Maoni yangu kwa album ya Harmonize (High School)

man pog

Member
Apr 8, 2020
13
16
Mimi ni chizi muziki napenda kila aina ya muziki najua mziki mzuri na mbaya.

Tukianza na ushabiki mimi ni timu Diamond

Yani Simba namkubali kindaki ndaki ata akifanyaga upuuzi huwa naona sawa tu. Ila niwe mkweli tuu leo nimesikiliza album ya Harmonize aisee huyu jamaa ni noma katika nyimbo 17 nimependa nyimbo kama 10.

Mara nyingi wasanii wa bongo wakitoa album unaishia kupenda 3 mpaka 5. Yaani toka waanze kutoa maalubam yao ukiacha ile ya darasa basi hii itakuwa ya pili kuipenda.

Nimegundua kitu kwa Hamo, Harmonize hana sauti nzuri ya kuvutia ila ni fundi mzuri wa kucheza na melody. Ndo mana pia tunamuana anafanya vizuri kwenye amapiano na kwenye hii album amenisibitishia hilo kupitia nyimbo yake ya singeli alo imba kiingereza.

Na chakumalizia ni kwamba jamaa naona anaharibu tu kwenye video yaani anakuwa ajiongezi kabisa anashindwa hata na MARIOO.

Audio worldwide halafu video za kawaida.

1636116242294.png
 
Mimi ni chizi muziki napenda kila aina ya muziki najua mziki mzuri na mbaya.

Tukianza na ushabiki mimi ni timu Diamond

Yani Simba namkubali kindaki ndaki ata akifanyaga upuuzi huwa naona sawa tu. Ila niwe mkweli tuu leo nimesikiliza album ya Harmonize aisee huyu .
Jamaa yuko vizuri kikubwa hapo anatakiwa awe na crew ambayo itakuwa inamdesignia namna ya video games of qualities.
Naomba kuwasilisha
 
Kusema ukweli Harmonize ni mmoja ya wasanii ambao hakika anazidi kuniprove wrong.... mwanzo alipotoka kwa Diamond sikufikiri kama atafanikiwa kusimama..... lakini alinishangaza kwa kutoa moja ya Album bora kabisa kwa mwaka 2020.

Lakini alivyotangaza kutoa album nyingine mwaka huu nilipata mashaka sana....kwani niliona ni mapema sana.. lakini naendelea kuisikiliza album yake kwakweli ni album nzuri sana.... japo kuna mapungufu kwani si parfect album lakini album ina nyimbo nyingi nzuri na hit Song..
Nimezipenda
mdomo ft ibrah
SERIOUS LOVE- HASA BEAT
-Mtaje..
-USIA
-sORRY
 
Kondeboy ni fighter af mtu wa Wana Sana , kutojifungamanisha na wadada Sana kama ilivyozoeleka Kwa wanamziki wa WCB kumempa hipe Kwa Wana wa kitaa, kwenye vijiwe vya washikaji Kondeboy anakubalika kinyama
Acha bla bla timu Masifa, we tupe maoni kuhusu album, kuwa mtu wa wana hata Mbowe ni mtu wa wana😁😁😁😁
 
Album yake mbovu.. sijaona nyimbo ya maana walau moja.

Content kubwa kwenye album ni Diamond na Rayvanny bila hivyo hali ingekuwa mbaya zaidi.
haya twambie hizo nyimbo zipi wametajwa hao watu kama sikosei ni moja tu

Kunya anye kuku akinya bata kaharisha mara ngapi konde anapondwa lakini hamsemi
 
Kondeboy ni fighter af mtu wa Wana Sana , kutojifungamanisha na wadada Sana kama ilivyozoeleka Kwa wanamziki wa WCB kumempa hipe Kwa Wana wa kitaa, kwenye vijiwe vya washikaji Kondeboy anakubalika kinyama
Hata mimi nimeliona ila kosa analo lifanya kukimbilia kupiga show nje, wakati ndani anahitajika sizani kama anashindwa kuorganize show za label yake na kuwachukua baadhi ya wasanii wachache hata watano wanao fanya vizuri, andae show kwenye viwanja vikubwa apige hela.

Mziki ulivyo wakati unavuma ndicho kupindi cha kupiga hela,ukikukataa unahesabu mavuno yako uliyo yapata.Nandy naona kwa miaka miwili amevuna hela kupitia show anazo ziandaa yy mwenyewe.
 
Back
Top Bottom