Maoni yangu kwa Vyombo vya Usalama

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,221
Ninavipongeza vyombo vyote vya Usalama pamoja na mifumo yote ya usalama wa Taifa la Tanzania.

Kazi yetu iliyotukuka na inayoogofya hata kusimuliwa hapa ndio ujasiri wetu kama Taifa.

Kuna Jambo linataka tokea na huenda Jambo hili lisipoangaliwa kwa umakini tunu za Taifa hili zitakuwa ni wimbo katika midomo ila matendo hakuna.

Kama kuna Jambo linatutisha Sisi tulio nje ya uwanja ni chuki, ukabila, udini, undugunaisation , upendeleo wa wazi, Uhuru na haki ya watanzania kama ilivyo ainishwa ktk katiba not otherwise.

Haya mambo yamepata mpenyo mkubwa Sana ktk utawala wa awamu ya tano. Tuseme kweli hatuwez pinga tawala zingine zilikuwa na hayo mambo Ila this time yamekuwa Kwa sauti kubwa Jambo Lina Tishia Sana umoja wetu, undugu wetu na utaifa wetu.

Lugha zinazotumika katika siasa iwe Kwa wapinzani au chama tawala kiukweli zinatisha zinatishia umoja wa Taifa letu. Sorry nitatoa mfano wa dhahiri kabisa mfano kitendo cha Mh Spika kumpa fursa Fursa Mch na Yule Mch kutumia lugha ya kuudhi kusema kelele za Mbwa while akijuwa mbwa ni haram Kwa waislam na hao mbwa wanaweza Kuwa watu wema ktk kushauri ni mojawapo ya mambo yanatishia uhai wa umoja wetu.

Ni lazima mlimulike hili ili kuliokoa Taifa.

Tumejiwekea malengo makubwa katika kujenga Taifa Ila nilazima tukumbuke pasipo umoja pasipo kusikilizana kama Taifa tunaweza kujikuta tunakuwa kama Ethiopia.

Najua miaka hii mitano itakuwa sio mirahisi kama wengi wanavyodhani vuguvugu la uongozi ndani ya chama tawala na nje litavuma sana hivyo kama idara liangalieni hili Kwa ustawi wa Taifa.
 
Jambo kama hilo unapaswa kuweka na ushadi ili kujitenga na porojo za kila siku mitandaoni.
 
Ni hivi, Gwajiboy hakupewa ile nafasi kwa kushtukizwa, lazima alishaambiwa kuwa yeye ndo atatoa comment fupi ya hotuba ya Rais, akajiandaa akachagua maneno yake mapema tu.

Lakini huyo ndo amewahi kutukana dini ya kiislamu akiita ya Majini, Akatukana Ukatoliki akaita ni dhehebu la mpinga Kristo, Ila amewezeshwa tu na System awe pale alipo bila kujali kuwa uwepo wake pale ni divisive, yaani umeweka ufa kati ya wananchi na serikali .
 
Watakunanga lakini umenena ukweli tupu . ila ujue Taifa lilipofikia neno usalama wa Taifa ni rahisi kulitamka ila kiukweli hii Tasisi ipo kulinda maslahi ya Chama fulani iwe jua au mvua.

Kama unataka kuongelea Taifa sahau. Ufisadi mkubwa mkubwa ukiwemo aliotaja Mkapa kwenye Kitabu chake jiulize usalama walikuepo ama hawakuepo?

Angalia uchaguzi ulivoendeshwa kura ziko kwenye migongo ya mabegi ya manjata je usalama wapo au hawapo?

Angalia madudu yote ya ufisadi mbali mbali je usalama upo ama?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Siku zote mwanasiasa anaongea kitu kitakacho wakera wapinzani wake na kuwafurahisha upande wake.
 
Mnaomkandia huyu jamaa ina maana hamuoni mpasuko kwenye jamii yetu kwa sasa?

Kuna mdau kasema huko mpanda kuna soko wauzaji na wanunuaji wamepangiana kutokana na vyama, kipande cha CCM, ACT, CHADEMA na hakuna anayeenda kwa mwingine, mtandaoni siyo kama zamani uchaguzi ukiisha watu wanasahau hii ya sasa inaonekana ni level nyingine kabisa tupo.

Niko Twitter kule naona hata jamaa wa Mtwara wana mashabiki kabisa wakisema ndiyo wakombozi wao, nyie mnaona sawa haya?
 
Punguza chuki mkuu.

Huyo mtu unaemzungumzia (Gwajima) alinukuu kutoka kwa mwanafalsafa flani, na amemtaja.

Nikawaida yetu sisi binadamu kujifunza kutokana na fikra zinazoishi. Hata ukifa Leo fikra zako tunazihitaji.
 
Back
Top Bottom