Maoni ya Dr. Azaveli Lwaitama Juu ya Lowassa Kuingia UKAWA

Maoni ya Dr. Azaveli Lwaitama Juu ya Lowassa Kuingia UKAWA

Je, Lowassa atakaposimika mfumo wake ndani ya CDM na hatimaye CDM wakashindwa kumfuga Lowassa, kitu gani kitatokea? Naona wanazuoni wanataka kuhadaa Watanzania na nadharia zao za kipuuzi.Mwanzoni walituletea nadharia kwamba upinzani hautaweza kuchukua dola toka CCM hadi watakapoungana. Leo hii wapinzani wameungana na aliyewaunganisha siyo Lowassa. Na mchezo unaoendelea sasa siyo kwamba upinzani utamtumia Lowassa kuingia ikulu bali Lowassa atautumia upinzani kuingia ikulu. Je, Lwaitama anashindwa kujua hilo?
 
Lowasa kaondoka CCM ,ila kila uchao tunaona wagombea wa ccm wanakamatwa na rushwa ,wana toana ngeo ni uroho wa madaraka tuwakatae hawafai
 
Jamaa kaandika vizuri sana, hamana mahali upinzani pure umewahi kuchukua madaraka kwa amani pasipo kwanza kupasu chama tawala! Ccm wanajua sasa hivi ngoma ni nzito walitarajia wapinzani watendelea kuimba ufisadi tu wakisubiri mtakatifu aingie ikulu! Mungu hafanyi kazi yake kama wanadamu wanavyo fikiri ni lazima jambo la Mungu liwashangaze wanadamu na ndivyo hata hili limewashangaza maana kwa akili za kibinadamu likikuwa haliwezekani! Yasiyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yote yanawezekana! Kama walidhani walipokuwa wanasema nibmpango wa Mungu walidhani Mungu atajibu kama wanadamu! God has proven that He is the only Him!

Ngonini 100% umenikosha maneno kuuuuuuuntuuuuu!!!!
 
Last edited by a moderator:
usafi gani huo mkuu mlio nao ccm?

watoeni na weziwa EPA,KAGODA,MELEMETA,ESCROW na wezi wengine ambao hawajulikani mbele ya umma.

watoeni na hawa wanaokamatwa na takukuru wakitoa rushwa kwenye kura za maoni. naibu waziri,nape chambiri

hivi hata escrow aliyeiba alikuwa lowasa?

chenge,tiba,mnikulu,ngeleja, na wale wa stanibic

nani msafi ndani ya ccm?

huyo jamaa naona hajielewi,,, ufisadi wa ccm ni mfumo, na ndomaana hata baaada ya lowasa kujivua uwaziri mkuu bado madudu lizidi shamili ndani ya serikali, kama vile dowans, escrow , gasi nk. Napia inshu ya richmond imepatiwa ufumbuzi kuwa kuna cheo ndani ya serikali kina itwa KATIBU MKUU KIONGOZI ana nguvu zaidi ya waziri mkuu, na hiki cheo ndo source ya kutokuvujwa kwa mkataba wa richmond na bwana lowasa akiwa waziri mkuu
 
Dr.Slaa, Mbowe, Mnyika, Lema, wanatakiwa kikiri mbele ya watanzania kuwa wanakula matapshi yao lakini hawana budi kuungana na Lowassa.
 
Huyu mzee nampenda anaunga mkono mabadiliko bila masharti kweli anayo dhamira ya kuiondoa CCM madarakani. Tutamkaribisha kwenye mkutano mkuu aje kutoa muhadhara.
 
hao wote ni team lowasa, JP akichukua dola lazima wapande kisutu, EL anaomba siasa za kistaarabu mwambieni hazipo, mafisadi yote lazima yaende segerea.

Kuhusu huyo JP, the infamous appropriation of government quarters/properties remains the biggest corruption scandal this country has ever witnessed. JP's nomination as CCM's flag-bearer was a myopic strategy aimed at ensuring that this passes with impunity. Alas, no stone will be left unturned!!
 
Dr.Slaa, Mbowe, Mnyika, Lema, wanatakiwa kikiri mbele ya watanzania kuwa wanakula matapshi yao lakini hawana budi kuungana na Lowassa.

Mbona Akina Nape na CCM mlisema ajivue gamba na marafiki zake wawili yaani Rostam na Chenge, sasa imekuwaje mnakuwa wasahaulifu hivyo, halafu List of Shame hadi JK yupo mbona hamsemi huyo.
 
Kumeguka kwa CCM-Mambo Leo kama taasisi ya kakundi kawana mtandao ulioingiza serikali ya sasa ya Tanzania madarakani mwaka 2005 ni faraja kwa wote wenye kuitakia mema nchi hii na ni kiashiria cha kukomaa kwa vuguvugu la ukombozi wa pili wa Tanzania utakao chukua sura ya demokrasia zaidi ilikuwa na na maendeleo endelevu zaidi yapatikane kupitia kupatikana nafasi chanya zaidi ya kupitishwa kwa Katiba Mpya kama ilivyopendekezwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza vyama vy siasa vya upinzani kiuhalisia ( tofauti na vile ambavyo vimebebwa na watawala wa sasa kwa lengo la kuua upinzani wa kisiasa kijanja kijanja kama ACT- Wazalendo) sasa vimeunganishwa na kupigania Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Warioba ( UKAWA) badala ya kuunganishwa na kutaka kuondoa CCM madarakani pekee.

Patamu sana hapo
 
Wanazuoni uchwara tu hawana lolote. Kazi kupalamia siasa na vyuo vyao kuishia kuporomoka! Fanya kazi mliyotumwa hatutaki kuona mnawaadaa wananchi kawaadae wanafunzi wenu.
 
Hiyo mifano kawadanganye nayo watoto wa social science mwaka wa kwanza.
 
Wanazuoni uchwara tu hawana lolote. Kazi kupalamia siasa na vyuo vyao kuishia kuporomoka! Fanya kazi mliyotumwa hatutaki kuona mnawaadaa wananchi kawaadae wanafunzi wenu.

Asilimia 80 ya wanafunzi wake hawana kazi...huyu mzee ni laana
 
Nilimpinga sana Lowasa,nilipofikiria hili nimeona ni jambo la kheri kumuunga mkono Lowasa.Mkuu Bukanga nipe link ya Wanabidii

Siyo wewe tu uliekuwa unampinga Lowasa, hata mimi pia nilikuwa mmojawao. Tukisema tusubiri tuingie ikulu hivihivi kwa kusema tuwatumie watu "wanaoitwa wasafi" tunaweza ngoja mda mrefu sana. Kanuni ya kwanza kabisa ni kuitoa CCM madarakani kwa namna yoyote ile (iwe ni kwa sanduku la kura au kijeshi). Kanuni ya pili ni kuanza kuisafisha na kuitengeneza hii nchi ambayo imekwisha haribiwa na CCM. Baada ya kuiondosha CCM madarakani ndo nitaangalia nijiunge na chama gani. Kwa sasa mimi ni mshabiki wa CHADEMA tokea nilipoanza kupiga kura mara ya kwanza mwaka 2000.
 
This is perfect at this moment our mother Tanzania needs..
 
Mbona Akina Nape na CCM mlisema ajivue gamba na marafiki zake wawili yaani Rostam na Chenge, sasa imekuwaje mnakuwa wasahaulifu hivyo, halafu List of Shame hadi JK yupo mbona hamsemi huyo.
Kama JK yupo ndiyo nini si mwambieni Dr.Slaa aende mahakamani kama alivyosema fisadi Lowassa.
 
Back
Top Bottom