Maoni ya Dr. Azaveli Lwaitama Juu ya Lowassa Kuingia UKAWA

Mzee umemaliza tunasubiri kuapishwa
Dr. Ni mmoja wa waliokuwa wakiitwa wasomi uchwala na rais mkapa. Lakini pengine naye ni sawa tu na kingunge. Anatumia theory nyingi za wakati huo kusolve kila tatizo la wakati huu. Mwalimu aliwahi kusema ni uchizi kubadirisha kipande chako cha almasi kwa kipande chenye ukubwa sawa na kinachong'aa kama alimasi lakini kikiwa ni chupa.
 
Ukimsikiliza lwaitama, nakua na wasiwasi na uelewa wako
 
CCM ni wasafi,kama unaushahidi wa maovu yao nenda mahakamani or else shut up!

Umemaliza kazi mkuu.Hawa jamaa sijui hawana akili au wamelewa.Kwa Lowasa wanadai tuhuma na haijathbitishwa popote na mahakama, je hao wa Escrow wamethbıtishwa na mahakama?In a simple way CCM hakuna fisadi zaıdı ya Mramba na Yona!
 
CCM haijameguka akili zako ndio zimemeguka kwa kuona lowasa kajivua gamba kwa ufisadi sasa CCM imebaki cream safi kama imezaliwa leo safi kabisa CCM.

Pole ndugu yangu kwa kusema eti ccm ni wasafi baada ya lowasa kuihama.hivi maescrowers mtawapeleka wapi?
 
Dr. Ni mmoja wa waliokuwa wakiitwa wasomi uchwala na rais mkapa. Lakini pengine naye ni sawa tu na kingunge. Anatumia theory nyingi za wakati huo kusolve kila tatizo la wakati huu. Mwalimu aliwahi kusema ni uchizi kubadirisha kipande chako cha almasi kwa kipande chenye ukubwa sawa na kinachong'aa kama alimasi lakini kikiwa ni chupa.

Hongera, kuna watu mnaongea points humu mpaka nafurahı.Hayo mambo hayawezi kueleweka kwa watu ambao wameshkwa akili zao na mtu km Mbowe.Nchi bado ına hazına kubwa ya watu km wewe wenye uelewa.
 
Wewe ni mwenzangu.Nilimpinga sana Lowassa, na niliwahi tamani akiteuliwa na CCM, basi niukane na Utanzania wangu.

Lakini pamoja na kuwa yeye kwake kama yeye ana mapambano binafsi ya kutaka kuwa Rais iwe isiwe na kwamakubaliano yao na JK. Sisi kwa upande wetu kama raia wema,tutumie upenyo huo kuondoa chama dhalimu CCM na syndicate yake yote. Amini ninawaambia tutaanza mwanzo mzuri sana na mtashuhudia Tanzania nyingine kabisa yenye democrasia ya kweli, tutaheshimiana na unafiki wetu wote utaanza kwisha na tutapata maendeleo ya kweli na kuheshimika sio tu Africa bali duniani kote.

Kubwa zaidi tuombe mungu sana uchaguzi uende salama na CCm wakubali kukabidhi madaraka kwa amani ili tuongeze heshima hiyo Tanzania kama nchi ambayo ilipata uhuru wake bila damu, haijawahi kupigana ama kwa kikabila ama dini na sasa inaingia transition nyingine kwa amani ya aina yake. Tunaomba jeshi letu ambalo limetokea kuwa Jeshi tukuka na lenye nidhmu ya hali ya juu Africa, lilinde heshima ya jina lake Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT) kushuhudia hii transition bila kujiingiza hata JK angesema nini na tunajua ni marafiki na Mkuu wa Jeshi. Kadhalika tunaliomba Jeshi letu la Polisi, pamoja na kuwa ni kweli limekuwa na upendeleo wa wazi na kuitwa PolisiCCm, sasa ni wakati wa kujipambanua. Simamieni usalama wetu wetu kwa kipindi chite hiki cha mpito ili tuweke historia.

HII NI HISTORIA YETU SOTE KAMA WATANZANIA UWE RAIA, ASKALI POLISI AMA JESHI NA SIFA NA UCHUMI UNAOKUWA UTAKAO FUATIA NI WETU WOTE NA VIZAZI VYETU. KWA NINI HATUTAKI KUWA SINGAPORE AMA KOREA NA UWEZO HUO TUNAO NA HATA ZAIDI?
 
Historia inaonesha kuwa vipindi fulani katika mstakhabali wa nchi unalazimisha kupima nini ni janga zaidi ya jingine. Marehemu Samora Machel na Frelimo walikubali kutia saini Mkataba wa Nkomati wa ushirikiano na Makaburu kama mkakati wa kujinusuru na kutoa nafasi kukabiri janga kubwa kuliko zote wakati huo la kuondolewa serikali ya Frelimo na Renamo ikisaidiwa na Makaburu. Wakomunisti wa Afrika ya Kusini waliingia ubia na ANC ya mabweneyenye weusi ili kutokomeza kwanza ukaburu na mapambano na ubepari yaje baadaye. Katika Vita Kuu ya Dunia ya Pili wakomunisti walishirikiana na mabwenyenye wa mrengo wa kulia na kati kutokomeza janga kubwa zaidi wakati huo la ufashisti, yaani ubepari wa mrengo wa wa kulia kupitiliza. Hivyo hivyo mapambano ya kuleta uhuru wa Tanganyika yalivyo unganisha nguvu za mabwenyenye wazungu na waasia pamoja na zile za wakulima na wafanyakazi wa rangi zote kwa azimio lile la mkutano wa mkuu wa Tanu wa 1958 pale Tabora. Hivyo hivyo Mandela na ANC waliingia "urafiki wa mashaka" na De Clerk kiongozi wamakaburu ili kuondolewa ukaburu kuwe kwa amani ya "kula matapishi" ya kuwalaani huko nyuma kuwa ni wabaya wa Mwaafrika!!

Mabadiriko ya haraka haraka yanayoendelea hapa Tanzania yenye lengo la kuondoa CCM madarakani kama chama dola kinachodumaza na kudhoofisha ushindani wa kisiasa miongoni mwa mabwenyenye watabaka tawala Tanzania ni mbadiliko yatayoleta neema kwa Watanzania wote. Ile tu CCM kudhoofishwa na kujiunga UKAWA kwa Lowasa ni kuvuja kwa pakacha ambayo ni nafuu ya mchukuzi.....Nikuondoa kizingiti kikuu cha kushamiri kwa demokrasia pana na maendeleo endelevu Tanzania ambacho ni kuhodhiwa na ukiritimba wa chama dola cha CCM kinachojinadi kama chama cha mrengo wa kushoto wakati ni chama cha mrengo wa kulia kama vyama vyote vya siasa Tanzania kwa sasa.

Kumeguka kwa CCM-Mambo Leo kama taasisi ya kakundi kawana mtandao ulioingiza serikali ya sasa ya Tanzania madarakani mwaka 2005 ni faraja kwa wote wenye kuitakia mema nchi hii na ni kiashiria cha kukomaa kwa vuguvugu la ukombozi wa pili wa Tanzania utakao chukua sura ya demokrasia zaidi ilikuwa na na maendeleo endelevu zaidi yapatikane kupitia kupatikana nafasi chanya zaidi ya kupitishwa kwa Katiba Mpya kama ilivyopendekezwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza vyama vy siasa vya upinzani kiuhalisia ( tofauti na vile ambavyo vimebebwa na watawala wa sasa kwa lengo la kuua upinzani wa kisiasa kijanja kijanja kama ACT- Wazalendo) sasa vimeunganishwa na kupigania Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Warioba ( UKAWA) badala ya kuunganishwa na kutaka kuondoa CCM madarakani pekee.

Ghafla mwanasiasa mwenye nguvu nyingi ndani ya chama cha kifisadi cha CCM, mwanasiasa ambaye umaaarufu wake umetokana na kuongoza mtandao uliouweka utawala wa sasa wa CCM madarakani, Ndugu Edward Lowasa, amekasirishwa na kukatwa jina lake na aliodhani ni rafiki zake ndani ya CCM na kuamua kusema basi na lolote liwe kwa kujiunga na vuguvugu la kupigania katiba mpya!! Naye sasa kang'amua kuwa Katiba ya sasa na ile Pendekezwa ni za ovyo maana haziruhusu kuwepo mgombea huru bila mizengwe. Hasira za Lowasa zimezaa tunda zuri la kug'amua kuwa Watanzania wanaitaji mabadailiko kupitia Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Hasira hizi za mkizi ni furaha ya kunguru na ni busara kwa viongozi wa Chadema na UKAWA kwa ujumla kutoongopa "kula matapishi yao" kwa kumkaribisha Ndugu Lowasa ...huyu huyu waliomwita fisadi... kujiunga na UKAWA na kugombea urais. Nafasi ya kihistoria imejitokeza ya kukiondoa CCM madarakani kwa amani!!

Sishangai wasaliti wa vuguvugu la kukiondoa CCM madarakani wanatushauri sisi Watanzania wenye shauku ya kuutumia upenyo huu wa mpasuko ndani ya CCM kukiondoa CCM madaraka!!!Eti tuombe radi kwa" kula matapishi yetu" wote tulio wahi kumwita Lowasa fisadi! Wao wanataka tuendelee kuvumilia kutawaliwa na CCM labda kwa miaka mitano au zaidi hivi mpaka chama kipya cha watakatifu kiitwacho ACT-Wazalendo kitakapo kuwa tayari kututawala badala ya CCM!! Sishangai kusikia ushauri huu kutoka kwa wasaliti hawa ambao kazi yao hata huko nyuma imekuwa nikuudhoofisha upinzani dhidi ya CCM na kukisaidia CCM kiendeleee kuwa madarakani!! Hawa jamaa ni wasomi sana na ni wajanja sana, ilo lazima kulikiri!!!

Sitashanga kama haya ninayoyasema yatapigwa madogo na wasaliti hawa!! Historia itakapoandikwa baada ya UKAWA kupata viti vingi zaidi Bunge lijalo au hata kuuchua urais na kupata Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba itawapa hukumu yao stahiki, wajanja na welevu hawa! Bila shaka wanaoomba UKAWA ishindwe kupata viti vingi Bunge lijalo na iukose urais na hivyo tuendelee kutawaliwa na CCM na wao wapate viti vya kutosha kuwa viongozi wakuu wa eti upinzani muruwa wenye maadili ya Azimio la Arusha Tanzania!! Ni haki yao ya binadamu kuendelea na matumaini haya kama na sisi tulivyo na haki ya kuendelea na matumani yetu ya uwezakano wa ushindi mnono chini ya UKAWA dhidi ya ukiritimba wa chama kimoja chama dola cha CCM!
Mwl. Lwaitama

Culled from Wanabidii..

Cc Mchambuzi Mzee Mwanakijiji Character X Mag3 Matola Ritz Lizaboni

Huyu mzee ukimsikiliza hata akizungumza unajua akili yake haiko sawa!Unapotezaje muda wako kuleta refernce zake hapa, nadhani kuna wasomi wengi tu wa kuwanukuu sio huyu aliyeshindwa hata kuandika majarida ya maana ili apande ngazi na kuwa professor kwa miaka zaidi ya 30 ndani ya chuo kikuu
 
Nakumbuka Mh. Joshua Nassari alipata ubunge wa Arumeru Mashariki kwa propaganda za ufisadi wa Lowassa.
Mh. Tundu Lissu amepata umaarufu na heshima zaidi kwa gear ya 'List of shame' ambapo EL ni mmojawapo.
Na hata Mh. Mbowe hadhi yake inapanda kila anapoonekana kuwapinga mafisadi ambao 'kiranja' wao alionekana ni EL maana ndiye alimtengeneza hata JK.

LAKINI:
Kitendo cha hawa watu kuja front na kumkubali EL bila hata woga kimetustua wengi.
Tafakari zaidi iliibuka pale Prof. Ibrahim Lipumba alipoamua kuachia kugombea urais baada ya kupitishwa na chama chake!
Confusion zaid iko kwenye uzi niliouona hapa aliopost Dr. Wilbroad Slaa dhidi ya kamanda mwenzake Yeriko Nyerere.

Haya matukio yote inabdi yatufundishe kitu kama wananchi 'tuliochanganyikiwa', na kama walivyosema akina Nassari, Lissu, Prof. Lipumba nk kuwa nao walichanganyikiwa hapo awali lakini wakatuasa kumsikiliza wenyewe Edward Lowassa na ndipo tuhukumu. Na hasa dhambi kubwa ya ufisadi wake ukiwa ni RICHMOND ambayo ndiyo anatakiwa aitolee ufafanuzi.
Baada ya kupitia andiko la Daktari Azaveri Lwaitama na mifano sahihi aliyotoa inayokidhi kiu ya yeyote mwenye kutafakari ni dhahiri katoa walao mwongozo ni wapi pa kuanzia kufikiri juu ya hili. Na wengi kama sio wote tunamjua Dr. Lwaitama kupitia mijadala yake kwenye media asivyo mchoyo wala mwoga kushare elimu yake na wengine.

CCM kuondoka madarakani wakati huu (KWA AMANI) kutaepusha matatizo mengi kwa Mtanzania wa kweli.

CCM haijameguka akili zako ndio zimemeguka kwa kuona lowasa kajivua gamba kwa ufisadi sasa CCM imebaki cream safi kama imezaliwa leo safi kabisa CCM.

Taja majina yote 11 ya mafisadi wa Mwembeyanga, kisha jiulize hao wengine wana usafi gani ukiondoa huyo anayewapa "hofu"
 
Huyu mzee ukimsikiliza hata akizungumza unajua akili yake haiko sawa!Unapotezaje muda wako kuleta refernce zake hapa, nadhani kuna wasomi wengi tu wa kuwanukuu sio huyu aliyeshindwa hata kuandika majarida ya maana ili apande ngazi na kuwa professor kwa miaka zaidi ya 30 ndani ya chuo kikuu
du, hataree!
Na huyo mwenye 'PhD' sijui tano na Professor tatu amewahi kuchapisha hata makala kwenye gazeti la uwazi au sani!?

CCM haijameguka akili zako ndio zimemeguka kwa kuona lowasa kajivua gamba kwa ufisadi sasa CCM imebaki cream safi kama imezaliwa leo safi kabisa CCM.

Cream safi wakati watuhumiwa wa escrow wapo mtaani wanapeta,
 
Historia inaonesha kuwa vipindi fulani katika mstakhabali wa nchi unalazimisha kupima nini ni janga zaidi ya jingine. Marehemu Samora Machel na Frelimo walikubali kutia saini Mkataba wa Nkomati wa ushirikiano na Makaburu kama mkakati wa kujinusuru na kutoa nafasi kukabiri janga kubwa kuliko zote wakati huo la kuondolewa serikali ya Frelimo na Renamo ikisaidiwa na Makaburu. Wakomunisti wa Afrika ya Kusini waliingia ubia na ANC ya mabweneyenye weusi ili kutokomeza kwanza ukaburu na mapambano na ubepari yaje baadaye. Katika Vita Kuu ya Dunia ya Pili wakomunisti walishirikiana na mabwenyenye wa mrengo wa kulia na kati kutokomeza janga kubwa zaidi wakati huo la ufashisti, yaani ubepari wa mrengo wa wa kulia kupitiliza. Hivyo hivyo mapambano ya kuleta uhuru wa Tanganyika yalivyo unganisha nguvu za mabwenyenye wazungu na waasia pamoja na zile za wakulima na wafanyakazi wa rangi zote kwa azimio lile la mkutano wa mkuu wa Tanu wa 1958 pale Tabora. Hivyo hivyo Mandela na ANC waliingia "urafiki wa mashaka" na De Clerk kiongozi wamakaburu ili kuondolewa ukaburu kuwe kwa amani ya "kula matapishi" ya kuwalaani huko nyuma kuwa ni wabaya wa Mwaafrika!!

Mabadiriko ya haraka haraka yanayoendelea hapa Tanzania yenye lengo la kuondoa CCM madarakani kama chama dola kinachodumaza na kudhoofisha ushindani wa kisiasa miongoni mwa mabwenyenye watabaka tawala Tanzania ni mbadiliko yatayoleta neema kwa Watanzania wote. Ile tu CCM kudhoofishwa na kujiunga UKAWA kwa Lowasa ni kuvuja kwa pakacha ambayo ni nafuu ya mchukuzi.....Nikuondoa kizingiti kikuu cha kushamiri kwa demokrasia pana na maendeleo endelevu Tanzania ambacho ni kuhodhiwa na ukiritimba wa chama dola cha CCM kinachojinadi kama chama cha mrengo wa kushoto wakati ni chama cha mrengo wa kulia kama vyama vyote vya siasa Tanzania kwa sasa.

Kumeguka kwa CCM-Mambo Leo kama taasisi ya kakundi kawana mtandao ulioingiza serikali ya sasa ya Tanzania madarakani mwaka 2005 ni faraja kwa wote wenye kuitakia mema nchi hii na ni kiashiria cha kukomaa kwa vuguvugu la ukombozi wa pili wa Tanzania utakao chukua sura ya demokrasia zaidi ilikuwa na na maendeleo endelevu zaidi yapatikane kupitia kupatikana nafasi chanya zaidi ya kupitishwa kwa Katiba Mpya kama ilivyopendekezwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza vyama vy siasa vya upinzani kiuhalisia ( tofauti na vile ambavyo vimebebwa na watawala wa sasa kwa lengo la kuua upinzani wa kisiasa kijanja kijanja kama ACT- Wazalendo) sasa vimeunganishwa na kupigania Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Warioba ( UKAWA) badala ya kuunganishwa na kutaka kuondoa CCM madarakani pekee.

Ghafla mwanasiasa mwenye nguvu nyingi ndani ya chama cha kifisadi cha CCM, mwanasiasa ambaye umaaarufu wake umetokana na kuongoza mtandao uliouweka utawala wa sasa wa CCM madarakani, Ndugu Edward Lowasa, amekasirishwa na kukatwa jina lake na aliodhani ni rafiki zake ndani ya CCM na kuamua kusema basi na lolote liwe kwa kujiunga na vuguvugu la kupigania katiba mpya!! Naye sasa kang'amua kuwa Katiba ya sasa na ile Pendekezwa ni za ovyo maana haziruhusu kuwepo mgombea huru bila mizengwe. Hasira za Lowasa zimezaa tunda zuri la kug'amua kuwa Watanzania wanaitaji mabadailiko kupitia Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Hasira hizi za mkizi ni furaha ya kunguru na ni busara kwa viongozi wa Chadema na UKAWA kwa ujumla kutoongopa "kula matapishi yao" kwa kumkaribisha Ndugu Lowasa ...huyu huyu waliomwita fisadi... kujiunga na UKAWA na kugombea urais. Nafasi ya kihistoria imejitokeza ya kukiondoa CCM madarakani kwa amani!!

Sishangai wasaliti wa vuguvugu la kukiondoa CCM madarakani wanatushauri sisi Watanzania wenye shauku ya kuutumia upenyo huu wa mpasuko ndani ya CCM kukiondoa CCM madaraka!!!Eti tuombe radi kwa" kula matapishi yetu" wote tulio wahi kumwita Lowasa fisadi! Wao wanataka tuendelee kuvumilia kutawaliwa na CCM labda kwa miaka mitano au zaidi hivi mpaka chama kipya cha watakatifu kiitwacho ACT-Wazalendo kitakapo kuwa tayari kututawala badala ya CCM!! Sishangai kusikia ushauri huu kutoka kwa wasaliti hawa ambao kazi yao hata huko nyuma imekuwa nikuudhoofisha upinzani dhidi ya CCM na kukisaidia CCM kiendeleee kuwa madarakani!! Hawa jamaa ni wasomi sana na ni wajanja sana, ilo lazima kulikiri!!!

Sitashanga kama haya ninayoyasema yatapigwa madogo na wasaliti hawa!! Historia itakapoandikwa baada ya UKAWA kupata viti vingi zaidi Bunge lijalo au hata kuuchua urais na kupata Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba itawapa hukumu yao stahiki, wajanja na welevu hawa! Bila shaka wanaoomba UKAWA ishindwe kupata viti vingi Bunge lijalo na iukose urais na hivyo tuendelee kutawaliwa na CCM na wao wapate viti vya kutosha kuwa viongozi wakuu wa eti upinzani muruwa wenye maadili ya Azimio la Arusha Tanzania!! Ni haki yao ya binadamu kuendelea na matumaini haya kama na sisi tulivyo na haki ya kuendelea na matumani yetu ya uwezakano wa ushindi mnono chini ya UKAWA dhidi ya ukiritimba wa chama kimoja chama dola cha CCM!
Mwl. Lwaitama

Culled from Wanabidii..

Cc Mchambuzi Mzee Mwanakijiji Character X Mag3 Matola Ritz Lizaboni

Lengo nikuing'oa hli genge La wanyang'anyi bungeni
 
CCM ni wasafi,kama unaushahidi wa maovu yao nenda mahakamani or else shut up!

hata usafi wa mavazi hawamo, kwenye wizi hamna atakayepona. mbona lowasa amewambia mwende mahakamani mmeufyata?
 
du, hataree!
Na huyo mwenye 'PhD' sijui tano na Professor tatu amewahi kuchapisha hata makala kwenye gazeti la uwazi au sani!?

Bora huyo hakuwa staff member wa academic institution, alipewa tu hizo sio huyu mhadhili mzoefu!
 
Back
Top Bottom