Maonyesho ya viwanda ni kichekesho

Maonyesho ya viwanda ni kichekesho

Hata hao UDSM ukienda kwenye mabanda yao utakuta wana concrete mixer na mashine za kusaga unga 😀😀, vitu ambavyo watu wa jua kali wanatengeneza - Pathetic

Tatizo la Tanzania ni strategic planning, kila mtu anayeingia anafanya ya kwake bila mkakati endelevu. Nchi zilizoendlea kiviwanda zilijiwekea mikakati na implementation program ambazo zinafanyiwa assessment from time to time. Kwa mfano india ina entrepreneurship development program kwa vijana ambao ndo wanakuja kuwa wawekezaji wa baadae, Small industries development program, Land allocation, skill upgrading progrm nakadharika.
Sisi mtu ametoka kupiga pushapu jukwaani anakuja na wimbo wa viwanda ambao hata yeye haujui
 
Viwanda vya kucharanga wapinzani mapanga na kuwamiminia AK 47
 
Wakuu,

Jana nilienda sabasaba kuangalia maonyesho ya viwanda, orodha ya viwanda nilivyo vikuta kule:

1. TBC
2. University of Dar es Salaam
3. Waagiza solar kutoka nje ya nchi na kuuza nchini
4. Waagiza incubator na mashine kutoka china kuleta nchini
5. Wauzaji wa bidhaa za kilimo kutoka Kenya
6. Wanaonunua asali wanapack nyumbani na kuja kuuza, hii haina tofauti na vyerehani vinne.
7. Viwanda vya ukweli ni Bakhresa, Nyumbu, watengeneza viatu pamoja na watu wa food processing kama tomato (red gold) nk

Maonyesho haya yaonekane kama changamoto kwa taifa, haiwezekani importers nao waende kwenye maonyesho ya viwanda wakati wao wanaagiza tu na kuuza. Wakuu ukweli ni kwamba Tanzania ya Viwanda bado, hamna viwanda kabisa.

Serikali ipunguze sehemu ya bajeti yake inayotumika kununua wapinzani na hizo pesa wapewe mikopo watu wenye nia ya kuanzisha viwanda.
Ni uongo mtupu , hakuna maonyesho ya viwanda pale , mimi na mameneja wangu wa kanda tulifuatwa kupeleka bidhaa zetu lakini tukakataa ili kulinda heshima ya kiwanda chetu .
 
Viwanda vitajengwa kwa matendo na siyo maneno.
Mawazo ya kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda yatafsiriwe kivitendo, sekta binafsi ipewe motisha kwa kuanzia.
 
Uko sahihi Comrade

Ingawa umeongea uchochezi....kesho fika ofisi ya uhamiaji kwa mahojiano

Viwanda vinahitaji steps
1. Raw Material
2. Strategic Plan
3. Action Plan
4. Monitoring and evaluation Plan
5. Resources kama ardhi, mtaji, skills n.k

Kinyume chake
Hatuwezi kufanikiwa
 
Ukimkuta mtu anazungumzia viwanda bila kutaja chamzo cha umeme/ power, malighafi/kilimo cha kisasa na yahusuyo, soko na mtaji .jua huyo anadanganya wenzake/au anajidanganya mwenyewe ili kujifurahisha. Angalia bajeti yetu ya kilimo itakujibu, angalia uwekezaji kwenye kilimo, angalia wataalam wa kilimo na angalia chanzo cha umeme wetu. Kumwambia tu abood yule wa moro kwamba utamnyang'anya viwanda haimanishi lolote kwenye uchumi wa viwanda. Wala hamsemi hata aina ya viwanda mmekazana na idadi kama shule za kata. Jana kulikuwa na habar kwamba wafanya biashara hawakopesheki kwa kuwa mabenk yamebadilisha masharti ( kifupi serikali.inahodhi pesa) hivyo viwanda atafungua nani? Zama hizi serikali inafikiria kufanya biashara?
 
Back
Top Bottom