kuwa kuna big brother[ muungano] kwamfano sasa wanapopata taabu ya umeme. Nyiewazenj mkumbuke kuwa YOU CANNOT EAT YOUR CAKE AND STILL HAVE IT!!
 
Hawa wazenj ni watu wa ajabu sana, mambo yao yakiwa mazuri hawautaki muungano; kama wakati walipodanganywa kuwa mafuta yamegunduliwa huko kwao; lakini mambo yanapowachachia ndio wanakumbuka kuwa kuna big brother[ muungano] kwamfano sasa wanapopata taabu ya umeme. Nyiewazenj mkumbuke kuwa YOU CANNOT EAT YOUR CAKE AND STILL HAVE IT!!

,,,,aaah Bro TANGANYIKA njoo basi utusaidie na tatizo hili la umeme,tunajua unatupenda sana kwa kuturushia huo umeme mpaka ng'ambo ya pili huku,lakini tha tha tatizo kuutia humu majumbani kwetu kwa sasa ndo KIMEO,hiki ki kampuni chetu uchwara cha ZECO hakiwezi kitu,kila kitu kinategemea mzungu kutoka SOUTH wakati Bro TANESCO mambo anayaweza tu,jana mzungu katutestia naskia WAYA limeungua tena,Bro njoo bana tusaidie,huenda ikawa ZECO wanaona noma kukuomba msaada wako,hii tabu sijawahi kuisikia mikoani huko,hata ka kuna tatizo kubwa,basi huwa ikichukua nuda mrefu basi 5 days,sasa habari zinazotokea huko kwa ZECO huenda ikawa mpaka JANUARY katikati,kwani ZUNGU limeenda kula X-MASS south....HALI MBAYA BRO' njoo.
 
..Sheria za bahari zinasema...



..

..Raisi Museveni naye anazungumzia jambo hilohilo...
Kwa mujibu wa Museveni Tanganyika na Zanzibar ni Nchi zinazohitajiana. Kufutwa kwa mpaka pale Chumbe kueleweke kwa mantiki hii na siyo favour kwa Wazanzibari. Nanyi Mnatuhitaji Bwana. Hilo analolizingumza Museveni peke yake linawachachafya-achilia mengine mengi yaliyopo. We are partners and not subbordinates
 
Jamani,
Mwungano hauhitaji marekebisho. Mwenyezi Mungu kisha take care. Mmesikia global warming? Zanzibar itazama baharini kwa muda usiotimia miaka 50 ijayo. Hawa tunawakaribisha bara bila visa. Na mafuta yatakuwa yetu sote.

Shughuli pevu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom