Maoni ya Hussein Bashe bungeni kuhusu TTCL

Sasa huyu anataka treasury registrar aajiri inamaana serikali kwenye Mashirika ya reli, umeme, maji, Mawasiliano, matibabu, viwanda muajiri awe mmoja hivi huyo muajiri anakua na utaalamu gani wa kujua sifa na vigezo vya watu wote hao wakati fani yake ni uchumi?

Gawa majukumu kwa kila mtu ili kuwe na ufanisi waziri sio mjumbe wa nyumba 10/10

Lakini unaweza kushangaa watu wanaona anaongea points kumbe pumba tu, nimejua yaani kama utakua unapinga tu masuala Bungeni ndio nyumbu wanakuona wa maana bila kujali kipi unapinga na uhalali wake
Kazi ya mchumi ni kuulinda na kusimamia uchumi. TTCL ni taasisi ya kibiashara inayopanga na kujiendesha kichumi. Huyo waziri aliyesoma HGL wapi na wapi na biashara? Au umekariri ukishakuwa waziri kila kitu unaweza? Hiyo ofisi unayoiponda inasimamia mashirika mengine ndio yenye wataalamu wa kutosha. Unataka shirika liendeshwe kwa utashi au weledi?
 
Safi sana Mh. Bashe...@ttcl & TCRA kumejaa utumbo tu, mpaka wawe serious, otherwise wataendelea na ubabaishaji wao na kufanya kazi kwa mazoea..
Kuhusu Bodi sijuwi kama watakubali, maana pale ndipo wanapeana ulaji na maposho yasiyo na mbele wa nyuma, kama hatutabadilika tutabikia vile vile miaka nenda miaka rudi...
 
CCM tumekamilika kila idara, hapo Bashe anakesha akijisomea nondo, akifika bungeni anashusha nondo tupu. Huku kuna Milinga na Lusinde wakiinuka wanatukanatukana mitusi wanakaa. Mtakatizia wapi
 
TTCL wapo ICU nilishangaa jamaa walikuna kufunga internet ofisin wakasema ofisi imezungukwa na miti mingi ndo maana network haipatikani vizuri labda tukate miti. Pumbavu zao tulipoenda kuchukua internet ya Airtel ikafanya kazi vizuri sana na wakasema wao wanapata internet kutoka TTCL
 
Kazi ya mchumi ni kuulinda na kusimamia uchumi. TTCL ni taasisi ya kibiashara inayopanga na kujiendesha kichumi. Huyo waziri aliyesoma HGL wapi na wapi na biashara? Au umekariri ukishakuwa waziri kila kitu unaweza? Hiyo ofisi unayoiponda inasimamia mashirika mengine ndio yenye wataalamu wa kutosha. Unataka shirika liendeshwe kwa utashi au weledi?
Katiba ya Tanzania sifa kuu ya waziri lazima awe mbunge na si awe na taaluma ya Wizara anayoiongoza
 
Kazi ya mchumi ni kuulinda na kusimamia uchumi. TTCL ni taasisi ya kibiashara inayopanga na kujiendesha kichumi. Huyo waziri aliyesoma HGL wapi na wapi na biashara? Au umekariri ukishakuwa waziri kila kitu unaweza? Hiyo ofisi unayoiponda inasimamia mashirika mengine ndio yenye wataalamu wa kutosha. Unataka shirika liendeshwe kwa utashi au weledi?
Appointing za wizarani zinatolewa na waziri husika akishauriwa na wataalam wa wizarani akiwamo katibu Mkuu ambao ndio wabobezi katika fani ya mteuliwa, huko treasury anashauriwa na nani? Au ndio hiyo one man show?

Hivi kwa akili yako robo TTCL itahitaji mchumi zaidi kuliko mbobezi wa masuala ya Mawasiliano na namna ya uendeshaji wa makampuni ya Mawasiliano?

Mashirika yote ya serikali ni uchumi tu? TFDA, TBS, TANESCO, MSD hawa utakua unateua wachumi?
 
Sasa huyu anataka treasury registrar aajiri inamaana serikali kwenye Mashirika ya reli, umeme, maji, Mawasiliano, matibabu, viwanda muajiri awe mmoja hivi huyo muajiri anakua na utaalamu gani wa kujua sifa na vigezo vya watu wote hao wakati fani yake ni uchumi?

Gawa majukumu kwa kila mtu ili kuwe na ufanisi waziri sio mjumbe wa nyumba 10/10

Lakini unaweza kushangaa watu wanaona anaongea points kumbe pumba tu, nimejua yaani kama utakua unapinga tu masuala Bungeni ndio nyumbu wanakuona wa maana bila kujali kipi unapinga na uhalali wake

Yaania Registrar ndio mwenye mali kisheria, swali utakuwaje mwenye mali wakati uwezi kusimamia mali??? wanasiasa wanayo nia lakini wanatia mikono yao hawataki kutoka asilimia mia waziri siku hizi pia hanauhakika na kesho yake lakini msajili yuko siku zote mbona raisi ni mmoja.

Anza kugawa majukumu ya raisi kwa kuleta katiba mpya uone Pogba na timu yake anavyosimamia vidole gumba. Bashe hapingi ananatimiza wajibu wake wa kufikiri tofauti na wewe ebu anza kufikiri tofauti uone raha ya maisha. Umeshadumisha sana fikra za mwenyekiti ebu weka na fikra zako uoene kama atuendi hata Dr. Louis kakushinda na katoka nje ya box na ametusua.
 
Laiti kama wabunge wote wa CCM wangekuwa kama Bashe................Tungekuwa mbali!
 
Yaania Registrar ndio mwenye mali kisheria, swali utakuwaje mwenye mali wakati uwezi kusimamia mali??? wanasiasa wanayo nia lakini wanatia mikono yao hawataki kutoka asilimia mia waziri siku hizi pia hanauhakika na kesho yake lakini msajili yuko siku zote mbona raisi ni mmoja.

Anza kugawa majukumu ya raisi kwa kuleta katiba mpya uone Pogba na timu yake anavyosimamia vidole gumba. Bashe hapingi ananatimiza wajibu wake wa kufikiri tofauti na wewe ebu anza kufikiri tofauti uone raha ya maisha. Umeshadumisha sana fikra za mwenyekiti ebu weka na fikra zako uoene kama atuendi hata Dr. Louis kakushinda na katoka nje ya box na ametusua.
Mali ni ya umma au ni ya mtumishi wa umma? Sheria gani inasema Mashirika ya umma ni mali ya registrar?

Hata Rais anavyoteua kila mtu ipo kisheria na kikatiba the same way to the minister anateua akishauriwa na wataalam wa wizarani akiwamo katibu mkuu wa wizara.

Registrar ni kama commissioner wa TRA kisa yeye anakusanya kodi ndio apangie matumizi kodi?
 
CCM tumekamilika kila idara, hapo Bashe anakesha akijisomea nondo, akifika bungeni anashusha nondo tupu. Huku kuna Milinga na Kusinde wakiinuka wanatukanatukana mitusi wanakaa. Mtakatizia wapi

Halafu wote, mwenye kukesha akisoma na anayeinuka kutukana na kukaa wanalipwa posho ile ile kwa kodi yako, yangu na ya yule! Only in Tanzania!!!
 
Mali ni ya umma au ni ya mtumishi wa umma? Sheria gani inasema Mashirika ya umma ni mali ya registrar?

Hata Rais anavyoteua kila mtu ipo kisheria na kikatiba the same way to the minister anateua akishauriwa na wataalam wa wizarani akiwamo katibu mkuu wa wizara.

Registrar ni kama commissioner wa TRA kisa yeye anakusanya kodi ndio apangie matumizi kodi?

Umma uliuona wapi, katika kazi na sifa za kiongozi mojawapo ni figure head hii ni kazi ya asili ya kiongozi maana yake kiongozi au afisa husika ndiye anayewakilisha umma, sababu umma haupo katika kuendesha mali. Hapa jifiche aibu yako ya kutokujua ili ujifunze zaidi na uongozi. Hata ukisema nchi ni fictitious, raisi akisimama ndio nchi hiyo. Ukiambiwa msajili wa hazina kwa mamlaka aliyopewa yeye ndio anakuwa umma kwa nafasi na kwa mujibu wa sheria iliyomuweka. Registrar ni msajili sio sawa na commissioner wa TRA ebu dogo ingia chaka usome kidogo ili ukija tuone uko dip hata kidogo.
 
Ttcl imejaa wababu na wabibi wa kikoloni yaani ilitakiwa wapigwe chini wote tupia vijana wa Tehama wenye damu changa tupia mkurugenzi anayejua mambo ya kidigital muone moto mbona hawa voda na tigo watasanda.
 
Sasa huyu anataka treasury registrar aajiri inamaana serikali kwenye Mashirika ya reli, umeme, maji, Mawasiliano, matibabu, viwanda muajiri awe mmoja hivi huyo muajiri anakua na utaalamu gani wa kujua sifa na vigezo vya watu wote hao wakati fani yake ni uchumi?

Gawa majukumu kwa kila mtu ili kuwe na ufanisi waziri sio mjumbe wa nyumba 10/10

Lakini unaweza kushangaa watu wanaona anaongea points kumbe pumba tu, nimejua yaani kama utakua unapinga tu masuala Bungeni ndio nyumbu wanakuona wa maana bila kujali kipi unapinga na uhalali wake
Umumuelewa Bashe?? Unajua kzi ya board of directors?? Unajua wanatakiwa wawe na sifa zipi??
 
Back
Top Bottom